Katoto kenyewe kabaya, kaache kafe

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,645
155,016
NI STORI NZURI YENYE FUNZO HASA WALE TUNAOCOMMENT KTK MITANDAO YA KIJAMII BILA BUSARA, HEKIMA WALA STAHA.

MY STORY: KATOTO KENYEWE KABAYA, NANI ATAKACHANGIA, ANGEKAACHA KAFE TU!

Tofauti na watu wengine ambao wakimaliza chuo wanahangaika kupata kazi mimi haikua shida kabisa. Nilizunguka mara mbili tatu nikapata kazi katika kampuni moja kubwa tu. Sikutarajia kwani sikuwa na uzoefu kabisa, niliingia kazini na kufanya kazi vizuri tu, bosi wangu alikuwa ni mtu poa sana. Kampuni ilikuwa ikimilikiwa na mtu na mke wake lakini mke ndiyo alikuwa anasimamia kila kitu.

Siku tu ya usaili yule dada alinichangamkia sana, sikuwa na uzoefu lakini nilishangaa napata kazi tena kwa mshahara mzuri. Nilipoanza kazi alikuwa karibu yangu sana, alikuwa ananisaidia kukua, ananishirikisha kwenye mambo mengi na dili zote za pesa alikuwa akinishirikisha. Nilifanya kazi kwa mwaka mmoja na mambo yangu yalikuwa mazuri nilijiona kabisa napanda cheo.

Siku moja Bosi wangu alinikaribisha kwake, pamoja na mazoea na wafanyakazi wake lakini hakuwa mtu wa kumkaribisha mgeni kwake. Nilikuwa nalielewa hilo na kikubwa nilisikia kuwa pamoja na pesa zao nyingi lakini walikuwa hawajabarikiwa kupata mtoto, walishakuwa naye lakini alifariki akiwa na miaka mitano.

Mtoto wao alizaliwa na matatizo ya moyo na figo, walihangaika naye sana ktk hospitali mbali mbali na nilisikia kuwa kuna kipindi walikaribia hata kufunga kampuni kwani walishauza kila kitu ili kugharamia matibabu lakini mtoto wao alifariki dunia na hawakubahatika tena kupata mtoto. Hiyo ilikuwa ni miaka mitatu nyuma. Nilifurahi kukaribishwa, nilifika aliniandalia vizuri, mume wake hakuwa nyumbani.

Basi nilikaa. Ukutani kulikuwa na picha kubwa ya mtoto wao, niliiangalia naye akaanza kunitambulisha kwa mtoto wake kupitia ile picha. Akaniambia jinsi alivyohangaika naye mpaka kufia mikononi mwake. Aliongea huku akilia, nilimuonea huruma. Kwa kuingalia ile picha tu mtoto alionekana anaumwa sana.

Wakati tumekaa alinionesha albam ya picha za mtoto wake. Alinionesha picha nyingi sana mpaka picha nyingine wakiwa hospitalini, akiwa amempakata mtoto wake ana hali mbaya, picha za mazishi, alikuwa akilia wakati wote mpaka mimi nikalia. Mwisho alinyamaza ghafla, akachukua simu yake, akafungua kitu kisha akaniambia.

“Maombi yako yalitimia, mtoto wangu alikufa kama ulivyotamani iwe” aliniambia, nilishituka kwani sikudhani kama ningeweza kufanya hivyo.
“Unamaanisha nini?” Nilimuuliza kwa mshangao. Hakutaka kuongea sana, aliingia Facebook, sijui alifanya nini ni kama alikuwa kaandaa hiyo post akanionyesha Comment yangu ambapo nilicomment miaka kama mitatu au minne nyuma kipindi hicho nikiwa chuo mwaka wa kwanza.

Kuna group ilipostiwa picha ya mtoto wake akiwa anaumwa anaomba mchango kwa ajili ya matibabu na mimi nilicomment “Katoto kenyewe kabaya nani atakachangia angekaacha kafe tu!” Ilikuwa ni comment ya zamani, yaani hata nilikuwa siikumbuki. Niliishiwa nguvu kwani kwenye hiyo post ni mimi tu niliongea hivyo, watu walinichamba sana lakini niliishia kuwatukana na kuzidi kumtukana mtoto ili tu kujionyesha mbabe.

“Jina lako siwezi kulisahau, nilijuta hata kuomba msaada kwani baada ya wewe kuandika vile pamoja na kupata pesa lakini haikupita wiki mtoto wetu alifariki dunia. Machungu niliyoyapata nilishindwa kukusahau, ndiyo maana nilipokuona umekuja kuomba kwenye usaili pamoja na kwamba hukuwa na vigezo nililazimisha kukuajiri ili kukuonesha kuwa maisha yana kesho….”

Aliongea mambo mengi sana kwa uchungu, nilimuomba msamaha kuwa niliandika tu kiutani na sikudhamiria. Yeye hakuwa na neno, aliniambia amenisamehe ila alitaka tu kunifundisha maisha. Nilishindwa hata kukaa, nilinyanyuka na kuondoka. Hakunifukuza kazi lakini sikuweza tena kurudi pale kazini. Niliacha kazi sikurudi hata kudai kitu chochote.

Alijaribu kunitafuta ili nirudi kazini lakini sikuwa na huo ujasiri, nilikua naogopa sana kiasi kwamba nilidhani kama nikirudi anaweza kunifanyia kitu kibaya. Nina mwaka wa pili sasa tangu niache hiyo kazi na bado sijapata kazi nyingine. Maisha yamekuea magumu sana, mpaka leo najuta, unaweza kuongea kitu kama utani au kutaka sifa kwa watu bila kujua unaharibu maisha ya wengine au kuwasababishia maumivu makubwa sana.

MWISHO
 
Hii kitu huwa inaponza wengi sana.

Nakumbuka siku niliyopata kazi niliambiwa dogo mbali na kukidhi vigezo vyote vya usaili pia tumekufuatilia hadi Post zako zote za Facebook na Insta na umekidhi mahitaji yetu.
Nikajifunza kuwa kitu cha hovyo unachoweza kukifanya leo, kinaweza kukuharibia mambo huko mbele ya safari yako ya kimaisha.
 
Ujumbe mzuri sana mkuu huwa naona hata kwenye habari za kuumiza mioyo kama msiba na magonjwa baadhi ya watu wanakoment dhihaka. Mtu kama uwez kukoment vizuri bora ukae kimya tu kuliko kutafuta attention kwa jambo la hovyo.
 
NI STORI NZURI YENYE FUNZO HASA WALE TUNAOCOMMENT KTK MITANDAO YA KIJAMII BILA BUSARA, HEKIMA WALA STAHA.

MY STORY: KATOTO KENYEWE KABAYA, NANI ATAKACHANGIA, ANGEKAACHA KAFE TU!

Tofauti na watu wengine ambao wakimaliza chuo wanahangaika kupata kazi mimi haikua shida kabisa. Nilizunguka mara mbili tatu nikapata kazi katika kampuni moja kubwa tu. Sikutarajia kwani sikuwa na uzoefu kabisa, niliingia kazini na kufanya kazi vizuri tu, bosi wangu alikuwa ni mtu poa sana. Kampuni ilikuwa ikimilikiwa na mtu na mke wake lakini mke ndiyo alikuwa anasimamia kila kitu.

Siku tu ya usaili yule dada alinichangamkia sana, sikuwa na uzoefu lakini nilishangaa napata kazi tena kwa mshahara mzuri. Nilipoanza kazi alikuwa karibu yangu sana, alikuwa ananisaidia kukua, ananishirikisha kwenye mambo mengi na dili zote za pesa alikuwa akinishirikisha. Nilifanya kazi kwa mwaka mmoja na mambo yangu yalikuwa mazuri nilijiona kabisa napanda cheo.

Siku moja Bosi wangu alinikaribisha kwake, pamoja na mazoea na wafanyakazi wake lakini hakuwa mtu wa kumkaribisha mgeni kwake. Nilikuwa nalielewa hilo na kikubwa nilisikia kuwa pamoja na pesa zao nyingi lakini walikuwa hawajabarikiwa kupata mtoto, walishakuwa naye lakini alifariki akiwa na miaka mitano.

Mtoto wao alizaliwa na matatizo ya moyo na figo, walihangaika naye sana ktk hospitali mbali mbali na nilisikia kuwa kuna kipindi walikaribia hata kufunga kampuni kwani walishauza kila kitu ili kugharamia matibabu lakini mtoto wao alifariki dunia na hawakubahatika tena kupata mtoto. Hiyo ilikuwa ni miaka mitatu nyuma. Nilifurahi kukaribishwa, nilifika aliniandalia vizuri, mume wake hakuwa nyumbani.

Basi nilikaa. Ukutani kulikuwa na picha kubwa ya mtoto wao, niliiangalia naye akaanza kunitambulisha kwa mtoto wake kupitia ile picha. Akaniambia jinsi alivyohangaika naye mpaka kufia mikononi mwake. Aliongea huku akilia, nilimuonea huruma. Kwa kuingalia ile picha tu mtoto alionekana anaumwa sana.

Wakati tumekaa alinionesha albam ya picha za mtoto wake. Alinionesha picha nyingi sana mpaka picha nyingine wakiwa hospitalini, akiwa amempakata mtoto wake ana hali mbaya, picha za mazishi, alikuwa akilia wakati wote mpaka mimi nikalia. Mwisho alinyamaza ghafla, akachukua simu yake, akafungua kitu kisha akaniambia.

“Maombi yako yalitimia, mtoto wangu alikufa kama ulivyotamani iwe” aliniambia, nilishituka kwani sikudhani kama ningeweza kufanya hivyo.
“Unamaanisha nini?” Nilimuuliza kwa mshangao. Hakutaka kuongea sana, aliingia Facebook, sijui alifanya nini ni kama alikuwa kaandaa hiyo post akanionyesha Comment yangu ambapo nilicomment miaka kama mitatu au minne nyuma kipindi hicho nikiwa chuo mwaka wa kwanza.

Kuna group ilipostiwa picha ya mtoto wake akiwa anaumwa anaomba mchango kwa ajili ya matibabu na mimi nilicomment “Katoto kenyewe kabaya nani atakachangia angekaacha kafe tu!” Ilikuwa ni comment ya zamani, yaani hata nilikuwa siikumbuki. Niliishiwa nguvu kwani kwenye hiyo post ni mimi tu niliongea hivyo, watu walinichamba sana lakini niliishia kuwatukana na kuzidi kumtukana mtoto ili tu kujionyesha mbabe.

“Jina lako siwezi kulisahau, nilijuta hata kuomba msaada kwani baada ya wewe kuandika vile pamoja na kupata pesa lakini haikupita wiki mtoto wetu alifariki dunia. Machungu niliyoyapata nilishindwa kukusahau, ndiyo maana nilipokuona umekuja kuomba kwenye usaili pamoja na kwamba hukuwa na vigezo nililazimisha kukuajiri ili kukuonesha kuwa maisha yana kesho….”

Aliongea mambo mengi sana kwa uchungu, nilimuomba msamaha kuwa niliandika tu kiutani na sikudhamiria. Yeye hakuwa na neno, aliniambia amenisamehe ila alitaka tu kunifundisha maisha. Nilishindwa hata kukaa, nilinyanyuka na kuondoka. Hakunifukuza kazi lakini sikuweza tena kurudi pale kazini. Niliacha kazi sikurudi hata kudai kitu chochote.

Alijaribu kunitafuta ili nirudi kazini lakini sikuwa na huo ujasiri, nilikua naogopa sana kiasi kwamba nilidhani kama nikirudi anaweza kunifanyia kitu kibaya. Nina mwaka wa pili sasa tangu niache hiyo kazi na bado sijapata kazi nyingine. Maisha yamekuea magumu sana, mpaka leo najuta, unaweza kuongea kitu kama utani au kutaka sifa kwa watu bila kujua unaharibu maisha ya wengine au kuwasababishia maumivu makubwa sana.

MWISHO
Aisee
Nimejifunza kitu
 
Back
Top Bottom