Katibu Mkuu wa CCM: Bila Nape na Bashe CCM itakufa

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2016
Posts
2,194
Reaction score
4,805
Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru amenukuliwa akisema eti wale wabunge wanaoikosoa sana serikali bungeni ndio wanaotakiwa, la sivyo CCM itajifia!

Katibu mkuu huyu inaonekana haendani na Magufuli kwenye mambo mengi, kuanzia kwenye suala la katiba mpya ambayo alinukuliwa akisema hii haifai kwa mfumo wa vyama vingi akihojiwa na Azam Tv

Magufuli na wengine wanataka katiba hii hii inayompa rais madaraka mengi pamoja na nguvu nyingi pia CCM

Lingine ni suala la watendaji wa Serikali kujihusisha na mambo ya chama, katibu huyu alipiga marufuku watu kama wakuu wa wilaya na mikoa kutojihusisha na siasa za vyama

Hili nalo ni kinyume na itikadi za Magufuli ambaye anachanganya sana mambo ya chama na serikali, ikiwemo anateua makada wa vyama katika nafasi mbalimbali na mashirika ya umma , hata wakurugenzi wa Halmashauri, pia shughuli za CCM kuzifanyia Ikulu

Kingine ni hii kusema kuwa eti wabunge kama Nape n Bashe ndio wanaotakiwa CCM, wabunge wanooonekana ni waasi mara nyingi na hata Nape alipokosoa bungeni ishu ya korosho na kusema CCM itashindwa uchaguzi kusini, JPM alitamka na bila kumtaja jina na kusema aondoke....yaani hamtaki kabisa

Pia JPM amekua akionekana kuwatisha wabunge kwa njia indirect mara kadhaa kwa kutamka kila mara kuwa Naangalia Sana Bunge ( kutuma ujumbe wa Be careful, i'm watching you)

Pia kuna kipindi alimtuma prof. Mpango awapelekee ujumbe live bungeni baada yq kusikika wakikosoa mpango wa ujenzi wa Stieglers Gorge
 
mmhh.. Labda hawajamuelewa, soon atasahihisha kauli yake hio yenye ukakasi!
 
Last edited:
Nilipata kwenda kijijini siku moja nikaingia kwenye klabu ya pombe za kienyezi Boha, yaani ile inayotengenezwa kwa miwa. ( wakuu Elli na zumbemkuu wanaielewa vyema) Basi mle ndani baada ya masaa kadha kila mtu anaongea lake. Sio mnywaji wala muuzaji au yule uliyeongozana naye. Yaani mambo ni vululu vululu.

Hiyo ndiyo hali halisi ya CCM ya sasa, kila mtu kivyake. Papaa Mukulu anazoza vyake, Mr Chakubanga naye ana singo zake zenye mapigo tofauti sasa kaingia Dr Kigeugeu naye anachapa lapa ajuavyo.

Hao vijana kina Nape na Bashe wanacheki tuu, kisha wanacheka hiiiiiiiiii!
 
Wanaishangaa Demokrasia ilivyoshamiri ndani CCM walikuwa wanafikiri ni chama cha kufukuzana kama walivyomtimua Zitto.
 
Last edited:
CCM Lowasa aliamini bila yeye na Kingunge CCM inakufa Sababu waliamini kuwa wao ndio wenye hisa nyingi CCM kilichowakuta hawasau milele Na CCM iko pale pale.
 
Nape na bashe kutumika kweny kampen buyungu....
 
Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru amenukuliwa akisema eti wale wabunge wanaoikosoa sana serikali bungeni ndio wanaotakiwa, la sivyo CCM itajifia!

Katibu mkuu huyu inaonekana haendani na Magufuli kwenye mambo mengi, kuanzia kwenye suala la katiba mpya ambayo alinukuliwa akisema hii haifai kwa mfumo wa vyama vingi akihojiwa na Azam Tv

Magufuli na wengine wanataka katiba hii hii inayompa rais madaraka mengi pamoja na nguvu nyingi pia CCM

Lingine ni suala la watendaji wa Serikali kujihusisha na mambo ya chama, katibu huyu alipiga marufuku watu kama wakuu wa wilaya na mikoa kutojihusisha na siasa za vyama

Hili nalo ni kinyume na itikadi za Magufuli ambaye anachanganya sana mambo ya chama na serikali, ikiwemo anateua makada wa vyama katika nafasi mbalimbali na mashirika ya umma , hata wakurugenzi wa Halmashauri, pia shughuli za CCM kuzifanyia Ikulu

Kingine ni hii kusema kuwa eti wabunge kama Nape n Bashe ndio wanaotakiwa CCM, wabunge wanooonekana ni waasi mara nyingi na hata Nape alipokosoa bungeni ishu ya korosho na kusema CCM itashindwa uchaguzi kusini, JPM alitamka na bila kumtaja jina na kusema aondoke....yaani hamtaki kabisa

Pia JPM amekua akionekana kuwatisha wabunge kwa njia indirect mara kadhaa kwa kutamka kila mara kuwa Naangalia Sana Bunge ( kutuma ujumbe wa Be careful, i'm watching you)

Pia kuna kipindi alimtuma prof. Mpango awapelekee ujumbe live bungeni baada yq kusikika wakikosoa mpango wa ujenzi wa Stieglers Gorge
Nyie hamjaelewa mbinu ya ccm..
Hawa jamaa wanabembelezwa kwa mda huu mfupi wa kampeni watatumiwa na hapo baadae watatupwa ile mbaya na kama hamuamini mimi bado nipo mtakuja kuamini ninachosema.
Nimesikia eti wataenda kufanya kampeni huko kigoma maana wanaushawishi baada ya hapo mtaona kitakachotokea.
 
Mleta mada badilisha kichwa cha habari, ulichokiweka hakina ukweli hata chembe. KM hakusema hivyo amesema Bashe NA Nape sio wajeuri bali wadadisi.
Hao wanavutwa tuu muda mfupi huu wa vikampeni hivi vikiisha bado hatma yao iko pale pale
Naomba niwakumbushe kuwa huyo katibu wao alishasema 2020 wale wabunge wote wakongwe wasahau kurudi majimboni mwao maana wanakatwa wote
 
Back
Top Bottom