Kauli 10 za walimu darasani.

Kauli 10 za walimu darasani.

kuchangumu

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2014
Posts
724
Reaction score
290
1: Mkimaliza kuongea, niambieni niendelee kufundisha.
2: Baba yako aliuza ng'ombe ili alete ng'ombe mwingine shuleni.
3: Kama unajua kuliko mimi, njoo ufundishe wewe.
4: Ulikuja peke yako na utaondoka peke yako.
5: Hata msipoelewa, mshahara wangu uko pale pale.
6: Baba yako anahangaika kulipa ada wewe unafanya utumbo tu.
7: Hata nikeshe nafundisha, wengine ni mizigo hawatoki na lolote.
8: Bichwa lako kubwa lipo kwa ajili ya kutenganisha masikio yako.
9: Bichwa kubwa ubongo nukta.
10: Wengine hapa wamekuja kukua tu.

Unayo nyingine? Mkumbuke mwalimu wako.
 
mimi nilipokuwa mwalimu sikuwahi kutumia hayo maneno.... labda ni hawa wakisasa....
 
masuala ya mikopo hayanihusu mimi kama hujalipa ada hakuna kufanya mtihani. prof
 
hizo ni kauli za kuwatia moyo wanafunzi ndo maana walio wengi mmetoka.. shukurunii
 
Nimewaambia masuala ya mapenzi huu si wakati wake, subirini mkimaliza shule hata mkitaka kuzilamba mtazilamba...Our second master....R.I.P
 
Wale wote niliowaandikia 'see me' na hawakuja kuniona wapite mbele...:angry::angry:
 
namba nne ni kweli ila inauma sana i miss ma friends badly sijui wako pande zipi muda huu
 
Back
Top Bottom