Kauli kali za Mrisho Mpoto

kazikubwa

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2010
Posts
597
Reaction score
151
Ndugu wana JF, mada hii naiweka hapa kwenye jukwaa la siasa licha ya kuwa mhusika wa mineno mikali ni mwana burudani mzuri. Mwimbaji nguli mwenye tamathali za semi, mwenye kauli kali zenye misimamo ya kisiasa amekuja na single kali yenye nukuu zifuatazo, kwa uchache ni:

1. Wazito wengi nchini wamekomaa sana ki mawazo na fikira. Lakini ukomavu wao upo kuanzia shingoni kwenda chini.
2. Aliahidi akipata nauli atakwenda kwa mjomba, lakini sasa hataki kwenda tena na hataki kuulizwa kwanini
3. Amechoka na ameshindwa kuvumilia jinsi hali ilivyo sasa nchini, waliokuwepo sasa tumewachoka, na hao wanaojiandaa
kuingia hatuwaamini kabisa, bora liwe hivyo hivyo liwalo na liwe.
4. Maneno ya kitoto kwa watoto ni utani tu, lakini maneno ya kitoto kuwaambia watu wazima ni upumbavu, hatutaki
kudanganywa.
5. Sisi tunachagua mavi ya panya kwenye mchele wewe unatuletea kuni zenye maji ili tupikie, hii ni dharau hatukubali.

Wadau maoni na mitazamo yenu kisiasa ni muhimu, naomba tutupie humu.
 
Uliwapaka wanja sasa wamekupaka pilipili machoni

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
Hahaa ila huyu jamaa huwa anaongeaga vitu vya maana saa zingine.
 
1.Ukipewa kipande cha nguru kabla haujakila muulize kaoshwa? kama hajaoshwa usile...
2.Chura anapenda maji lakini siyo ya moto
3.Chiriku mzee akamatwi kwa makapi
 
Reactions: awp
Nyoka hana kiuno ndo maana havai shanga---(shangazi ya mpoki)
 
Ukisikia buuu,ujue ni bomu. Kutumia roho za watu kama mtaji wa kisiasa ama.njia kuelekea ufukweni ni ujinga...Adela nyosha kidole!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…