Umeshajiuliza haya katika Siasa za Afrika na viongozi wake?

The kankara

Member
Jul 17, 2020
58
88
Huwa najiuliza mara kwa mara, kwanini wanasiasa wa Afrika kipindi cha uchaguzi ni kama vita? Maana hata bajeti ya dharula kwa vyomno vya usalama huwa inawekwa kama sikosei!

Maana kuweka askari attention na vifaa vyao si bure ni gharama. Lakini mwisho wa siku huwa tunasikia hata waangalizi kutoka sehemu nyingine huwa wanasema mambo yalikuwa huru na haki.

Inawezekana kweli mtu uliyeamka mwenyewe kutoka nyumbani kwake bila kulazimishwa akafika kupanga mstari kupiga kura, halafu kukawa kuna vyombo vya usalama pembeni vikiwa na dhana za kujihami? (mabomu ya machozi, virungu, magari ya kuwasha n.k)

Na wakati mwingine sehemu mbali mbali Afrika hii imekuwa kama sheria, ukishapiga kura hamna kuzengea zengea maeneo hayo?

Na imekuwa desturi kwa bara la Afrika kipindi kuelekea chaguzi mpaka muda wenyewe wa chaguzi raia lazima waumie, wajeruhike, wengine wafe, wapotee yaani vurugu mechi!

Sasa turudi katika mada ya msingi. Ni nini kinachowafanya viongozi wa Afrika kung'ang'ania kitu wasichokiweza?

Kwa sababu tunafanya chaguzi, tunatumia gharama za kutosha na bado hatufikii malengo yale ya uchaguzi na demokrasia kama zinavoimbwa majukwaani na wahusika.

Kwanini viongozi wasijifikirie kuweka mfumo wao tofauti Afrika wanaouona wanauweza?

Maana kama chaguzi zinatumia gharama nyingi na bado hazifikishi malengo halisi na bado zinapelekea chuki, visasi, kuumizana mpaka kuuana zina faida gani? (Mfano mzuri siku chache zilitokea vurugu nchini Kenya,na mpaka sasa hivi kuna vugu vugu la vurugu)

Twende mbele turudi nyuma, hulka ya muafrika ni kutokuridhika wala kutosheka (hii haikwepeki ndo maana ufisadi haushi na mfano mzuri ni rais wa nigeria wa sasa) sasa kama viongozi wa Afrika hulka yao ni kung'ang'ania madarakani ni nini kinachowashinda kutenda yanayotakiwa kutendeka kwa wananchi hasa hali za kiuchumi na hali za kijamii ziwe nzuri ili wasibughudhiwe kuondoka?

Afrika na demokrasia imeshakuwa chui na paka (ndio maana mwanasiasa anapita kuomba kura kwa unyenyekevu wiki mbili tatu akiingia madarakani anakuamrisha wewe wewe aliyepita kukuomba kura kwa unyenyekevu mwezi uliopita,tena ukimsumbua zaidi anaweza amrisha mpaka upigwe na rungu) Sasa kama swala ni hivi kwanini wasiachane na ufisadi,ubinafsi na ubadhirifu wa fedha za mapato ya ndani halafu wakaachana na mikopo ya wazungu ili wasiwalazimishe kufanya mambo ya demokrasia tukarudi enzi za ufalme na u chief?

Anyway, ushauri tuu

Ifike muda wanasiasa afrika wasitumie nguvu nyingi sana kusalia madarakani, wawatendee wananchi wale wanayoyaahidi, watimize wajibu wao, waache ufisadi, ubadhirifu wa fedha za umma, waboreshe miundo mbinu, sekta za afya, elimu na vipato vya mtu mmoja mmoja,hawatapata shida tena hata ya kupigana na mabomu wala kusimamiana na mitutu ya bunduki vipindi vya uchaguzi.
 
Back
Top Bottom