karv
JF-Expert Member
- Dec 26, 2019
- 1,799
- 3,221
Nawasalimu kwa jina la jamuhuri
Bado naendelea kufuatilia masuala mazima ya ndoa hasa katika nyanja kuu 3 kimila, kidini na kiserikali.
Suala la kulipa mahari kwa mwanamke lipo na limeelezwa katika vitabu vya dini za imani zote. Kama kuna mtu anapinga hilo hebu arudi kwa mwalimu wake wa dini amfundishe vizuri.
Kimila kuna baadhi ya makabila mahali hutozwa kutokana na elimu ya binti, kwingine ubikira /kigoli (sio kwa sasa), Rangi ya ngozi, shepu, Urafiki, koo na mambo mengine.
Katika upande wa serikali bado sijafahamu kama wanaruhusu mwanamke kulipiwa mahari au la na kama ipo ni kwa misingi gani na sheria ipi (wanasheria mtatusaidia hapa).
Naomba nije kwenye swala zima la mahari kwa upande wa kidini na hapa naomba kuzungumzia katika dini ya kiislamu ambapo katika hili wapo wazi sana licha ya kwa upande wa pili WAKRISTO biblia imeelezwa kuhusu mahari pia. Lakini kama upo ufafanuzi mzuri katika hilo wanaweza kuuleta hapa tukaangalia pia sheria za ndoa ya kikristo wanazungumziaje swala hilo.
Katika dini ya kiislamu japokuwa mimi sio muumini wao nimekuwa nikisikia na kufuatilia pia katika kusikia kwaku nimenukuu vitu viwili ambavyo vinafanya niwape hongera na pongezi.
Vitu hivyo ni
~Mwanamke ndiye anayetaja mahari yake.
~Mahari ni ile iliyokuwa nyepesi kulipwa.
~Kulipa mahari ni lazima kama isipolipwa ni ruksa mwanamke kukataa ndoa.
KWANINI WAMEUPIGA MWINGI?
Ndoa nyingi zimeshindwa kufungwa sababu tu ya mwanaume kutajiwa mahari kubwa na wazazi wa mwanamke na kwamba mfanya yeye ashindwe kulipa.
Kama mwanamke anakupenda kweli hawezi kukutajia mahari ya kukukomoa maana anajua anaweza kumkosa ampendaye hivyo atataja mahari kutokana na uwezo wako.
Mtu atatajiwa mahari ambayo ipo ndani ya uwezo wake wa kulipa hivyo kupunguza malalamiko na mambo mengine.
Kuna baadhi ya wanawake huwasaidia waume zao kulipa mahari ili tu mambo yaende sawa
~Kama kuna mengine mnaweza kuongeza kwa kugusia pande zote yani kimila, kidini na kiserikali.
Ili tujue swala zima la ulipaji mahari lipoje katika makabila yetu
.................AHSANTENI.................