Katika hili mlichemka pakubwa sana, haiwezekani tozo izidi kodi ambayo ipo kihalali

Kingsmann

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
3,099
2,000
Hebu angalia gharama hizi za huu muamala hapa chini

IMG_20210720_140215_1626779593289~2.jpg


👉Gharama ya muamala(kodi) = 3500/=
👉Tozo ya mshikamano = 7500/=


Hii uliona wapi? Hata kama ni uzalendo huu sasa ni unyanyasaji, hata kama ni mshikamano huu sasa ni mshikwamano. Yani tozo ambayo kiuhalisia ilipaswa iwe hiari inakuwa mara 2 ya kodi ya muamala husika?

Katika uhalisia tuu wa maisha, hata kwa ambaye hajasoma uchumi, angeambiwa apendekeze tozo ya mshikamano basi angependekeza japo nusu ama robo ya kodi husika kwenye kila muamala. Kwanza nusu ni kubwa sana, angeanzia kwenye robo na kurudi chini.

Mfano kama kodi ya muamala husika ni 4000/= basi nusu ni 2000/= na robo ni 1000/=. Kama tozo ya mshikamano ni robo ya kodi ya muamala husika basi jumla ya makato ingepanda kutoka 4000/= mpaka 5000/=. Hii tozo ingekuwa himilivu na isingeleta shida sana.

Lakini eti tozo ya mshikamano inakuwa mara 2 ya kodi ya muamala husika? Hii hata mjinga ambaye hajaenda hata darasa la kwanza asingethubutu kupendekeza aina hii ya tozo. Asingethubutu hata kidogo.

Ina maana serikali hapa ilitaka itengeneze faida mara 2 ya makampuni husika? Ama lengo lao ni nini hasa? Yani kodi nilipe 3500/= kisha tozo ya mshikamano nilipe 7500/=? Like seriously? Yani tozo ni mara 2 ya kodi ya muamala husika? Aisee Mwigulu hauwezi kuwa serious hata kidogo.

Ningekuwa mimi ndio waziri niliyeleta hii kanuni na basi ningeshaachia ngazi mapema sana, maana hapa ni zaidi ya kuboronga.
 

arch81

JF-Expert Member
Sep 20, 2017
358
500
Hawa wanamfitinisha raisi na wananchi kwa koto la uzalendo pia washauri wake wameshindwa kumshauli
 

Tempus Fugit

JF-Expert Member
Jun 22, 2016
524
1,000
Hiyo gharama ya muhamala 3500 TZS si kuwa yote ni kodi. Hiyo ni service charge ambayo ndani yake ndimo kuna kodi ya serikali. VAT imo ndani ya hiyo 3500.

Yaani inamaanisha ktk hiyo 3500 kuna hela ya kampuni inayotoa huduma na kuna kodi ya serikali. So kodi iliyopo hapo ni ndogo na affordable.
 

Flano

JF-Expert Member
Aug 7, 2019
683
1,000
Mama tunampenda na tuna matumaini makubwa sana juu yake, ila awe makini sana tena saaana na hawa washauri na wasaidizi wake, akifanya nao masihara watamfitinisha na kumgombanisha mama na watoto wake.
 

Manjagata

JF-Expert Member
Mar 7, 2012
8,123
2,000
Shetani unayenishawishi niitukane serikali na mwigulu nchemba ushindwe.
Maana naona kabisa unaniambia mtukane, mtukane , mtukane maana kafanya maamuzi ya kiwendawazimu
Mkuu kutukana watu siyo vizuri, lakini katika hili hata Mungu atakuelewa! Tukana tu!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom