Katibu Mkuu wa CCM: Bila Nape na Bashe CCM itakufa

Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru amenukuliwa akisema eti wale wabunge wanaoikosoa sana serikali bungeni ndio wanaotakiwa, la sivyo CCM itajifia!

Katibu mkuu huyu inaonekana haendani na Magufuli kwenye mambo mengi, kuanzia kwenye suala la katiba mpya ambayo alinukuliwa akisema hii haifai kwa mfumo wa vyama vingi akihojiwa na Azam Tv

Magufuli na wengine wanataka katiba hii hii inayompa rais madaraka mengi pamoja na nguvu nyingi pia CCM

Lingine ni suala la watendaji wa Serikali kujihusisha na mambo ya chama, katibu huyu alipiga marufuku watu kama wakuu wa wilaya na mikoa kutojihusisha na siasa za vyama

Hili nalo ni kinyume na itikadi za Magufuli ambaye anachanganya sana mambo ya chama na serikali, ikiwemo anateua makada wa vyama katika nafasi mbalimbali na mashirika ya umma , hata wakurugenzi wa Halmashauri, pia shughuli za CCM kuzifanyia Ikulu

Kingine ni hii kusema kuwa eti wabunge kama Nape n Bashe ndio wanaotakiwa CCM, wabunge wanooonekana ni waasi mara nyingi na hata Nape alipokosoa bungeni ishu ya korosho na kusema CCM itashindwa uchaguzi kusini, JPM alitamka na bila kumtaja jina na kusema aondoke....yaani hamtaki kabisa

Pia JPM amekua akionekana kuwatisha wabunge kwa njia indirect mara kadhaa kwa kutamka kila mara kuwa Naangalia Sana Bunge ( kutuma ujumbe wa Be careful, i'm watching you)

Pia kuna kipindi alimtuma prof. Mpango awapelekee ujumbe live bungeni baada yq kusikika wakikosoa mpango wa ujenzi wa Stieglers Gorge

CCM haiwezi kufa kwa kukosekana kwa Nape na Bashe. Kama kweli kayasema haya, Katibu Mkuu awe mwangalifu na kauli kauli zake. Mimi nilivyomwelewa aliimanisha hawa vijana ni muhimu kwa "checks and balance" kwa jinsi wanavyotoa hoja zao za kuwachangamsha mawaziri bila uwoga
 
Mtu yeyote anayeelewa maana ya siasa hawezi kuendana na Jiwe. Jiwe hakidhi kigezo chochote cha kuwa mwanasiasa wala kuwa kiongozi bora.
 
Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru amenukuliwa akisema eti wale wabunge wanaoikosoa sana serikali bungeni ndio wanaotakiwa, la sivyo CCM itajifia!

Katibu mkuu huyu inaonekana haendani na Magufuli kwenye mambo mengi, kuanzia kwenye suala la katiba mpya ambayo alinukuliwa akisema hii haifai kwa mfumo wa vyama vingi akihojiwa na Azam Tv

Magufuli na wengine wanataka katiba hii hii inayompa rais madaraka mengi pamoja na nguvu nyingi pia CCM

Lingine ni suala la watendaji wa Serikali kujihusisha na mambo ya chama, katibu huyu alipiga marufuku watu kama wakuu wa wilaya na mikoa kutojihusisha na siasa za vyama

Hili nalo ni kinyume na itikadi za Magufuli ambaye anachanganya sana mambo ya chama na serikali, ikiwemo anateua makada wa vyama katika nafasi mbalimbali na mashirika ya umma , hata wakurugenzi wa Halmashauri, pia shughuli za CCM kuzifanyia Ikulu

Kingine ni hii kusema kuwa eti wabunge kama Nape n Bashe ndio wanaotakiwa CCM, wabunge wanooonekana ni waasi mara nyingi na hata Nape alipokosoa bungeni ishu ya korosho na kusema CCM itashindwa uchaguzi kusini, JPM alitamka na bila kumtaja jina na kusema aondoke....yaani hamtaki kabisa

Pia JPM amekua akionekana kuwatisha wabunge kwa njia indirect mara kadhaa kwa kutamka kila mara kuwa Naangalia Sana Bunge ( kutuma ujumbe wa Be careful, i'm watching you)

Pia kuna kipindi alimtuma prof. Mpango awapelekee ujumbe live bungeni baada yq kusikika wakikosoa mpango wa ujenzi wa Stieglers Gorge

Ilishajifia siku nyingi, inaishi kwa oxygen machine( mtutu wa bunduki).
 
Mtu yeyote anayeelewa maana ya siasa hawezi kuendana na Jiwe. Jiwe hakidhi kigezo chochote cha kuwa mwanasiasa wala kuwa kiongozi bora.
Kwa hiyo unamanisha Jiwe ni kama.kapi tu.
 
CCM imezaliwa 1977, Nape na Bashe labda walikuwa wanatambaa wakati huo. Ni makosa makubwa kudhani kuwa chama kikongwe kinaweza kufa kwa sababu tu ya wabunge wawili.
 
CCM Lowasa aliamini bila yeye na Kingunge CCM inakufa Sababu waliamini kuwa wao ndio wenye hisa nyingi CCM kilichowakuta hawasau milele Na CCM iko pale pale.

Sisiem imekufa siku nyingi sana! Kinachofanyika saa ivi ni mabavu!
 
CCM imezaliwa 1977, Nape na Bashe labda walikuwa wanatambaa wakati huo. Ni makosa makubwa kudhani kuwa chama kikongwe kinaweza kufa kwa sababu tu ya wabunge wawili.

Chama kimekufa siku nyingi sana, unachokiona na unaowaona ni waigizaji tu wanaotumia mabavu na uonevu kwa wasiokuwa na hatia
 
Wanaishangaa Demokrasia ilivyoshamiri ndani CCM walikuwa wanafikiri ni chama cha kufukuzana kama walivyomtimua Zitto.
Kumbe Twaweza wako sahihi. Kwani Zitto alifukuzwa au alijifukuza?! Katiba ya Chadema inasemaje mwanachama anapopeleka shauri mahakamani dhidi ya Chama na akashindwa kesi?!
 
Chama kimekufa siku nyingi sana, unachokiona na unaowaona ni waigizaji tu wanaotumia mabavu na uonevu kwa wasiokuwa na hatia
Kalagabaho. Utaishi mpaka siku yako ya mwisho duniani, na pengine utakiacha hiki chama. Fanya kazi, matatizo yako sio ya kila mtu.
 
Nyie hamjaelewa mbinu ya ccm..
Hawa jamaa wanabembelezwa kwa mda huu mfupi wa kampeni watatumiwa na hapo baadae watatupwa ile mbaya na kama hamuamini mimi bado nipo mtakuja kuamini ninachosema.
Nimesikia eti wataenda kufanya kampeni huko kigoma maana wanaushawishi baada ya hapo mtaona kitakachotokea.
Baba anaangalia TV watoto wanaleta ugali mezani kwa viboko(nidhamu feki) au kwa kupenda( nidhamu halisi).Kama hawakuhama CCM unategemea nini?
 
Kauli ya Mwalimu Bashir Ally (Katibu Mkuu wa CCM Taifa) naiona kwa namna mbili:
1. Kwamba zama hizi wabunge wa CCM wanao uhuru wa kukosoa serikali (kutoa maoni mbadala) nje ya mfumo wa circus ya chama tofauti na ilivyokuwa enzi za akina Rostam Azizi (kujivua gamba) na hivyo kuwataka wananchi wasiwe na wasiwasi wa kumchagua mbunge wanayehisi kwamba anao uwezi wa kuikosoa serikali au;
2. Kuwafanya Bashe na Nape waendelee kujiropokea ili CCM ipate kisingizio cha kuwaondoa kwenye chama.
sijui!
 
Kalagabaho. Utaishi mpaka siku yako ya mwisho duniani, na pengine utakiacha hiki chama. Fanya kazi, matatizo yako sio ya kila mtu.

Nyamaza we chakula!! Najua jinsi unavyoishi kwa mgongo wa chama na umefanya ndo pumzi yako!! Mimi ni mtu huru na sina chama chochote nilichokuwa attached nacho kama wewe!! Na kazi zangu, nitafanya tena bila influence yoyote ya vyama vya siasa. Ukisikia ccm inakufa unabanwa na mharo maana unajua ndo mwisho wa maisha. Come on, live a free life mum!
 
Hahahaha pole sana mkuu. Naona unaitumia jamii forum kama sehemu ya kupunguzia hasira zako za maisha.
 
Kumbe Twaweza wako sahihi. Kwani Zitto alifukuzwa au alijifukuza?! Katiba ya Chadema inasemaje mwanachama anapopeleka shauri mahakamani dhidi ya Chama na akashindwa kesi?!
Nimeamini ndio maana Chadema hawawezi kuandika Zinjanthropus.
 
anawapaka mafuta kwa mgongo wa chupa 2020 asubuhi tu watakuwa washakatwa
 
Back
Top Bottom