GuDume
JF-Expert Member
- Jan 18, 2015
- 6,652
- 14,247
Akili,mfumo na mawazo ya watanzania wengi wanaamini kama wewe si ccm basi ni cdm au cuf n.K wanashindwa kuelewa kuna watu ambao hatuja uza utu,akili na fikra zetu. Kuna watanzania huru ambao wao wamegoma kudumisha fikra za mwenyekiti au za chama husika.
Hili kundi ipo na lina watu wengi pia.Na vyama karibia vyote vimeshindwa kulitumia kundi hili sababu utakuta kwenye kampeni,kwenye mikutano na mihadhara kundi hil linatengwa.Tofauti na nchi za wenzetu zilizoendelea. Hizi huwa na kundi kubwa la wananchi ambao si wanachama wa chama chochote na hawa wanategemea sera za mgombea uongozi.
Nchi za kiafrika hasa tanzania ni tofauti. Its either with us or against us.Ndo maana kwa mwono huu ukiipinga ccm watakuita wewe cdm. Ukiipinga cdm watakuita wewe CCM. Kwanini? Sababu hawaamini katika fikra huru au demokrasia ya kweli.Ukishakuwa wewe ccm basi unatakiwa upinge kila linalosemwa na cdm. And the vice versa is true. Unadhan hapa inchi itawezeje kuendelea?
Kama mtu atatoa wazo hatutaliangalia wazo. Tutaangalia aliyesema ni chama gani,wakati flani inaweza kuwa dini gani au kabila gani. Halafu ndo tunaamua tuunge au tupinge hiyo hoja kwa kuzingatia vigezo hafifu kama hivyo.
Ufuasi wa chama au mtu ni utumwa, ni kuuza nafsi, akili ,fikra na utambuzi wa mambo. Na hiki ni kigezo kikubwa cha kuwa na fikra duni,dhaifu au kondefu.Maana tunajikuta kuwa tumejizungushia wigo katika kufikiri.Hatufikiri nje ya wigo huo.
Binafsi niliacha kuwa mfuasi wa mtu au chama mwaka 2000.Miaka 19 baadaye watu bado wanakumbatia ufuasi, utumwa wa kifikra. Na hawa huwa wanakuwa waliosoma (lakini hawajaelimika) na wasiosoma hivyo wana ujinga bado. Tanzania itabadilika ikiwa kuna siku mtu ndani ya cdm atakosoa jambo na kuheshimiwa au mawazo yake kutendewa kazi na mwingine ndani ya ccm atakosoa na pia kaendelea kuheshimiwa na mawazo yake yakafanyiwa kazi.
Tunajiweka kazi hali ya u-mbwa pale tunapoteua kuwa na bwana wa kumtumikia na kumuunga mkono katika kila jambo. Huu si ubinadamu. Mbwa humsikiliza bwana ake yu asemaje au yu ataka nini naye huunga mkono jambo hilo au hulitenda pasipo kuhoji.Hii ni hali mbaya kwa taifa hasa kwa vijana ambao kwa sasa ndo wamekuwa wafuasi wa vyama na watu mpaka wanakinaisha.
Ombi langu:
Mkiwa kwenye vyama vyenu, ufuasi wenu na mabwana zenu, hali ninyi mkiwa watwana basi msisahau tupo na sisi ambao tumegoma kuwa wafuasi, tumegoma kuuza nafsi, tumegoma kulaza ubongo. Sisi ambao tumeamua kuita nyeupe nyeupe na nyeusi nyeusi pasipo kujali anayetuoesha anapendelea hizo rangi ziitwe nini.
Mimi sihitaji kuwa mwanachama au mfuasi wa kiongozi flani ili nitoe mawazo yangu. Nitabaki kuwa mtanzania asiye na chama wala mfuasi wa mtu yeyote ili niweze kutizama na kuona mambo katika mwanga bora.
"Ufuasi ni upofu wa kifikra, ukada ni upumbavu" tukatae kutumika.... Wanaowatumia wanawadhalilisha sana. Kiakili,kifikra,kiimani na kimwili.
"Tanzania kwanza, vyama baadaye"