Katibu mwenezi wa CCM Longido ajivua gamba

Mpaka 2015 Chama Chama Magamba atakuwa amebakia Fisadi wa Magogoni na House boy wake Nape pamoja na Majambazi
 
Wadau ngoja niwasiliane na huyu bwana maana nimekuwa nikimtafuta kwa skype maana yupo USA jimbo la Indiana na sijui amekuja Tanzania lini au amepiga simu but wacha nimtafute maana ni mtani wangu kwa upande wa siasa ni pro CCM na amekuwa akisema kadri siku zinakwenda anachoka madudu ya CCM.
 
Ukisikia yalaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaah, ujue limempata huyu, na bado tutavuna wengi tu, polepole wameanza kujua
 
Huyu dogo amesema kweli, leo nimeona gazeti la jambo leo limeandika Cdm ni chama cha freemason. Wameweka picha za viongozi wa nchi flani flani wanaonyesha alama ya vidole viwili. Pia wamemweka hadi papa benedicto wa 16. Wameandika Dr. Slaa ana jini sebuleni. Ki ukweli leo nimejisikia vibaya kuona zile habari ila kwa sababu najua jambo leo ni gazeti la serikali nikajua ni mkakati wao wa kuidhoofisha Cdm ambapo hata hawawezi. Gazeti la jamba leo ni uchafu kabisa. Huyu dogo wa Longindo ndo atamwondoa Lekule Laizer welcome kijana.
 
Jamani hizi habari ziko kwa uhakika? Maana nataka kumshawishi kamanda wangu ambaye ni askari aingie kwenye mpambano na magamba coz yupo tyr kuacha kazi ili asiendelee kuwasujudu magamba!
 
Wakuu, EL akigombea 2015 basi tuna jimbo maana M4C eneo la MTO-WA-MBU inatisha balaa, na 40% ya wapiga kura wanatoka eneo hilo. Kama mnahesabu majibu na hilo mliweke. M4C brings changes for sure.
 
Wakuu magamba yanazidi kupata moto. Katibu mwenezi wa vijana wilaya ya Longido Ndugu YOHANA LAIZER ameamua kuhama ccm na bado hajaweka wazi atajiunga na chama gani. Katibu huyo anadai kachoshwa na magamba kuchanganya siasa na mila.

Pia anadai magamba wamekuwa wakidanganya wananchi kuwa alama nyekundu iliyopo kwenye bendera ya CDM inaonyesha kuwa ni chama cha hatari hivi wasijiunge nacho.

Pia imefika mahali wanatumia viongozi wa jamii ya Kimaasai kuwalaani watakaojiunga na Upinzani. Chanzo mahojiano na Sunrise Radio. Na bado!! Nawasilisha!

KORIANGA ni muda wao kushika hatamu. Wazee wote wakapumzike.
 
Kwa nini hamuuoni huu mkakati?
Kwa nini wote wanaojitoa na kuonyesha kutaka kujiunga na CDM ni wafuasi wa EL?
Hamgundui EL amegundua mkakati wa kuirudisha Arusha chini ya himaya yake?
Baada ya uchaguzi Arumeru mlitaka kujua EL atafanya nini
Haya ndiyo majibu
Wafuasi wake watajiunga CDM watagombea kupitia CDM lakini kama ambavyo hawakuwa wakifanya kazi kwa maslahi ya CCM bali ya EL, vivyo hivyo hawatafanya kwa manufaa ya CDM
Kama nia ya CDM ni ruzuku kuongezeka kutokana na idadi ya Wabunge, wamepata
Kama nia yao ni kupinga ufisadi na ukandamizaji, wameliwa
 
Mbona rangi nyekundu kwa wamasai ndio dili sana? Mmasai hanunui nguo isiyo na rangi nyekundu, Morani wote wanavaa nyekundu Hata himi nina nguo hizo, na Mama yeyo za Bluu. Hivyo CDM inaweza kupata ujiko huku umasaini wakibadilisha misemo hiyo. By the way nimepita leo ktk jimbo la Arumeru Magharibi nikawa naongea na jamaa zangu wanasema huko ni CDM tupu inatawala, nikawaambia nataka kugombea ubunge mwaka 2015 kwa tiketi ya CCM wakanishangaa kuwa sitapata kitu ni afadhali nigombee kwa tiketi ya CDM. nikaona kweli CDM imekamata AR.
 
Huyu dogo amesema kweli, leo nimeona gazeti la jambo leo limeandika Cdm ni chama cha freemason. Wameweka picha za viongozi wa nchi flani flani wanaonyesha alama ya vidole viwili. Pia wamemweka hadi papa benedicto wa 16. Wameandika Dr. Slaa ana jini sebuleni. Ki ukweli leo nimejisikia vibaya kuona zile habari ila kwa sababu najua jambo leo ni gazeti la serikali nikajua ni mkakati wao wa kuidhoofisha Cdm ambapo hata hawawezi. Gazeti la jamba leo ni uchafu kabisa. Huyu dogo wa Longindo ndo atamwondoa Lekule Laizer welcome kijana.

Propaganda za kupakazia wengine magamba hazitawasaidia tena! huenda walifaidika nazo huko nyuma, lakini si katika kizazi hiki!
 
Back
Top Bottom