Wakati wa kampeni ya uchaguzi wa mwaka jana Dr Slaa alisema kuirudisha CCM madarakani ni sawa na kujitafutia maafa. Hali inavyokwenda sasa Serikali imepigika, wananchi wamepigika. Mnaionaje kauli yake hii jamani ?
Na kwa hali hii tutegemee kuona vichapo vikiendelea kwa wabunge wa ccm katika majimbo mbalimbali.Utabiri umeshatimia, ndio maana hata majimbo mengi yaliyochagua wabunge wa CCM wameshaanza kuwachoka mapema kabisa.
Kwa upepo ulivyo ****** anaweza asifike 2015.
Watanzania wanauawa kama wanyama, hii haijawahi kutokea tangu utawala wa serikali ya awamu ya kwanza mpaka serika ya zama za uwazi na ukweli. madini yetu yanachimbwa na hawa maumbwa koko tukidai tunapigwa!
Kuna kila dalili ya mapinduzi kutokea Tanganyika sooner than later.
Freedom is coming!
-Kwa sasa Watumishi wa serikali wanakula mishahara ya mikopo toka mabenki ya biashara.
-Miradi mikubwa yote ya ujenzi mabarabara imeshasimama.
-Bei za mafuta ndiyo hizo.
Na Mimi NATABIRI sasa kuwa kutokana na ukata huu wa serikali, vyuoni kutakuwa na migomo na maandamano mingi sana kutokana na usanii utakaofanywa na HELSB, maana lazima pia watakuwa wamepigika.