Katika katiba mpya naona hili mumesahau hamukuona umuhimu wowote !

GHIBUU

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
4,432
3,006
Nimefatilia mijada ya katiba mpya, kila nikiangalia watetezi wa wananchi kuna mambo bado yanasahaulika katika kumkomboa mwananchi kutoka katika umasikini.
Suala la rasilimali.

Nilitegemea kuona mtu au jumuiya au chama cha siasa au kitengo chochote cha kiraiya kinaweka mbele maslahi ya wananchi, kwa mfano rasilimali.

Nilitaka kuona kuwa rasilimali zinapendekezwa kuwa mali za wananchi hivyo basi serikali iweke asilimia zaidi ya 30 kuenda kwa wananchi, tena asilimia hizo zijikite katika kumtoa mwananchi katika ukali wa maisha, kama makazi, serikali iwe inajenga makazi na kuwapa wananchi bure bila ya ubaguzi kwa mikoa yote, kwa wale wenye uwezo yaani kazi iwe amejiajiri au muajiriwa alipia asilimia ndogo kwa serikali au iwe bure kabisa au kama anataka kununua auziwe kwa bei ya chini kabisa.

Hi itasaidia kupunguza ukali wa maisha,pili suala la elimu, katiba mpya itoe ursa kima mwananchi ana haki ya kupata elimu kwa age yoyote bila ya ubaguzi, elimu hadi ya juu na bure, kuwe na utaratibu maalum.

Tatu huduma ya afya, serikali ihakikishi kila mikoa kuna hospitali ya rufaa badala ya kutumia hospital ya muhimbili tu, huo unakuwa ni mzigo mkubwa kwa taifa ambalo lina watu milioni 44, huduma ziwe bure, na serikali iweke kipao mbele kuwatoa elimu ya udaktari ili kuweza kutoa huduma hizo kwa wananchi.

Huduma zozote zinazotolewa na serikali katiba mpya ikane kabisa kwa chama cha siasa kujitolea sifa kwa hilo kwani kikatiba hilo sio juhumu la chama cha siasa bali lipo kikatiba, hivyo vyama vya siasa hutumia mwanya kuwarubuni wananchi eti wamewaletea maendeleo na kuweka ubaguzi katika vyama vyengine kushindwa kuwaletea maendeleo, kwani mendeleo yote yako kikatiba na nilazima kila mwananchi apatie huduma zote,iwe maji, barabara, elimu , huduma ya afya na mengine.

Na mwisho kwa kumaliza nimeona wananchi wakitoa maoni kuwa rasilimali ziwaaidishe wananchi lakini kulikosekana kwa kina kueleza vipi wanufaike, huo ndio muono wangu katika kutengeza katiba mpya.

Nawakilisha.
 
Pamoja na mawazo yako mazuri, je Wewe ni Mtanzania? Je umeshatoa maoni yako? Umelifikisha hilo?
 
Nawakilisha.[/QUOTE
Mbona hata ilivyo sasa rasilimali zilizopo ni mali ya wananchi na wajibu wa serikali mahali popote ni kuhakikisha mali hizo zinagawanya vizuri. Tatizo ni vipaumbele vya serikali iliyoko madarakani ambavyo huwezi vijumlisha kwenye katiba.
 
Mawazo kama haya ni magumu mno kwa maisha ya mtanzania. Kama pamoja na kukusanya kodi zote watu bado wanachota maji ambayo hata kuogeshea mifugo siwezi kukubali ndo watatujengea nyumba? Wameshindwa kusecure health system kwa watz wote?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom