Alikuwa hana sababu ya msingi ya kuwaambia watanzania kuwa ndiye mshindi wakati ukweli anaujua na alikuwa anaendekeza hasira za kabila lake. Idadi ya Wabunge wa CDM ndo kipimo tosha hata kwa mtoto mdogo kama wewe kuwa kura alizopata SLAA ndiyo ilikuwa stahiki yake na si vinginevyo. Hakuna mwananchi ambaye angemwaga damu wakati wengi wanajua walimpigia JK.
Ni kweli sifa mojawapo ya kiongozi bora ni kuwa na busara hata hivyo hakuna busara inayoruhusu kukubali kuporwa haki.
samahani kaka le mutuz ndio mdudu gani?uchambuzi mzuri dogo, upo kidato cha 5 au 6 bilashaka ila uchambuzi wako umeenda shule hasa, umewazidi hata le mutuz aliyekaa ulaya miaka 30 na madigrii yake hahahahahahaha
2008 uko form leo umeua form six.... That doesnt add up
Safi sana kijana, unaona mbali.
Karibu M4C
Dogo umetisha! Kila la kheri
Ulivyopangilia hoja umethibitisha kwamba wewe si wa sekondari za kata a.k.a saint kayumba. Kama nimekosea dogo H ataniambia. Ki ukweli dakt Slaa sio tu anastahili sifa bali Anastahili heshima.Dakt ni msumari wa moto kwenye masaburi ya magamba
mpuuzi mmoja hivi babake aliwahi kuwa waziri mkuu....samahani kaka le mutuz ndio mdudu gani?
hivi inakuwaje dogo kama huyu anamzidi akili libaba kama nchemba?nimeamini kuna shahada za kufoji
Leo nimevuta fikra sana na hatima yake nimeona Slaa anastahili sifa na ikiwezekana anafaa kuwa rais wa nchi yetu.
Kikubwa zaidi kilichonifanya niseme hivi ni baada ya kukumbuka majirani zetu Kenya mwaka 2008 nikiwa kidato cha kwanza.Katika uchaguzi uliofanyika mwaka huo, Kibaki Mwai ndo alitangazwa mshindi dhidi ya Odinga Raila. Kutokana na madai ya kuwa Mwai hakushinda kwa uhalali, Odinga aliwaambia wafuasi wake kuwa yeye ndiye alikuwa mshindi na badala yake wananchi walimwaga damu.
Pia kumbukumbu yangu ikanijia kufikiri tukio jingine hapa kwetu Z'bar. Sharif Hamad alidai kuwa ktk uchaguzi uliofanyika mwaka 2000, yeye ndo alikuwa mshindi na hatimaye wazanzibar walimwaga damu isivyo kifani.
Ninachotaka kukizungumzia hapa ni kwamba,kiongozi anaweza akawa msomi,mwenye lundo la shahada na hata masters lakini bila kuwa na hekima na busara,huyo mtu hafai.Kiongozi anayekuwa hana huruma na roho za binadamu ama analazimisha siasa hadi kwenye uhai,huyo hafai.
Kwanini nimesema Dr Slaa anafaa kusifiwa?
Katika uchaguzi huu uliofanyika mwaka 2010 nikiwa kidato cha tatu umenifanya nimpende Slaa na kummwagia sifa kemkem japo bado nipo mwanafunzi na sijaijua vizuri siasa lakini kwa hili imenibidi leo nivunje ukimya. Tuhuma nyingi zilionekana kuwa Slaa alikuwa na kura nyingi katika majimbo mengi na hivyo angeamua kuwaambia mashabiki wake kuwa yeye ndo alistahili ushindi, sidhani kama vita vingekosekana kama kenya na Z'bar.
Mwenyezi Mungu amjalie 2015 aweze kuichukua nchi maana hata mimi nitakuwa ndiyo kwanza nimemaliza kidato cha sita hivyo nitakuwa na muda kumpigia debe. Dr Slaa ana uamuzi mzur wenye hekima na busara.Nampenda sana Slaa.
sasa siwezi kukumbuka kichwani.ukitaka undani wa data hizi nenda ofisi za tume ya uchaguzi.iko pale posta ukifika ulizia tu utaoneshwa.kwa swali moja ni kuwa kura za Slaa hazijulikani na wala za JK hazijulikani sio tume ya uchaguzi wala kwene vyama vyao wala kwa msajili wa vyama mfano niambie matokeo ya urais jimboni kwako Jk alipata ngapi?
tembelea ofisi za tume ya uchaguzi uwaombe makabrasha ukatoe copy.Nidyo maana watu mnafeli mtihani.
Hukuombwa matokeo ya URAIS wa Tanzania mwaka 2010 kwa ujumla. Amekuomba matokeo ya Urais wa Tanzania mwaka 2010 kwa KILA JIMBO. Wewe unatoa ya jumla, sijui huwa mnawahi nini kujibu bila kusoma?
Ni heri wala usingelijibu kabisa kuliko kuweka jibu ya swali ambalo hujaulizwa.
Faida ya Baiskeli ni nini? Jibu: "Spoko za Baiskeli ni nzuri sana kwa kufanyia mishikaki."