Hizi hapa Kauli 10 mbaya za walimu darasani, unakumbuka ipi?

Drax001

JF-Expert Member
Aug 22, 2017
439
221
1:mkimaliza kuongea mniambie niendelee kufundisha
2:baba yako kauza ng'ombe ili alete ng'ombe mwingine shule
3:kama unajua kuliko Mimi njoo ufundishe wewe
4:ulikuja peke yako na utaondoka peke yako
5:hata msipo nisikiliza mshabara wangu upo pale pale
6:baba yako anahangaika kulipa ada wewe unafanya utumbo tu
7:hata nikeshe nafundisha wengine mizigo hawatoki na lolote
8:tuna visaidia tu kwani vikifanikiwa mbeleni hata salamu havitoi
9:kichwa kubwa ubongo nukta
10:wengine hapa wamekuja kukua tu
Ipi ulishawahi kuambiwa shuleni na mwalimu wako?
Mimi niliambiwagwa kama unajua kuliko Mimi njoo ufundishe wewe
 
Namba 5 hasa walm wa kike walikuwa wanapenda
mimi kuna mwalimu mmoja nilikuwa na bifu nae alikuwa akiingia tu dalasani atanitafuta nilipo ili aniulize swali nikikosa2 matusi yanaanza na misemo yao nilikuwa nakelekwa sana
 
5. Alikua anaitia vionjo vionjo, hata msiponisikiliza mwisho wa mwez naenda kukinga, sisahau kauli za yule dada enz zile. Halaf kumbe ilikua sijui lak na 80 kama si elf 80, afanalek kweli ukipata wa kuoshea osha,
 
Dah kuna teacher mmoja alikua anachapa sana asee kwenye table, akiuliza 7x6 kabla hujajibu tayari unayo ya mgongo.

Dah huyu mwalimu siku hizi namnunulia beer eti amekuwa best yangu wakati enzi za standard three na four alinicharaza kinoma
 
5. Alikua anaitia vionjo vionjo, hata msiponisikiliza mwisho wa mwez naenda kukinga, sisahau kauli za yule dada enz zile. Halaf kumbe ilikua sijui lak na 80 kama si elf 80, afanalek kweli ukipata wa kuoshea osha,
aaaah haahaaa kweli alafu walimu wanawake ndio wanakuwa na misemo ya ajabu ajabu
 
Dah kuna teacher mmoja alikua anachapa sana asee kwenye table, akiuliza 7x6 kabla hujajibu tayari unayo ya mgongo.

Dah huyu mwalimu siku hizi namnunulia beer eti amekuwa best yangu wakati enzi za standard three na four alinicharaza kinoma
huyo mkumbushie enzi zake umwambie ticha enzi zako ulikuwa wewe mbaya ubest unaweza kupungua
 
Aisee kuna mwalimu wangu wa Geography O level kipind nko form 3 aliniambia " Mimi nafundisha hapa mbele Wewe dg unapiga piga kelele humu darasani. Halafu inaonekana wazazi wako ni maskini sana kuliko hata wazazi wangu. Wewe DG kuanzia sasa nisije nikakuona kwenye kipindi changu, nikiingia tu ww utakua unatoka"


Baada ya pale akanilamba stiki za kutosha. Kilichokua kinaniuma ni kwamba mm nilikua nasoma arts na pia nilikua napendelea kwenda kusoma Hgl coz ni combination niliyokua naipenda na kuiweza, alikua ni mwl mzur sana wa Geography.


Sikusoma vipind vyake km wiki mbili hv, nikaona huu ni uboya so nikaamua kwamba nitabaki kwenye Geography km atanichapa tena bora anichape coz kwa hatua hii nitafel. Nikawa nabak kwenye somo lake na wala hakunifualitia tena na hata hakunichapa.

Baada ya kumaliza form four Advance nikaenda kusoma zangu hgl . Hahahahaaa baada ya kumaliza zangu six ile kuingia Udsm kusoma bachela yangu nikamkuta yule ticha anapiga zake masters, yule tcha hata alikua hanikumbuk tena mpaka namaliza chuo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom