Katika kilimo tunakosea nini hadi tunashindwa kutosheleza chakula chetu?

girgirmo

Member
Jan 11, 2017
44
32
Wana jf hapa najua kuna wataalamu wa kilimo. Sisi Watanzania asilimia kubwa ni wakulima, hata uwe mfanyakazi wa ajira sehem fulani baadhi yao wanalima.

Kinachoniskitisha hapa kwani tunashindwa kutosheleza chakula chetu kwa kiwango kikubwa na wakati tunalima? Nchi ya Marekani robo ya watu wanalima mahindi wanawalisha Wamarekani wote na wana export nje ya nchi yao. Kwetu sisi tuna kasoro gani katika kilimo?

Naomba mnisaidie
 
Sisi kilimo chetu ni chakujikimu tu. Halafu sio cha kitaalamu. Halafu tunategemea mvua sehemu kubwa.
 
kwa kilimo chetu cha heka tatu hiki mtu anaona kalima kwa kweli tz bado sana
 
Mkuu umeuliza swali muhimu kuhusu sisi WaAfrica ,ata mimi nimekuwa nikijiuliza kwanini watu wengi wanalima hawafanikiwi, wengi wanafanya biashara hawafanikiwi kama mataifa ya kigeni. Siku moja niliamua kusearch jibu la swali langu google upande wa ufugaji samaki kwanini hatufanikiwi wakati Thailand/Malaysia wamefanikiwa nikakuta majibu mepesi mara maji yetu yana chumvi na sababu kibao. Ila baada ya kusoma material mbali mbali nimeona mambo kadhaa mfano ukosefu wa professionalism katika kilimo au biashara, ukosefu wa nia thabiti, malengo na kujituma kama wenzetu, pia Waafrika tunapenda kuajiriwa kuliko kujiajiri yaani tunaogopa risks za ujasiriamali na biashara na kuridhika sana tunapokuwa na uhakika wa kulipwa mshahara.
 
siasa safi,
wataalamu hawapo huru na wanasiasa,wanasiasa wengi wanawatumia wananchi km mtaji wa muda yaani mtaji wa kura,hivyo wataalamu wengi wanaangushwa na siasa kuanzia ngazi ya chini mpaka ngazi ya juu.
uongozi bora,
hapa kuna suala la bodi za kitaalamu,mgawanyo wa bajeti,vipaumbele, malengo ya muda mrefu na muda mfupi ya taifa,usimamizi wa maadili
watu,
wataalam na wananchi wapo wa kutosha,tatizo ni matumizi sahihi ya wataalaamu,mafunzo kazini,shamba darasa,wananchi kupokea utaaalamu na kuufanyia kazi,motisha km ruzuku na pembejeo bora na sahihi
ardhi
tuna ardhi ya kutosha ila haijapagwa,upangaji wa ardhi kwa matumizi bora ni muhimu ili kujua kanda zipi za uzalishaji na mazao yapi hii inarahisha upelekaji wa wataalamu walio wabobezi kwenye maeneo husika
 
Tupunguze kuingiza siasa katika kila jambo. Lakini pia hamasa kutoka kwa viongozi msimu wa kilimo unapofikia ni jambo muhimu sana. Tunahamasisha zaidi michezo kuliko Kilimo.
 
bajeti kwa sgr ni ndogo imeshindwa kuweka wastani endelevu kwa bei ya mazao ya nafaka, hivyo kuporomoka kwa uzalishaji.
 
Mkuu umeuliza swali muhimu kuhusu sisi WaAfrica ,ata mimi nimekuwa nikijiuliza kwanini watu wengi wanalima hawafanikiwi, wengi wanafanya biashara hawafanikiwi kama mataifa ya kigeni. Siku moja niliamua kusearch jibu la swali langu google upande wa ufugaji samaki kwanini hatufanikiwi wakati Thailand/Malaysia wamefanikiwa nikakuta majibu mepesi mara maji yetu yana chumvi na sababu kibao. Ila baada ya kusoma material mbali mbali nimeona mambo kadhaa mfano ukosefu wa professionalism katika kilimo au biashara, ukosefu wa nia thabiti, malengo na kujituma kama wenzetu, pia Waafrika tunapenda kuajiriwa kuliko kujiajiri yaani tunaogopa risks za ujasiriamali na biashara na kuridhika sana tunapokuwa na uhakika wa kulipwa mshahara.
Kwa kweli wewe umesema vizuri kidogo, kitu cha kwanza ni kuwa wakulima wetu ni kilimo cha kujikim, mtu ana ekari mbili anapata gunia 15, ana watoto 6, kwa sababu ugali ni usiku na mchana basi matumizi yake ni gunia 10, tano ataziuza kwa ajili ya vijisenti, mwaka unaofuata mvua ikizingua tu basi mtu huyu anakuwa na njaa. Pili sisi watanzania tunadhalau kilimo kabisa, mimi ni mfanyakazi lakini nina lakini nina kijaruba kidogo huwa nalima, basi wenzengu wakinikuta shambani wananiambia unajisumbua nini? Si ununue tu, Mimi nawambia nafanya mazoezi, lakini huwezi kuamini hapo kwenye kijaruba napata mahindi hadi gunia nane, hadi nawauzia wafanyakazi wenzangu, Mimi matumizi yangu ni gunia moja tu.
Tatu sisi watanzania ni wavivu, ukimwambia mtu panda vizuri kwa kuzingatia utalaam, kama kupanda kwa mstari, kutumia mbegu bora watu hawataki tena wewe watakuona kama hayawani.
Nne utaona Kijana anatumia smart phone, hawezi kusoma mambo muhimu kama ya kilimo, ufugaji ni. Wewe angalia madaa kama hii wachangiaji wachache, ungeweka mada kama za kijinga kijinga, kwa mfano mtu maarufu amefumaniwa ungeona wachangiaji kibao.
Tano unajua siku za nyuma kilimo kilikuwa kinaonekana ni adhabu, kwani ulikuwa ukifanya kosa unapewa adhabu ya kulima, kwa hiyo vijana wengi wakawa wameweka kichwani kilimo ni adhabu.
Sita kilimo hapa Tanzania na Africa kwa ujumla hakijapewa msukumo mkubwa, bado wanaweka siasa katika kilimo.
Mwisho nasema kilimo ni safi, Mimi tangua mwaka 2011 sijawahi nunua mahindi wala maharage, mwaka huu mvua imesumbua lakini bado akiba ninayo nyingi tu kama ya kula miaka 6 hivi. Tusidhalau kilimo.
 
Mi naweza kuchangia kwa ufupi...

*Kwanza kutoka kizazi cha kwanza hadi cha nne(1st-4th Generation) cha wakulima wetu ni wa kujikimu(peasant) kwa hivyo vizazi ama generation vinarithi mbinu duni za kilimo....unapoja muingiliano na maendeleo ya elimu lazima tu watakidharau.
Thinking ya Mzimbabwe,Mzambia,Mkenya towards KILIMO ni tofauti sana na Mtanzania! Hata perception na akili zao ni tofauti sana. Asilimia 90 ya watanzania wametokea ktk uduni wa peasant economy...hata aelimike vipi hawezi ku-think kama kijana aliekulia anaona babu ,baba wanamiliki mashamba makubwa(Settlers,Farmers) ambayo ni mechanised-Mega tractors,Plantor,Combine Havesters ,Pivotal mobile irrigation,etc. Mtoto huyu ama kijana huyu mawazo yanaenda mpaka kwenye elasticity limit of possibilities....Lakini mtoto wa peasant anaona ni muujiza mtu kumiliki na khudumia eka 200! because siyo business economy oriented ni peasant economy oriented.
*Kingine matatizo ya nyuma yaliyotupata tulishindwa kuya-address vizuri.....mfano moja la bomu ambalo liliathiri akili zetu ni njaa ya mwaka 1974 na 1984....iliathiri sana mama ,baba,na watoto walidumaa akili na mwili...
Akili ya njaa ndio imetujengea kutokujiamini,kuwa duni katika kila jambo....
 
siasa safi,
wataalamu hawapo huru na wanasiasa,wanasiasa wengi wanawatumia wananchi km mtaji wa muda yaani mtaji wa kura,hivyo wataalamu wengi wanaangushwa na siasa kuanzia ngazi ya chini mpaka ngazi ya juu.
uongozi bora,
hapa kuna suala la bodi za kitaalamu,mgawanyo wa bajeti,vipaumbele, malengo ya muda mrefu na muda mfupi ya taifa,usimamizi wa maadili
watu,
wataalam na wananchi wapo wa kutosha,tatizo ni matumizi sahihi ya wataalaamu,mafunzo kazini,shamba darasa,wananchi kupokea utaaalamu na kuufanyia kazi,motisha km ruzuku na pembejeo bora na sahihi
ardhi
tuna ardhi ya kutosha ila haijapagwa,upangaji wa ardhi kwa matumizi bora ni muhimu ili kujua kanda zipi za uzalishaji na mazao yapi hii inarahisha upelekaji wa wataalamu walio wabobezi kwenye maeneo husika
ardhi kwetu sio ttz mkuu bali km nchi kilimo sio kipaumbele na weng tukizungumzia kilimo hatujuu tunamzungumzia nani lkn bado km nchi inawajib wa kuhakiksha zanq na pembejeo za kilimo zinapatikana na uwekezaji wa kweli kwenye umwagiliaj na si vingnevyo na sisi km wa wakulima ni wavivu jmn!
 
Back
Top Bottom