KATIKA HILI, SHERIA ZA KAZI ZINASEMAJE?

Ulimbo

JF-Expert Member
Aug 14, 2009
3,767
4,035
Kuna kampuni Ngare investment – Wamiliki wa hoteli ya NATRON PALACE iliyopewa uwakala wa kukusanya ushuru wa maegesho ya magari Arusha inawanyanyasa wafanyakazi wake.

Tangia wapewe tenda hiyo mwezi julai mwaka huu 2018, wamekuwa wakiwanyanyasa wafanyakazi – (Wakusanya ushuru) na baadhi yao wamesha acha kazi.

1: Wafanya kazi hawana mikataba ya kazi.
– wanaambiwa kuwakampuni imesaini mkataba wa mwaka mmoja na almashauri ya jiji, hivyo hawana sababu ya wao kuwa na mkataba na kampuni kwa kisingizio kuwa nao pia mkataba wao ni wa mwaka mmoja.

2: Wafanyakazi hawalipwi mishahara yao kwa wakati
- Mshahara wa mwezi wa saba hawajalipwa, wale waliocha kazi tu ndio wamelipwa.

3: Husipofikisha kiwango ulichopangiwa, utakatwa kwenye mshahara wako.
- Mshahara wao ni 150,000/= kwa mwezi. Kila mkusanya hushuru amepangiwa kiwango cha kukusanya kila siku, kuanzia 20,000/= hadi 150,000/= kulingana na eneo ulilopangiwa.
- Viwango hivi vimepandishwa mfono 20000/= hadi 25000 au 28000. Kama husipo fikisha hiki kiwango kwa siku, basi unakatwa kwenye mshahara wako na unaambiwa usahini kamaumechukua advance - umechukua sehemu ya mshaara kabla.
Kuna kipindi wafanyakazi walitaka kugoma, ila wakaambiwa watashughulikia hilo tatizo.
Kilichofuata ni kwamba walihitwa mmoja mmoja na kuulizwa kama anataka kazi au alipwe hela yako aondoke. Kuna ambao walilipwa wakaondoka, ila wengine walishindwa kuacha kazi kutokana na hali ya maisha na pia wanategemewa na familia.

WITO:
Naomba idara ya kazi Arusha ifuatilie ili jambo kuwanusuru haw ndugu zetu.
 
Hali ya maisha ni ngumu. Wegi wao wanategemea hicho kipato kuendeshea maisha
Hiyo kampuni inajihami, wanaogopa wasipopata tenda hiyo tena watawalipa nini? Labda kama hiyo kampuni inshughuli nyingine mbali na hiyo.
 
Hiyo kampuni inajihami, wanaogopa wasipopata tenda hiyo tena watawalipa nini? Labda kama hiyo kampuni inshughuli nyingine mbali na hiyo.

Maelezo ni kwamba kampuni iliweka dau kubwa ili wapewe tenda hiyo bila kuangalia hali halisi ya soko.
 
Wap
Maelezo ni kwamba kampuni iliweka dau kubwa ili wapewe tenda hiyo bila kuangalia hali halisi ya soko.
unguze hizo tenda na kama ni sababu za uchumi wawape redundancy ili wawalipe mafao hawataki wapelekeni Cmamkafungue mgogoro wa madai.
 
Back
Top Bottom