Katibu Mkuu Utumishi atembelea mradi wa SGR, watumishi zaidi ya 1000 kuajiriwa

Tanzania Railways Corp

JF-Expert Member
Mar 23, 2018
251
595
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Utumishi Dkt. Laurean Ndumbaro pamoja na Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wametembelea mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa - SGR kipande cha Morogoro – Makutupora Septemba 04, 2021.

Lengo la ziara hiyo ni kuona maendeleo ya mradi huo ambao umefika asilimia 70 ambapo pamoja na mambo mengine Katibu Mkuu na Watumishi wa Ofisi ya Rais, Utumishi waliweza kupata taarifa ya maendeleo ya mradi wa SGR Dar es Salaam – Morogoro ambao umefika asilimia 93.

Dkt. Ndumbaro amesema kuwa “Inafurahisha kwa hatua hii iliyofikiwa, kwa kuwa hizi reli (ya zamani na SGR) zinakwenda kwa pamoja kuna changamoto ya kupata watumishi katika reli hii ya mwendokasi”, pia ametoa maelekezo kwa uongozi wa Shirika la Reli Tanzania - TRC kuonana na Ofisi ya Rais Utumishi ili kuona namna bora ya kuajiri watumishi watakaokwenda kufanya kazi katika mradi huo pindi utakapokamilika.

Katibu Mkuu aliongeza kuwa “watumishi nilioambatana nao ni wawakilishi wa watumishi wengine katika kuona miradi hii ya kimkakati ili wawe mabalozi wazuri kueleza jinsi miradi inavyofanyika kwa kasi ile ile, naamini miradi hii itakapokamilika itaweza kuleta matunda makubwa”

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Bi. Amina Lumuli amesema kuwa maandalizi ya kupata wataalamu watakaoendesha mradi wa SGR yameshafanyika ikiwemo mafunzo ya ndani na kuandaa mahitaji ikiwemo vifaa na wataalmu wanaohitaji, na kinachosubiriwa ni hatua nyingine ikiwemo kupata vibali vya ajira.

“Maandalizi tulishafanya kuangalia idadi ya wafanyakazi na vifaa vinavyohitajika ili kuendesha mradi huo, kilichobaki ni kuwasiliana na vyombo husika kama hivi leo tuko na Utumishi ili kupata taratibu za kufuata ili kuweza kuajiri watumishi” amesema Kaimu Mkurugenzi

Bi. Amina aliongeza kuwa suala la mafunzo Shirika limejipanga kumtafuta mshauri mwelekezi ambaye atakuwa anasimamia mafunzo wakati wa shughuli za uendeshaji wa mradi huo pindi utakapoanza lakini pia Wakandarasi Yapi Merkezi wataendelea kuwepo kushirikiana katika kipindi cha awali cha uendeshaji wa mradi huu
Bi. Amina amebainisha kuwa fursa za ajira zipo na itakapofika hatua ya kutangaza ajira watahitajika wahandishi, madereva, mafundi, wataalamu wa umeme na mawasiliano pia ameeleza kuwa kwa kipande cha kwanza Dar es Salaam – Morogoro tathimini inaonesha kuwa watahitajika wafanyakazi 1046 ambapo wengine wapo na wengine wataajiriwa.

Cosmas Ngangaji, Mkurugenzi wa Idara ya Mipango Ofisi ya Rais Utumishi amesema kuwa “Mradi huu umejikita katika kuhakikisha nchi inakwenda katika dira ya maendeleo ya 2025 ambayo pamoja na maeneo mengine imelenga suala la maisha bora kwa kufungua fursa za kiuchumi ili nchi yetu iwe shindani”

Watumishi wengine walioambatana na Katibu Mkuu wametoa maoni yao na kueleza kuwa wamefurahishwa na wamepata matumaini na Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutekeleza miradi ya kimkakati itakayoleta manufaa kwa watanzania.


KM Utumishi Visit 04.08.2021.jpg
 
Ivi zile ajira/vibarua walizotangaza Yapi Merkez washaanza kuita watu?
 
Back
Top Bottom