Katuni ya Rais Magufuli by Gado

Kwa hiyo unataka kusema katumwa na Kenyatta mkuu?
Sijajua, ila mara nyingi propaganda kama hizo hawezi kuwafanyia watu kama wakenya.
Gado ni mtanzania lakini hajielewi alikuwa anafanya nation media ya kenya baadae akahamia DW ya ujerumani na nikawaida kueneza propaganda kama hizo kwa JPM na kuna katuni nyingi zingine zinaonesha kashfa kubwa kwa JPM alizochora gado akiwa DW, siwezi kuzipost hizo katuni kwani nitazidi kuusambaza ujinga wake.
 

Katuni za Gado nazifuatilia muda mrefu sana....ziko hapa......ni aina ya uchoraji wake....ukiweza cheki anavyomchora Kagame, Mugabe na Museveni! Hata anavyomchora Uhuru...kama anatumwa basi ni kwa maraisi wengi tu waafrika.....

Mifano michache....




 
Hana lolote huyo gado njaa ndio inayomsumbua kwa kutaka umaarufu kwa kupitia JPM, mbona sijawahi muona aki mchora uhuru kenyata hivyo?

Gado amekuwa maarufu kabla ya hata Magu hajaotewa uraisi.. Ukishakuwa na inferior complex katika suala lolote utaishia kumshambulia mleta ujumbe, badala ya kuuangalia ujumbe wenyewe..
 
Mitindo ya (ki dikteta) ...,

Sioni sababu yoyote ya kumuita mchora katuni..., MJINGA... Na hata ktk post yako sijaona uchambuzi wowote unaoelezea ujinga wake... Na jee..., ujinga wake uko ktk jambo lipi hasa...?! Fafanua..., ni mjinga ktk maswala ya kisiasa..,? Kiuchumi...? Au ktk kuchora katuni...?!
Mimi naona amefikisha ujumbe kwako na ndio maana umetoa hoja ya HASIRA kwake..., na huku ukionyesha MAHABA kwa Raisi wetu.. Sio vibaya kumpenda Raisi wako..., ila usiwe kipofu sasa..., usizuie maoni ya wengine kwa jinsi wanavyomwona Raisi wetu.. Wewe na wenzako wenye MAHABA kama wewe.., muwe wavumilivu. Rais ktk UTENDAJI wake anaumiza watu wake na anawafurahisha wengine, wanaoumia wana namna nyingi ya kulia, kulalamika, au hata kushtaki kwa Mungu...
WAACHENI WATU WALIOWAPA UONGOZI WAWAKOSOE..., NI HAKI YA KIRAIA NA KIKATIBA...
Gado hajazuia Raisi kufanya wajibu wake....
 
Gado amekuwa maarufu kabla ya hata Magu hajaotewa uraisi.. Ukishakuwa na inferior complex katika suala lolote utaishia kumshambulia mleta ujumbe, badala ya kuuangalia ujumbe wenyewe..
Haujaelewa mada unaishia kuongea usichokijua.
Lengo ni kujadili katuni za gado na maudhui yake kwenye hiyo katuni na sio mleta mada.
Siku nyingine jifunze kutulia sio una kurupuka kama umefumaniwa.
 
Maneno mengi ila point less, lengo langu si kuchambua bali kuelezea maudhui ya katuni za gado anapomuelezea JPM
 
Haujaelewa mada unaishia kuongea usichokijua.
Lengo ni kujadili katuni za gado na maudhui yake kwenye hiyo katuni na sio mleta mada.
Siku nyingine jifunze kutulia sio una kurupuka kama umefumaniwa.
Inawezekana wewe ni kaka yake jei.. Ngoja nikuache..
[emoji124] [emoji124] [emoji124]
 
Gado wachore tena Sanaa..Sioni chochote cha maana kutoka kwenye serikali hii isiyotofautiana na Kaole Arts Group
 
Issue hapa siyo sheria ya mtandao tu. Gado anahoji kulikoni mafisadi hawa shugulikiwa.
 
aisee Gado mkali!
 
Hii ni Sanaa tu hata viongozi wakubwa duniani wanachorwa sana. Ni kitu cha kawaida kwa nchi huru.
 
Reactions: SDG
hata mi ni mtaalam wa katuni, lakini sipendi kutumiwa kama huyu GADO. sipendi matatizo kwa nisiyoyajua pia na kumdhiaki mkuu wa nchi. gado uhuru wa habar bila sheria ni uwenda wazimu. poor gado
Mjini mtamu kwa nguruwe ...
 
Maneno mengi ila point less, lengo langu si kuchambua bali kuelezea maudhui ya katuni za gado anapomuelezea JPM
Ishii! sasa wewe apo unaona umeongea point gani..!? jipu ulicho ulizwa sio unatoka povu kama umefumaniwa na baba mkwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…