TANZIA Katibu Tawala Arusha, Bw. Richard Kwitega afariki Dunia

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,797
11,959
Salaam Wakuu,

Habari Mbaya ni kwamba Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Bw.Richard Kwitega amefariki Dunia kutokana na ajali.

1.jpg

Richard Kwitega kafariki alasiri ya leo kwa ajali ya gari katika kituo cha afya cha Magugu. Alikuwa anaenda Dodoma Kikazi, alipofika maeneo ya Mdori Manyara gari lake iligongana na Basi la Makala uso kwa uso, basi lilikuwa linalotoka Babati.

Baada ya ajali akakimbizwa kituo cha afya cha Magugu ili baadaye apelekwe Babati kwa matibabu zaidi.

Ilipofika saa tisa na dakika 50 akafariki Dunia. Mipango inafanyika ya kuurudisha mwili Arusha.

Apumzike kwa amani.
2.JPG


3.jpg
4.jpeg



22830FFD-658C-462C-800B-6EDB615A9257.jpeg
 
Back
Top Bottom