Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika afika kumjulia hali Mama Mzazi wa Alphonse Mawazo

Mgodo Mgodoki

JF-Expert Member
Jul 25, 2014
1,399
1,365
Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika afika Kijijini Chikobe Mkoani Geita akitokea kwenye mazishi ya Magufuli kumjulia hali Mama Mzazi wa Kamanda Alfonse Mawazo,Bi. Heleni Nyegera. Alphonse Mawazo aliuawa Kikatili Wilayani Chatto Mkoani Geita lakini hadi leo hakuna yeyote aliekamatwa.

Katibu Mnyika amemueleza Bi Helen kuwa Chadema inatambua na kuendeleza mchango wa Kamanda Mawazo katika kudai Haki,Katiba Mpya na Tume huru ya Uchaguzi.

FB_IMG_16168644221262371.jpg
 
Acha kuchochea chuki ndugu. Kumbuka kuna Mungu mtoa hukumu ya haki, utajibu nini siku hiyo kuudanganya umma kuwa mpka sasa waliohusika mauaji hawajakamatwa?

Je unafanya, hivi ili umufurahishe nani?

Wauwaji walishakamatwa na hukumu ya kifungo cha maisha ilishatolewa. Je, unataka nini cha zaidi?

Tubu hii dhambi lasivyo utakilaani kizazi chako mwenyewe.
 
Acha kuchochea chuki ndugu...kumbuka kuna Mungu mtoa hukumu ya haki, utajibu nini siku hiyo kuudanganya umma kuwa mpka sasa waliohusika mauaji hawajakamatwa?

Je unafanya, hivi ili umufurahishe nani?

Wauwaji walishakamatwa na hukumu ya kifungo cha maisha ilishatolewa. Je unataka nini cha zaidi.?

Tubu hii dhambi lasivyo utakilaani kizazi chako mwenyewe.
Acha vitisho wewe, hiyo dhambi ya kurithisha kizazi naona unamlenga aliezikwa jana saa10:52 jioni.
 
Alphonse Mawazo aliuawa Kikatili Wilayani Chatto Mkoani Geita lakini hadi leo hakuna yeyote aliekamatwa.
Mkuu,
Achaneni na ulaghai, mwisho wake uwe wiki hii. Fanyeni siasa za uhakika sasa.

Ndiyo, kifo hicho kilisikitisha, na kinaendelea kusikitisha, kama vilivyosikitisha hivi vya wengine na waliopotea wasijulikane wapo wapi hadi sasa.

Tuzike historia hiyo na aliyehusika naye, twende mbele kwa matumaini ya kuwa huru.

Na isije ukanielewa vibaya, na kama sijui kilichotokea kuhusu taarifa za Aliphonce Mawazo, naomba pia uniweke kwenye mstari sahihi.

Hapajawahi kuwepo na kesi ya kundi la watu waliohusika katika tukio hilo? Hiyo kesi iliishia wapi; au ulikuwa ni usanii mtupu?

Sasa basi, unapobandika hapa vitu kama hivi, tafadhali hakikisha unaweka kitu ulicho nacho uhakika. Usitafute tu kuchochea hisia za watu juu ya aliyekwishaondoka maishani mwao.
 
Mnyika ungeonesha na pesa kidogo hata million 5 hivi kumpoza mama kwani naona mama kama kilakitu kimekwama.
 
Haya ni mambo machache ambayo hata kama Magu angekuwa ananipa mkate na siagi kila siku,nisingemkubali. Huwezi kuona binadamu anachinjwa kama kuku halafu ukakaa kimya tu. Angekuwa kachinjwa DC ungekaa kimya?
Mambo kama hili ndiyo yaliyomwondolea heshima na kuharibu kabisa mazuri aliyokuwa akijaribu kuyatenda.

Ajabu ni kwamba kuna watu wanazima akili zao juu ya mambo kama haya, mradi barabara na madaraja yanajengwa!
 
Back
Top Bottom