Katika nchi nyingi za Afrika, wananchi wamejifunza kutosadiki kile waambiwacho na hawa wanasiasa

KUTATABHETAKULE

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
4,601
4,202
Kipindi cha kampeni kipo nasi kwa sasa hivi. Huu ni wakati ambao wananchi watapewa ahadi ambao zinashangaza sana masikioni na akilini pia. Alipata kusema Nikita Khrushchev, kiongozi wa RUSSIA, kwamba wanasiasa ulimwenguni pote hufanana.

Wanaahidi kujenga madaraja mahali ambapo hapana hata mto. Katika nchi nyingi za Afrika, wananchi wamejifunza kutosadiki kile waambiwacho na hawa wanasiasa.

Wanasema kuwa mkiwa katika chumba cha mkutano na mwanasiasa akawaeleza kuwa muda huo ni mchana, msimuamini kabisa. Tokeni nje ya chumba ili mjihakikishie pasi na shaka kwamba kweli jua lipo angani.

Je, kwa Tanzania mambo yakoje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…