Katika teuzi za Rais Samia, nani waondoshwe kazini kwenye kapu la Wakuu wa Wilaya?

kavyilu

Member
Dec 14, 2019
28
53
Wanabodi Salaam,

Naandika haya nikitambua kuwa kwa Mamlaka ya Rais. Rais hatalazimika kufuata ushuri wetu pindi atakapo kuwa akitimiza majukumu yake kwa mujibu wa katiba.

Hata hivyo ni muhimu kwa Rais kupitia ushauri wa wananchi anaowaongoza kwa kuwa mamlaka yake yametoka kwa wananchi.

Rais anaendelea kupanga na kupangua safu yake ya kumsaidia katika kuiongoza nchi yetu.

Katika teuza za majaji na wakuu wa miko,wengi wamepongeza isipokuwa tu kwa aliekuwa DPP na Wakuu wawili wa mikoa,yaani Chalamira na Ally Happi, waliosalia wamefaulu mtihani wa mchujo wa wananchi.

Uteuzi wa wakuu wa Wilaya

Huku ndio kuna utitiri wa viongozi wajinga na wanaoharibu taswira ya serikali.

Mamaa yetu mpendwa Rais Samia huku usifanye uhamisho,huku wabaki 20% tu.

Asilimia 80 teua ma DC wapya,nashauri katika uteuzi wako chukua watu kutoka Idara za serikali na sio vyama vya siasa.

Watumishi waliopo kwenye Idara mbalimbali za serikali wanaouzoefu mkubwa wa kufanya kazi za serikali.

Watumishi hawa wameshiba maadili ya uongozi wa umma tofauti na hawa malimbukeni wanaotukana watu na kujigeuza miungu watu.

Mh.Rais Samia watumishi hawa wanajua vizuri jinsi serikali invyofanya kazi,wamesoma uongozi na utawala,hawatakuangusha kama wanavyofanya aki na Sabaya.

Orodha ya wakuu wa wilaya wasiotakiwa kuwemo kwenye 20% ya watajaobakishwa.

1. Ole Sabaya Wa Hai afukuzwe rasmi(sasa amesimamishwa)

2. Komanya Kitwala wa Tabora mjini afukuzwe maana kazi yake ni kugombana na surbordinates wake.

3. Yule Mama wa Kilolo afukuzwe maana kagimbana na madereva 14, yaani hana moral authority ya kuendelea kuitwa DC.

4. Mtazame kwa jicho la Tatu DC wa Gairo, nae ni msumbufu na anamajivuno.

Karibuni wana jamvi ,mnisaidie kusaga kunguni kwa ma DC wa hovyo ambao Mama anatakiwa kuwafukuza kazi.

NB. Gondwe na Joketi wabakishwe kwenye 20%.

Ni hayo tu kwa leo.
 
DC wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza afurushwe haraka ana majivuno sana.Kila mara ni kuwadharirisha wafanyakazi.Wilaya imedumaa hana ubunifu zaidi ya majivuno tu.
 
Mbona Anthon Mtaka anasifiwa na kila chama,kwani nae ni Chadema?

Ukifanya wema watu watakusifia na kuombea, Januari Makamba anakubalika sana kutokana na tabia yake.
Asiyefahamu uchapakazi wa Antony Mtaka hatumuelewi kama ni mtanzania mwenzetu labda atakuwa anatumika na wale walioangukia pua.
 
Kuna kitu tumegundua Maka hatumbui islams kamwe .....kuna walakini kwa islams ...ila muda mwalimu mzuri tuendelee kujifukiza....huyo dada kilolo hataguswa
 
Gondwe bhaana..
Kwenye msiba wa mzee alikimbia na gari la msiba ka kilomita tano hivii toka taifa.😂😂😂

Dah.. Na u RC kakosa..
 
Jokate anastahili kubaki, yupo smart kwenye kazi yake na hana majivuno.
 
Back
Top Bottom