barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,874
Baadhi ya makada wa CCM walioshindwa kwenye mbio za urais na ubunge kuteuliwa kushika nafasi za Katibu Tawala wa Wilaya (DAS), wamezua mjadala kwa kile kilichoelezwa kuwa nafasi hizo ni za kiutendaji hivyo zinahitaji wasomi na wenye uzoefu serikalini.
Makada hao ni miongoni mwa watu 40 wapya kati ya 134 waliotangazwa juzi na Ofisi ya Rais-Utumishi kushika nafasi hizo kwenye uongozi wa wilaya.
Miongoni mwa makada waliotangazwa kuteuliwa kuwa Ma-DAS ni Amos Siyamtemi, ambaye aligombea urais kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita, lakini akaishia ndani ya mchakato wa CCM, Kasilda Mgeni, mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Star TV ambaye alikuwa kiongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM na aligombea ubunge wa viti maalumu mwaka 2010 bila ya mafanikio.
Wengine ni Mtella Mwampambwa, Aboubakar Assenga, Jasinta Mboneko, Gift Msuya, Hashim Mkomba, Edward Mpogolo na Adam Mzee, ambao wamewahi kugombea ubunge, udiwani au kushika nafasi kwenye ngazi tofauti za uongozi wa CCM.
Akiongea na gazeti la Mwananchi Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dr Benson Bana amesema ingekuwa vema nafasi hizo zingetangazwa,sababu zinahusu nafasi nyeti ya utumishi wa umma,sababu nafasi hizo zinahitaji watumishi walio wazoefu na wa muda mrefu katika kada ya utumishi wa umma
Katibu Mkuu Utumishi Dr Laurian Ndumbaro amekiri kuwa wengi wa wateuliwa hawana uzoefu wa kazi za serikali na hivyo wanahitaji mafunzo ya muda mfupi ili kuendana na kazi wanazotakiwa kuzifanya
Chanzo: Mwananchi