Katika hili la Mwangosi, Rais Kikwete ameonyesha udhaifu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katika hili la Mwangosi, Rais Kikwete ameonyesha udhaifu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Digutu Wamunu, Oct 11, 2012.

 1. D

  Digutu Wamunu Member

  #1
  Oct 11, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni aibu iliyoje kuona haya mambo ya ajabu yanatokea katika utawala wako, halafu hakuna kiongozi wa serikali mwenye mamlaka husika anayeweza kukemea uwongo huu wa mchana kweupe na mbele ya umma.

  Haiwezekani hata siku moja watu wenye taaluma za hali ya juu, ambao wanategemewa na jamii ya watanzania kuja mbele ya umma, bila hata aibu na kuwasomea ripoti iliyojaa upumbavu na vioja vya aina yake dhidi ya mauaji ya Mwangosi. Polisi wameua mchana kweupe, picha zipo, halafu bado serikali imetumia KODI ZA WANANCHI kwa kuandaa ripoti hii. Ile ripoti hata ungewatuma wanafunzi wa darasa la saba wangeweza kufanya kazi nzuri zaidi.

  Haya yote yasingefanyika katika nchi hii kama wewe usingekuwa dhaifu. Familia yoyote ile yenye wazazi werevu na wenye msimamo, kamwe haileti upumbavu. Kwani watoto wanajua wakileta mchezo tu watapata adhabu kubwa. Sasa wewe watendaji wako katika wizara zilizo nyingi wanajua udhaifu wako, wanajua kamwe huwezi kutoa adhabu, badala yake utawalinda. Ndio maana wanakula kulingana na urefu wa kamba yao. Wametugeuza watanzania kama jamvi la kukalia.

  Kuna mambo 2 ambayo yanaweza kuwa yamefanyika na kupelekea ripoti iandikwe kijinga namna ile;

  1. Mheshimiwa Rais Mrisho Jakaya Kikwete alitoa amri kwa Dr Nchimbi kuwa naomba ufanye kila uwezalo ili upepo huu upite. Maana nakujua vizuri sana Dr Nchimbi kwa Phd yako ya kuunga unga utaweza tu kuwapa changa la macho hawa watanzania mambumbumbu.

  2. Dr Nchimbi (kwa ridhaa yake mwenyewe) aliwapa amri kwa hawa wanakamati kuwa mtapewa posho zenu, lakini msitoe mchango wowote katika kuchunguza haya mauaji, bali mimi nitajua namna ya kuandaa ripoti ya kuwaridhisha hawa walalahoi ambao ni sisi watanzania

  Iwapo ni namba (1) ndio kilichotokea kupelekea kuleta ripoti hii ya kijinga na ni uwongo wa wazi, basi ni dhahiri kuwa wewe Rais Kikwete ni dhaifu wa kutupwa. Tena ni muuaji wa hali ya juu ambapo unang'ata na kupulizia.

  Kwa rais ambaye ana misingi ya uongozi na utawala bora, kamwe asingeweza kukaa kimya kwa hili tukio la kinyama lililosababishwa tena kwa makusudi mazima na chombo cha kuwalinda wananchi na mali zao. Lakini kwavile wewe ni kiongozi dhaifu tena wa kutupwa ndio maana umekaa kimya. Katika hotuba yake mheshimiwa rais ya mwisho wa mwezi wa (9) rais aliongelea kama vile anapita njia, wala hakuona kama ni jambo ambalo si la kawaida. Na wiki hii ripoti mbovu imetolewa tena ya kulidanganya taifa, lakini Kikwete kwake ni kawaida. Kweli Kikwete ataipeleka nchi yetu ya Tanzania pabaya sana kwa udhaifu wako.

  Hii ni ishara kubwa kwamba Wizara zote kwa Tanzania hii wanaendesha mambo kienyeji na kadri wanavyotaka, wakijua kuwa hakuna wa kuwauliza. Wanajua kuwa wewe ni dhaifu, na ukisoma ripoti ya kijinga kama hii ya leo ambayo ni kuwanyanyasa watanzania waliokupigia kura, wewe lazima utawachekea na kusema – mmefanya kazi nzuri sana vijana wangu!

  Kwa hili ni vyema mkaliangalia upya, kabla watanzania hawajaanza kuchukua sheria mkononi na kuharibu hali ya Amani na utulivu ambayo tulijua tunayo.

  Sasa ikiwa ni namba (2) ndilo lililofanyika, basi hiki ni kigezo tosha cha kuonyesha ni jinsi gani Tanzania yetu ilivyojaa viongozi waliooza, na ambao wanafanyakazi kwa maamuzi yao binafsi, ya kulinda maslahi yao binafsi. Kwamba yeye hapa haangalii tukio lilivyotokea, akaguswa, na kuwajibika ipasavyo kwa misingi ya uongozi bora kwa taifa zima kupitia Wizara yake.

  Busara kwa Dr. Nchimbi ingekuwa ni kuwawajibisha wale askari wote waliohusika, pamoja na RPC wa Iringa kwa kuwafukuza kazi na kuwapeleka mahakamani ili sheria nayo ichukue mkondo wake. Mara baada ya kupata taarifa Dr. Nchimbi alipaswa kukiri mbele ya watanzania kuwa kweli Jeshi la polisi haliko tayari kuendelea kuwaajiri hawa askari kwani hawakufuata maadili na taratibu za kazi.

  Na kwamba RPC wa Iringa alionyesha kuwa na chuki binafsi dhidi ya marehemu Daudi Mwangosi, ambapo ni kinyume na taratibu za kazi (completely unprofessional) kwake yeye kuchukizwa na maswali magumu ambayo waandishi wa habari wanamuuliza, ambayo ni kwa ajili ya maslahi ya wananchi na taifa zima.

  Badala ya kuonyesha upeo wake katika kufafanua hayo mambo, yeye anaamua kum-attack mwandishi mmoja mmoja. Hivyo nae hafai kuendelea na kazi yake, hususani kwa ukatili alioufanya wa kushuhudia Mwangosi akiuawa bila hata yeye kuwajibika kwa nafasi yake.

  Iwapo angefanya hivi, watanzania wengi naamini wangeelewa. Hata kama tuliumia kwa jinsi Mwangosi alivyouawa kinyama, lakini kwavile mamlaka husika kupitia Dr Nchimbi ambaye ni mwenye dhamana ya Jeshi la Polisi amekiri kuwa halikuwa jambo jema, na kamwe halitarudia tena. Hii ni njia rahisi na haikuhitaji gharama yoyote, wala haikuhitaji tume. Huu ni utashi wa kawaida iwapo kweli hawa viongozi wangekuwa wako kwa ajili ya maslahi ya taifa na si ubinafsi.

  Kwa nia njema tu, ni vizuri ukaachia ngazi kama mambo huyawezi, tena litakuwa jambo jema na la BUSARA. Maana hatukuzoea kuyaona haya katika historia ya viongozi wetu wote waliopita. Pia hatutaki kuingia katika vita dhidi ya serikali na wananchi wake. Tanzania ni nchi ya Amani, lakini udhaifu wako utasababisha hili neno AMANI litoweke katika fikra za watanzania.
   
 2. p

  politiki JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Utabiri wangu kitakachotokea ni kwa RPC kustaafu na marupuru wakati yeye ni criminal hicho ndicho kinachosubiriwa kutokea kwa hivi sasa.
   
 3. B

  Bahati Risiki JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 531
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Yani wewe unampigia tu mbuzi gitaa ili acheze. Huyu JK ni dhaifu kweli kweli wala hatakusikia. Hizo bembea na matoroli ya farasi vinamchnganya ndiyo maana kina Nchinbi wanajifanyia mambo yao wanavyoona.

  Ni bora akajua Tanzania ya leo sio ile ya jana. Kuna siku moto utamwakia na wala hataweza kuuzima. Yeye aendelee tu na ushemeji atajajuta sana maishani mwake kwani vita haina macho hata kidogo.
   
 4. Bitabo

  Bitabo JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 1,896
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Mkuu karibu sana JF

  Nimegundua kuwa kuendelea kumuita JK dhaifu ni kumuonea sana.
  DHAIFU NI SISI WANANCHI tuliompeleka Ikulu wakati tukijua fika kuwa hata kuwa katibu kata hafai na kilichotuponza ni kanga, kofia, tshirt ila kubwa zaidi ni ubwabwa wa bure na mwishowe tukaiuza nchi yetu.


  TAFAKARI NA CHUKUA HATUA
   
 5. G

  Gwakisa Mwandule JF-Expert Member

  #5
  Oct 11, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 520
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ee bwana huwa najua hii nchi raisi zoba kuliko vichaa wa majalalani lkn ktk hili la mwangosi na nchimbi nimejua kuwa huyu sio raisi mjinga ila ni muuaji na mpenda vifo na ni hatari kuwepo hapa duniani!ee mungu uliumbaje aina hii ya ujinga na uovu wa huyu mnyama jk?Ee mungu tunakuomba tuongoze ktk kuwatanguliza mbele za jehanamu au atutangulize na sisi kama mwangosi kwa mapenzi yako wewe lkn usitufanye kuwa marafiki wa shetani huyu wa Tz Aaaamin
   
 6. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  sema wewe ndo dhaifu,mi hata angegombea na jiwe ningepigia jiwe kuliko huyu mzee wa farasi
   
 7. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #7
  Oct 12, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Nchimbi nae Dhaifu
   
 8. Bartazar

  Bartazar JF-Expert Member

  #8
  Oct 12, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 805
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  Katika hili ameonesha udhaifu? Kwani ni yepi aliyoonesha yupo strong?
   
Loading...