Kauli 10 chafu za waalimu wawapo darasani

Kauli 10 chafu za waalimu wawapo darasani

Zuia Sayayi

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2011
Posts
841
Reaction score
140
Kauli 10 CHAFU za walimu darasani, unakumbuka ipi hapa??

1:Mkimaliza kuongea niambieni niendelee kufundisha
2:Baba yako kauza ng'ombe ili alete ng'ombe mwingine shule
3:Kama unajua kuliko mimi njoo ufundishe wewe
4:Ulikuja peke yako na utaondoka peke yako
5:Hata msiponisikiliza mshahara wangu uko pale pale
6:Baba yako anahangaika kulipa ada wewe unafanya utumbo tu
7:Hata nikeshe nafundisha wengine ni mizigo hawatoki na lolote
8:Tunavisaidia tu kwan vikifanikiwa mbelen hata salam vinatoa?
9:Bichwa kubwa ubongo nukta
10:Wengine hapa wamekuja kukua tu.

Ipi huwa inakukera zaidi??
 
Uandike, usiandike, utajua mwenyewe maana daftari lako najua litaishia kufungiwa vitumbua tu....aisee walimu kiboko
 
nikigeuka hapa mtalia na kusaga meno!
kusomesha ninyi ni kama kuflash pesa chooni..
 
Hii ya baba kauza ng'ombe asomeshe ng'ombe ingine........ni kauli ngumu sana.........
 
Namba moja ilikuwa inaniumiza sana, na kweli hafundishi mijitu inaendelea kupiga kelele
 
Hiyo number 4 nakumbuka tulifanya mgomo sasa kipindi tunafukuzwa shule mwalimu wa nidhamu akawa anatuambia halafu alikuwa na busara kweli yani ile kuanza kuondoka kila mtu yuko na begi lake anaanza kuwaza huko nyumbani inakuaje yani watu walikuwa wanalia kawa wamefiwa
 
duh inamaana wewe migomo umeanza long time ago?
hadi kwa mumeo unagoma!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom