Katibu Mkuu wa CHADEMA, Vincent Mashinji ampongeza Maalim Seif

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dkt Vincent Mashinji amempongeza aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF kwa hatua yake ya kujiunga na Chama cha ACT- Wazalendo na kusema uamuzi wake ni sahihi.

Katibu Mkuu wa CHADEMA Vincent Mashinji ametoa kauli hiyo leo akitoa maoni yake ili kufahamu juu ya maoni yake kama kiongozi wa juu wa chama kikuu cha upinzani nchini.
Mashinji amesema, "nimpongeze kwa uamuzi wake wa kuendelea na shughuli za kisiasa na kupigania mabadiliko kwenye taifa letu, watu wengi walitegemea yeye kupumzika lakini amejipima na ameona anahitaji kuendelea kufanya kazi ni hatua kubwa kwetu sisi wapinzani."
Mapema leo Machi 18, 2019 Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es salaam, ilitangaza kutambua uhalali wa mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa Profesa Ibrahim Lipumba.
Kufuatia maamuzi hayo ya Mahakama majira ya saa nane leo Machi 18, 2019 alitangaza uamuzi wa kuhamia Chama Cha ACT- Wazalendo kwa kile alichokidai amesoma katiba za vyama vingine na kubaini masharti ya chama hicho ni nafuu zaidi.
 
CHADEMA wanajilaumu sana kwnn Seif hajaenda kwao ila kajiunga ACT
 
mkuu bado hujaona dhamira ya upinzani?, lengo ACT wazalendo wawe chama tawala ZNZ na CHADEMA wawe chama kikuu bara

Ni hivi, CHADEMA sbb walikuwa na UKAWA pamoja na Maalim, walifanya mazungumzo ya siri kuwa ikiwa Lipumba atapewa uenyekiti na Mahakama, basi yeye ataenda CHADEMA, ila ghafla paaaaaap Seif katua ACT, yaani CHADEMA chenga kali sanaaa hiyo wamepigwa.. Haaa
 
hayo ni maneno ya ccm kuweka ufa kati ya chadema na cuf, ila ukweli ni kuwa kutakuwa na vyama viwili vyenye nguvu kimoja bara na kingine visiwani, lakini ikiwa chadema ikiwa chama kikuu bara na visiwani ilikuwa ni kazi rahisi ccm kuidhibiti chadema wakithibiti bara wanakuwa wamemaliza hata znz, kwa sheria ya sasa inampa mamlaka msajili kukifuta chama lakini sasa hivi hawezi kuvifuta vyama viwili kwa pamoja, akifuta bara basi wakina mbowe wanaenda znz kumsaidia ACT ichukue dola akiifuta ACT watahamia CHADEMA kuipasapoti
 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dkt Vincent Mashinji amempongeza aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF kwa hatua yake ya kujiunga na Chama cha ACT- Wazalendo na kusema uamuzi wake ni sahihi.

Katibu Mkuu wa CHADEMA Vincent Mashinji ametoa kauli hiyo leo akitoa maoni yake ili kufahamu juu ya maoni yake kama kiongozi wa juu wa chama kikuu cha upinzani nchini.
Mashinji amesema, "nimpongeze kwa uamuzi wake wa kuendelea na shughuli za kisiasa na kupigania mabadiliko kwenye taifa letu, watu wengi walitegemea yeye kupumzika lakini amejipima na ameona anahitaji kuendelea kufanya kazi ni hatua kubwa kwetu sisi wapinzani."
Mapema leo Machi 18, 2019 Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es salaam, ilitangaza kutambua uhalali wa mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa Profesa Ibrahim Lipumba.
Kufuatia maamuzi hayo ya Mahakama majira ya saa nane leo Machi 18, 2019 alitangaza uamuzi wa kuhamia Chama Cha ACT- Wazalendo kwa kile alichokidai amesoma katiba za vyama vingine na kubaini masharti ya chama hicho ni nafuu zaidi.
Hongera sana Chadema kwa kumpongeza Maalim na ACT

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CCM walivyosikia wazee wa CHADEMA wanamkaribisha Seif ajiunge CHADEMA wakapotea maboya kimoja.....siasa ni sayansi nyie endeleeni kutegemea tume na polisi ipo siku mtajua CHADEMA ni nani.
 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dkt Vincent Mashinji amempongeza aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF kwa hatua yake ya kujiunga na Chama cha ACT- Wazalendo na kusema uamuzi wake ni sahihi.

Katibu Mkuu wa CHADEMA Vincent Mashinji ametoa kauli hiyo leo akitoa maoni yake ili kufahamu juu ya maoni yake kama kiongozi wa juu wa chama kikuu cha upinzani nchini.
Mashinji amesema, "nimpongeze kwa uamuzi wake wa kuendelea na shughuli za kisiasa na kupigania mabadiliko kwenye taifa letu, watu wengi walitegemea yeye kupumzika lakini amejipima na ameona anahitaji kuendelea kufanya kazi ni hatua kubwa kwetu sisi wapinzani."
Mapema leo Machi 18, 2019 Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es salaam, ilitangaza kutambua uhalali wa mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa Profesa Ibrahim Lipumba.
Kufuatia maamuzi hayo ya Mahakama majira ya saa nane leo Machi 18, 2019 alitangaza uamuzi wa kuhamia Chama Cha ACT- Wazalendo kwa kile alichokidai amesoma katiba za vyama vingine na kubaini masharti ya chama hicho ni nafuu zaidi.

Huyu katibu kama vile ajielewi hivi sijui huwa anasinzia kwa nini hakuona makosa ya nasari kudoji vikao vya bunge mpaka anafutwa ubunge katibu yupo tu
 
Mkisema CHADEMA wamechukia maalim kwenda ACT mnamaanisha CHADEMA pia ilikuwa inachukia maalim kuwa CUF

Sasa Kama CUF inakufa inazaliwa ACT Kuna tatizo gani?

Hizi karata zimechangwa vizuri sababu jaji Mutungi anaweza kuifuta CHADEMA, ACT ikabaki Ila hawezi kuvifuta vyote viwili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hayo ni maneno ya ccm kuweka ufa kati ya chadema na cuf, ila ukweli ni kuwa kutakuwa na vyama viwili vyenye nguvu kimoja bara na kingine visiwani, lakini ikiwa chadema ikiwa chama kikuu bara na visiwani ilikuwa ni kazi rahisi ccm kuidhibiti chadema wakithibiti bara wanakuwa wamemaliza hata znz, kwa sheria ya sasa inampa mamlaka msajili kukifuta chama lakini sasa hivi hawezi kuvifuta vyama viwili kwa pamoja, akifuta bara basi wakina mbowe wanaenda znz kumsaidia ACT ichukue dola akiifuta ACT watahamia CHADEMA kuipasapoti
Yaani, uko sahihi kabisa hasa ikizingatiwa na hizi siasa za ccm ya kubebwa kwenye mbeleko ya tiss, jwtz, policeccm na NEC ni risk sana kuweka mayai yote kwenye tenga mmoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom