Katika historia ya AFCON

Polycarp Mdemu

Senior Member
Jun 2, 2019
165
209
Mahmoud El-Gohary na Stephen Keshi ndio watu pekee ambao waliwahi kutwaa ubingwa wa AFCON wakiwa kama Wachezaji, pia kwakuwa kama Makocha.

Mahmoud El-Gohary yeye alitwaa ubingwa kama mchezaji mwaka 1959, pia akatwaa kama kocha mwaka 1998, Mara zote mbili akiwa na timu ya taifa ya Misri.

Stephen Keshi yeye alitwaa ubingwa kama mchezaji mwaka 1994, pia akatwaa kama kocha mwaka 2013, Mara zote mbili akiwa na timu ya taifa ya Nigeria.

Aliou Cisse yeye kwa bahati mbaya alifika fainali ya AFCON akiwa kama mchezaji wa Senegal mwaka 2002, pia kwa bahati mbaya akafika fainali mwaka 2019 na kupoteza akiwa kama kocha, Kwa bahati nzuri 2021 akatwaa ubingwa huko kama kocha wa Senegal.
 

Attachments

  • Aliou_Cissé_2018.jpg
    Aliou_Cissé_2018.jpg
    22.8 KB · Views: 1
  • 2012-634822793102947172-294.jpg
    2012-634822793102947172-294.jpg
    17.1 KB · Views: 1
  • DfGLlE3UwAAb-E8.jpeg
    DfGLlE3UwAAb-E8.jpeg
    49.7 KB · Views: 1
Back
Top Bottom