PreGE2025 Katibu wa Organaizesheni CCM Issa Haji Gavu: Wajumbe msichague viongozi legelege kwenye kura za maoni

PreGE2025 Katibu wa Organaizesheni CCM Issa Haji Gavu: Wajumbe msichague viongozi legelege kwenye kura za maoni

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Katibu wa NEC - Oganaizesheni wa CCM Taifa (MCC) Issa Haji Ussi Gavu leo tarehe 23 Juni 2025 ameshiriki Mkutano Mkuu Maalum wa Jimbo la Kinondoni Jijini Dar es salaam, akiwa Mgeni Rasmi, uliofanyika katika Ukumbi wa Ubungo Plaza

Katika mkutano huo, Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Tarimba Abbas amewasilisha taarifa yake ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka (2020 - 2025)

Cde. Gavu amesema CCM kinawataka Wajumbe kuhakikisha katika kura za maoni hawachagui kiongozi legelege kwakuwa hatokuwa chachu ya upiganiaji maslahi ya Wananchi anaowaongoza, maslahi ya CCM na maslahi mapana ya Taifa kwa ujumla

Amesisitiza kuwa Viongozi wanahitajika kuendana na misingi ya utawala bora, uzalendo, uadilifu na kujitoa pasipo kusahau kukubali kukosolewa

“Tusije kufanya kosa la kujihakikishuia uongozi kwa nafasi za dola (ubunge na udiwani), siasa ya CCM kabla ya uchaguzi inakua kwenye majukwaa ya kisiasa kama vyama vingine na kupambana kwa sera na hoja, tukimaliza uchaguzi siasa ya CCM inahamia kwenye mabaraza ya madiwani na bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania"

“Mkichagua watu legelege maana yake mnapeleka watu wa siasa legelege kwenye baraza la madiwani na bunge

“Haiwezekani kumpeleka mtu kwenda kugombea nafasi za uongozi kupitia chama chetu ambaye hata chama chenyewe hakijui, hajui kamati ya siasa ni nini, halmashauri kuu ni kikao gani, mkutano mkuu ni nini haiwezekani"-amesema Issa Haji Ussi Gavu
-
 
Hahaha wakakamavu wasimsahau Mwijako, baba levo na msambwanda.
 
Back
Top Bottom