Katibu Mkuu wa Chadema Akikagua kiwanja kutakapojengwa ofisi ya chama kata ya Usimbe, Tabora

Mkuu anakagua Kiwanja au ujenzi hebu naomba urudie tena
Pa kujenga makao wakuu ya Chadema atakagua lini haoni aibu kukagua viwanja vya ofisi za matawi wakati makao wakuu wanapanga uswahilini.Huyu karibu mkuu kweli hana haya wala mshipa wa aibu.
 
Kuna kila sababu sasa chama kuwa na jengo lake la kisasa kama makao makuu.napendekeza jengo la makao makuu ya chadema lijengwe Dodoma.pia chama kianze kuwa na mkakati wa kujenga ukumbi wake wa mikutano kama wenzao Dodoma..sambamba na hayo chama kihakikishe kila kanda inakuwa na Majengo yake ya kisasa kama ofisi na vitega uchumi ikiwezekana...Ofisi za kanda nazo zipigane kuhakikisha wilaya zao, Kata, na vitongoji zinakuwa na Majengo yao ya ofisi mazuri na ya kisasa...ninaamini inawezekana chama kwasasa kina rasmali fedha na watu kutosha kabisa kuwa na Majengo ya ofisi ya kisasa na vitega uchumi kuanzia ngazi ya shina mpaka taifa.
 
Kata ya Usimba tayari jengo kubwa lilikuwa limejengwa, John Mrema aliwahi kufanya ziara huko 2012 akaahidi mabati.

Inakuwaje leo katibu mkuu anakagua kiwanja kitupu? au kuna ufisadi umefanyika?
 
Lini atakagua ujenzi wa ofisi kuu ya chama, Taifa.
Ni aibu kwa chama kinachopokea ruzuku ya shilingi milioni 200 kila mwezi kupanga kwenye kibanda kama kile cha mtaa wa Ufipa.
Huenda ule ni mradi wa mtu kupiga hela
 
Back
Top Bottom