Katibu Mkuu wa Wizara na Mshauri Mkuu wa Chama Pinzani

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
40,334
72,799
Katika serikali isiyo ya mseto anapatikana Mtendaji mkuu wa wizara (Katibu Mkuu) ambaye pia ni Mshauri mkuu wa Chama cha Upinzani chenye Mbunge Bungeni na Madiwani kadhaa huku kikiongoza Halmashauri moja nchini.
Hayo yametokea Tanzania na Mtu huyo ni Prof Kitila Mkumbo ambaye kachaguliwa kuwa Katibu mkuu wizara ya Maji na Umwagiliaji huku akiwa bado ni mshauri mkuu wa ACT Wazalendo.
Hii imekaaje? Atasimamia sera zipi au ataunganisha nguvu za ACT ndani ya serikali ya CCM?
 
Mradi hakuvunja sheria kila kitu kinawezekana,huku atakula kiapo cha kulinda siri za serikali na huku atashauri chama labda ujiulize wapi atakuwa kiutendaji zaidi lakini ni kama kabla ya hapo alikuwa na majukumu mawili Act na chuo kikuu,kanyaga twende baba mradi mpunga ndani ya kiroba!
 
Ulipaswa kuchangia tu mjadala uliopo humu. si vema kuanzisha mijadala kadhaaa inayohusu jambo moja
Wasaliti lazima wafunuliwe zaidi , na uzalendo wa Magufuli ni lazima utiliwe shaka , juzi alimuondoa Kwenye uteuzi wake mgombea ubunge wa ACT , sasa kwa Kitila Mkumbo imekuwaje ?

Huku kwetu Tandika Mwembeyanga kuna usemi wa kiswahili kwamba , UKIWA MUONGO USIWE MSAHAULIFU .
 
Alisema hataruhusu mpinzani kuwepo kwenye serikali yake, kumbe ni kweli ACT sio wapinzani, ni tawi la CCM.
 
Unafiki tu,huwa serkali makini zinalazmika kufanya hivyo kwa kuzingatia maana ya kuwa unachagua mtu wa kutoka upinzani kuwakalisha kundi kubwa la watu waliopo nyuma yake!!...
 
Katika serikali isiyo ya mseto anapatikana Mtendaji mkuu wa wizara (Katibu Mkuu) ambaye pia ni Mshauri mkuu wa Chama cha Upinzani chenye Mbunge Bungeni na Madiwani kadhaa huku kikiongoza Halmashauri moja nchini.
Hayo yametokea Tanzania na Mtu huyo ni Prof Kitila Mkumbo ambaye kachaguliwa kuwa Katibu mkuu wizara ya Maji na Umwagiliaji huku akiwa bado ni mshauri mkuu wa ACT Wazalendo.
Hii imekaaje? Atasimamia sera zipi au ataunganisha nguvu za ACT ndani ya serikali ya CCM?
ACT ni CCM B imedhihirika,na wamefurahia.
 
Huyu jamaa c ndiye aliyenukuliwa akisema rais aache kuteuwa wahadhiri?
Nategema kusikia akikataa uteuzi wake ili kusimamia alichokisema hapo mwanzo
 
Kuna CCM ananiambia mbona Lissu kapewa urais TLS na Magufuli!!!sijamjibu
Ha ha ha atakuwa Daudi Bashite huyo! hizo akili lazima ziwe zile za kusoma miaka sita degree ya miaka mitatu kisha Seneti inaamua kukupa tuu maana wamekuchoka nawe huondoki
 
Back
Top Bottom