Katibu wa BAVICHA Njombe Kusini afariki dunia!

Katibu wa BAVICHA Njombe Kusini afariki dunia!

Nashawishika kusema huduma hafifu kwenye zahanati/vituo vyetu vya afya vimechangia kwenye kifo cha huyo kijana.Very sad.

Nitoe pole wa ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu lakini zaidi nitoe pole kwa wazazi wa kijana. Ni huzuni iliyoje kwa mzazi kumzika mtoto? Mungu awape faraja. RIP kijana.
 
Mwenyezi Mungu amrehem mwendazake,ampokee kwny nuru ya uso wake.Pole kwa wafiwa na twawaombea faraja ktk kipindi hiki cha majonzi mazito na makamanda wote wa njombe kwa ujumla nawapeni pole kwa msiba mzito kwakuwa amepungua mpiganaji mwenzenu ktk kupgania haki na usawa ktk eneo lenu.MUNGU awape moja wa subira na kutokata tamaa,daima atawaleteeni makamanda wengine wa kushirikiana nao.roho ya mwendazake ipumzishwe mahala pema peponi.amen
 
Huyu hajafa mbona jamani mnamlalamikiaaaa! Ukweli huyu kapumzika tu wanaokufa ni wa "SISI M", wenye miroho mibaya, walevi wa madaraka, vipofu wa utawala bora, wabakaji wa rasilimali za taifa. Bwana hebu mwandalie huyo bwana mdogo makao yake.
 
Bwana ametoa

Bwana ametwaa

Jina la bwana lihimidiwe



Raha ya milele umpe eeh bwana na mwanga wa milele umwangazie......Apumzike kwa amani AMINA!
 
Katibu wa Bavicha Jimbo la Njombe Kusini (Njombe Mjini) kwenye Mkoa mpya wa Njombe, Jackson Mtakimwa amefariki dunia usiku wa kuamkia leo kwenye Zahanati ya TANWALT mjini Njombe. Septemba 25 mwaka huu Mtakimwa alipata ajali ya Pikipiki aliyokuwa anaendesha na kupata majeraha ya mwilini na kichwani.

Alifikishwa kwenye Hospitali ya Wilaya (Kibena Hospital) ya Njombe ambapo alitibiwa majeraha hayo na kuruhusiwa kurudi nyumbani. Mtakimwa alikuwa ni mmojawapo wa Makamanda waliokuwa waende kusaidia Kampeni za Udiwani kwenye Kata ya Mlangali Wilaya ya Ludewa lakini aliachwa kutokana na hali yake kutotengemaa.

Juzi alianza kukohoa na kutoa damu (inawezekana alipata majeraha ya ndani kwa ndani wakati wa ajali) na alipelekwa kwenye Zahanati ya Tumaini Mjini Njombe ambapo matabibu walidai ana Typhoid hivyo kuhamishiwa kwenye Zahanati ya kiwanda cha TANWALT mpaka mauti yalipomkuta saa saba usiku wa kuamkia leo.

Jackson Mtakimwa atazikwa kesho kijijini kwao Igwachanya (Njia Panda ya Tosamaganga) kwenye Jimbo la Kalenga, Wilaya ya Iringa Mkoa wa Iringa.
Dah! R.I.P Kamanda:

ila kamanda pamoja na kuwa na historia ya ajari lkn pia hao watu wa Tumaini Dispensary inawezekana kuwa wame-speed up kifo chake, wanafanya kazi kwa kubahatisha tu. Mi nilishawai kupeleka familia yangu kucheki afya mmoja alikua anawashwa mwili, mwingine alikua ni mtoto nilitaka apime uzito kama klinik ya kawaida kwa wototo na mwingine alikua aumwi ila aliamua kucheki tu marelia lakini wote waliambiwa kuwa wanasumbuliwa na minyooo; walipatiwa dozi kwa dawa ambazo tangu nimekua sijawahi kusikia kwamba zinatibu minyoo, kibaya zaidi formula ya umezaji wa dawa hizo ilikua ni moja kwa wote: nilibishana nao baada ya kugundua hilo ndipo Mganga Mkuu aliingilia kati kuniomba msamaha na hatimaye kunirudishia pesa nilizokuwa nimetoa.

R.I.P Kamanda
 
Madaktari wa voda fasta bwana, mgonjwa amepata ajli anakohoa damu afu unamtibu kama typhoid dah, mimi naona huyu kamanda amefariki kwa uzembe, na hata hospital waliko mdischarge immediately hawakutenda haki, kama mtu kapata majeraha ya kichwa anatakiwa alale hospital at least 24hrs then unaona kama hakuna danger sign then una mdhome, sasa voda fasta hizo. Tukigoma wanaona hatutaki kufanya kazi, ndo mjue sasa kuwa tunachotaka sisi ni huduma bora na si bora huduma.
 
pumzika kwa amani Kamanda: hivi kuna uhusiano wa typhod na kukohoa damu? kwa nini zahanati na si hospital ya wilaya? kweli siku yako ikifika imefika tu
 
kwanini viongozi wa chadema wanakumbwa sana na ajali za barabarani za mara kwa mara?
Wewe lazima utakuwa mchawi. Any way nilibahatika kufanya kazi na huyu kamanda. Nimepatwa na simanzi sana niliposikia habari hii, poleni makamanda wote hasa Thomas Nyimbo, Sagasaga na Alatanga Nyagawa lutondwe
 
Last edited by a moderator:
Pumzika kwa amani kamanda,umetangulia nasi tutafuata.
 
Back
Top Bottom