Katibu Mkuu wa CCM ana mamlaka ya kumfukuza kazi Mwenyekiti NEC na Waziri?

Invigilator

JF-Expert Member
Aug 16, 2016
3,207
5,990
Leo nimefuatilia mkutano wa Chama Cha Mapinduzi - CCM ulioongozwa na katibu mkuu wa chama Dk Bashiru wakati akizungumza na wajumbe wa chama hicho mkoa wa Magharibi mjini,Unguja,Zanzibar na kumsikia akitamka maneno yafuatayo;

"... nilitaka nijue,maana mimi nisingekwenda.Nilimpigia jaji Mtungi (simu) nikamwambia,ukienda huna kazi.Nikampigia pia waziri Jafo nikamwambia ukienda huna kazi."

Napenda kujua kwa mujibu wa katiba na sheria zetu za nchi,je katibu wa chama ana mamlaka ya kufanya hayo?..
 
CCM wanajiita chama dola,chama kinachoongoza serikali,chama kinachoisimamia serikali sasa sijajua Mamlaka ya kuisimamia hiyo serikali yanaanzia wapi na kuishia wapi na kwa mujibu wa katiba ipi yaan ya chama chao or katiba ya Nchi yetu tukufu.


Mwenyekiti wa CCM ndie boss wa chama na bahati nzuri ndie rais pia anaeunda serikali,sasa labda katibu mkuu wa CCM ajaribu kuwachomea utambi hao kina Jafo ili wafukuzwe kazi na boss wake ila si yeye aamke from no where aseme Jafo kazi basi.

Yaani ni kama sisi wanawake tunavyojaribu kuchombeza kwa waume zetu kuwa mtoto fulani simtaki sababu haniheshimu na kwa nguvu ya papuchi mume anamfukuza mtoto huyo ni hivyo tu najaribu kutaka kukuelewesha
 
Wazee wa Ombwe la Uongozi tunacheeeekaa

Kuna watu waliamini hata Jk angetaka kuwa Dikteta asingeweza kwa kuwa sie tayari ni Democratic Nation, nilikuwa nawakosoa sana wakawa hawaelewi

Sasa hivi Habari kama hizi nikifika kijiweni jion nazisoma kwa mbwembwe kweli kila mtu asikie
 
Ndio maana siku hizi naona hadi trafiki wanaogopa kisimamisha gari la mtu aliyeweka nembo au kutandaza bendera ya CCM juu ya dashboard, hata kama halina mlango au taa ataacha lipite tu, dizaini anaona kama amemsimamisha Raisi
 
Invigilator,

Full Kujimwambafai
1574951513329.png
 
CCM CCM CCM Mungu anawaona.japo Rais anachapa kazi bila kufuata sheria za Nchi kama kununua Ndege,Sgr,Chato airport,Elimu bure nk nk bila bajeti ya Bunge hii Jeuri namna hii mnaitoa wapi?Nchi yetu sote






Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Chakwale
Mungu Ibariki Gairo
 
CCM CCM CCM Mungu anawaona.japo Rais anachapa kazi bila kufuata sheria za Nchi kama kununua Ndege,Sgr,Chato airport,Elimu bure nk nk bila bajeti ya Bunge hii Jeuri namna hii mnaitoa wapi?Nchi yetu sote






Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Chakwale
Mungu Ibariki Gairo
Yaani Mkuu hawa jamaa wanachokifanya hata wao naimani inafikia kipindi wanakiri wanaipeleka nchi shimoni.
 
Back
Top Bottom