kauli kama hizi lazima zikutoe 'kipele kuku' neh | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kauli kama hizi lazima zikutoe 'kipele kuku' neh

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bei Mbaya, Mar 25, 2011.

 1. Bei Mbaya

  Bei Mbaya JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,265
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 160
  Nilikuwa nasoma habari iliyochapishwa katika gazeti moja kuhusu wananchi wa Kata ya Mwakibete jijini Mbeya ambao, chini ya Kamati ya Maendeleo ya Kata (KAMAKA) hiyo ya Mwakibete inayoongozwa na Diwani Lucas Mwampiki kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA, waliamua kiwango cha michango kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa shule za sekondari kiwe shilingi 3,000/= badala kiwango kilichozoeleka cha shilingi 10,000/=, kiwango ambacho Mkuu wa Wilaya hiyo, Evans Balama anakitambua .Sasa katika habari hiyo, ndipo nikabaki nastaajabia kauli hizi:“Mimi nimezaliwa ndani ya CCM, nimekulia ndani ya CCM, nimesomea ndani ya CCM, ninafanya kazi ndani ya CCM, hivyo sitakuwa tayari kuona vyama uchwara na sera zake uchwara ndani ya mamlaka yangu.”“Nina uwezo wa kukufanyia kitu chochote na jambo lolote kwa kuwatumia Usalama wa Taifa ili kukuondoa katika nafasi hiyo ya udiwani, japokuwa kufanya hivyo ni dhambi mbele za Mungu lakini nitamuomba Mungu anisamehe.”
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  H kauli chafu sana ila ni ulevi mkubwa wa madaraka ikizingatiwa Diwani ni mwakilishi wa wanainchi.
  Balama akajaribu kugombea udiwani tuone kama atapita mjinga mkubwa huyu.

  Hivi hawa wakuu wa wilaya wana umuhimu gani given DED +mameya/wenyekiti wa halmashauri wapo?
   
 3. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #3
  Mar 25, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Kuna baadhi ya kauli za wateule wa rais zinastaajabisha sana
   
 4. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #4
  Mar 25, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,393
  Trophy Points: 280
  hujiulizi watu wangapi wana uwezo wa kulipa hiyo sh 10 000 hapo kijijini?ccm haumuoni aibu mmeuza zain airtel kwa muhindi bhartel bila kuchukua kodi 450 bn?ingekua mimi hata thumni wasingelipa kama vile mrema alivyofutilia mbali kodi ya kichwa!shame on you!!
   
 5. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #5
  Mar 25, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,163
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Mungu hasemehi watu kama wewe, mnanenepesha matumbo bure subirini siku ya kiama mtaona.
   
Loading...