Katika kutoa huduma za mabasi ya mwendokasi DART, serikali inapiga mdogo sana

nasrimgambo

JF-Expert Member
Jan 10, 2017
1,858
2,348
Habari,
Jamani hali ni tete katika huduma za mabasi ya mwendokasi

Mara mia daladala,
Mabasi haya ni zero, ni sifuri, hamna kitu, ni bure kabisa, total rubbish, nada.

Muda wa kusubiri basi unazidi kuongezeka kadri siku zinaenda, ni kawaida kupoteza nusu saa hadi dakika arobaini na tano kusubiri basi

Yani ni sifuri

Serikali inapiga mdogo sana na ukweli iambiwe

Pia huduma yao ilikuwa ya kizungu ila kadri siku zinaenda inakuwa ya kienyeji yani ni sifuri sifuri sifuri kabisa
 
Fafanua, ni muda gani unasubiri sana na kituo kipi, maana wengine tunatumia hatujaona hiyo hali.
 
Watanzania baadhi tunajidai kujua sana vitu. Kituo kipi ambacho ww unapata usafiri wa mwendokasi bila kero? Acha kukebehi shida tunazopata wenzio.
 
Hilo nalo ni jibu? Ngoja nikusaidie...Mimi natoka Fire naenda kazini Mwenge naunganisha mabasi kituo cha Urafiki. Wewe je?
 
Umeona sasa Fire hakuna tabu ya mwendokasi unaweza kupanda ya Moroko. Lakini sisi wa Kimara na Mbezi tunakoma na haya mabasi
 
Mpaka ubembelezwe ndio useme kituo gani chenye shida? Hata hivyo hujaeleza Kama ni asubuhi, mchana au jioni, na uelekeo upi? Halafu unajiita Great thinker huwezi kujieleza kikamilifu? Unafikiri utasaidiwaje Sasa?
 
Kwa akili zako hizi naacha kukujibu maana haujitambui.
 
Umeona sasa Fire hakuna tabu ya mwendokasi unaweza kupanda ya Moroko. Lakini sisi wa Kimara na Mbezi tunakoma na haya mabasi
Yani huo ndio ukweli, mwendokasi uelekeo wa mbezi kimara kuna changamoto kubwa

Hawa mbezi
 
Usimamizi hafifu
Na haieleweki wanashindwa kiaje hasa,, maana kama pesa wanazikusanya kweli, na mabasi kila mara yanatangazwa yameongezwa

Sasa ajabu hayo mabasi yaliyoongezwa raia hatuoni mchango wake katika ubora wa huduma
 
Nilichokiona mimi wamepoteza target yao, wameweka nguvu kubwa kwa kibaha, kimara mbezi kwa magufuli.so huku kivukoni wamepunguza gari.
 
Watanzania baadhi tunajidai kujua sana vitu. Kituo kipi ambacho ww unapata usafiri wa mwendokasi bila kero? Acha kukebehi shida tunazopata wenzio.

Mjibu labda nyakati anazosafiri yeye huwa hakuto hilo ulisemalo. Anaweza kuwa sahihi kwa upande wake kama wewe ulivyo kwa upande wako
 
Nilichokiona mimi wamepoteza target yao, wameweka nguvu kubwa kwa kibaha, kimara mbezi kwa magufuli.so huku kivukoni wamepunguza gari.
Yani huko unakosema wameongeza nguvu, ndio kerokero kero
 
Back
Top Bottom