Katibu Mkuu UN kuitembelea Tanzania. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katibu Mkuu UN kuitembelea Tanzania.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwawado, Feb 23, 2009.

 1. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #1
  Feb 23, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) anatarajia kufanya Ziara ya kikazi Nchini Tanzania kuanzia wiki ijayo,Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkazi wa UN -Tanzania Bw. Fernandez Taranco inaonyesha kuwa Katibu Mkuu,Mr Moon atafanya Ziara katika Nchi za Congo-DRC,Rwanda,Afrika kusini na kumalizia Misri.

  Katika siku za karibuni Tanzania imekuwa inapata wageni Wakubwa wa kitaifa,kwa kipindi kisichopungua mwezi mmoja tumekuwa na ugeni wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola (Mr.Kamlash Sharma),Rais wa Jamuhuri ya Uchina (Hu Jintao) na majuzi tu Rais wa Uturuki (Abdalah Gul).Nini kinaashiria kuwepo kwa ugeni huu mkubwa mara kwa mara?
   
 2. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #2
  Feb 23, 2009
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,758
  Trophy Points: 280
  This is just international politics which brings no food on our table. Its just countries making aliances and amends.

  Ukweli ni kwamba watanzania sasa tunakosa kushughulikia mambo ya muhimu..tuna divert attention kwa akina Ki-Moon et al. These folks have nothing to do with our problems. Whether they come or they dont..it doesnt matter. Mmoja juzi katoka katuachia $$20M!

  Bado leo asubihi nilikuwa nasikia vyombo vya habari wakiongelea hizi ziara "kuwa inaonyesha viongozi wetu ni wachapa kazi" nimetamani kuivunja radia yangu! Anyway..viongozi wetu ni reflection yetu wenyewe.

  Ki-Moon aende Congo na Somalia wanamuhitaji zaidi kuliko sisi.
   
 3. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #3
  Feb 23, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Mwawado na Masanja,

  Ukiwa mtu mwema utapata marafiki wengi..wakubwa na wadogo watakutembelea!

  Pia ukiwa na confilicts kama DRC na Somalia unaweza kupata wageni kukusaidia kurekebisha mambo! UN wana 20,000 Peace Keepers DRC!

  Hii ni nzuri kwa nchi yetu..pamoja na matatizo tulikuwa nayo..waje tu!

  Pia JK na role yake AU inaweza ikawa imeipandisha pia chart Tz!

  Halafu mnajua JK alisafiri sana hapa siku za nyuma..naona wengine wanareciprocate!


  Masanja hivi mtu akipenda kuja kukusalimia nyumbani kwako..je utamwambia asije?
   
 4. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #4
  Feb 24, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Ziara ya Bush ilisaidia kidogo maana ilikuja na kitita cha hela, sijui kama ziara za maraisi wengine ni ishara ya nini na sijui zina maana gani kiuchumi. INawezekana ndio huko kutembeleana na kusalimiana. Inawezekana hazitumiki ipasavyo kuleta maendeleao ya kiuchumi na inawezekana zinatumika vizuri, lakini bado haionekani ni vipi. Hata Ban Ki Moon akija sijui kama itasaidi kitu au itabadilisha kitu chochote!!
   
 5. J

  JokaKuu Platinum Member

  #5
  Feb 24, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,729
  Likes Received: 4,948
  Trophy Points: 280
  Bongolander,Masanja,Mwawado,

  ..mapokezi ya ugeni mzito kama huo yana gharama sana kwa nchi masikini kama Tanzania.

  ..nadhani PM Pinda, kama alivyofanya katika gharama za semina na mashangingi, anapaswa kulitupia macho suala la gharama kubwa za safari za ndani na nje za maofisa wa serikali, pamoja na mapokezi ya viongozi wa nje.
   
 6. H

  Hauxtable JF-Expert Member

  #6
  Feb 24, 2009
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 386
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35


  ....nothing the matter Mkuu...ni ule msimu tu,si unajua ile exodus ya 'the big five' kule kwenye mbuga zetu,watu wanakuja kupumzika tu.
   
 7. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #7
  Feb 25, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Serikali imebaini kuwapo mpango mchafu wa kutaka kuvuruga ziara ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki-moon nchini, imeelezwa.Akizungumza jana Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, alisema kuna kundi la watu wanaojiita 'Wazee wa Pemba' linapanga siku hiyo kuingilia ratiba ya mgeni huyo na kufanya maandamano.

  Katibu Mkuu wa UN anatarajia kufanya ziara kuanzia kesho hadi Jumamosi, kutokana na mwaliko aliopewa na Rais Jakaya Kikwete walipokutana New York, Marekani, Septemba mwaka jana.

  Waziri alisema baada ya Serikali kulibaini hilo, hivi sasa inalifanyia kazi ikiwa ni pamoja na lile la wapinzani wa Ba Ki-moon kutoka nje ya nchi, wanaopanga kutumia baadhi ya vyombo vya habari kuandika habari mbaya kumhusu."Ombi letu ni kuhakikisha watu hao hawafanikiwi katika azma yao ya kutumia vyombo vya habari vya hapa nchini kuandika mambo mabaya ya kumchafulia jina mgeni wetu," alisema Waziri Membe.

  Waziri alisema ziara ya Ban Ki-moon ina lengo kuu moja, la kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na UN. Katibu Mkuu akiwa nchini mbali ya kufanya mazungumzo na Raia Kikwete, pia atatembelea miradi inayosimamiwa na mashirika mbalimbali ya UN na mradi wa majaribio wa ONE UN.

  Pia atakwenda Zanzibar keshokutwa na kufanya mazungumzo na Rais Amani Abeid Karume na kuzindua jengo la UN Zanzibar, kisha atakwenda Arusha kutembelea Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR). Katibu Mkuu huyo aliipa heshima kubwa Tanzania ya kumteua Mtanzania kushika nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa UN, Dk Asha-Rose Migiro, ambaye ni mwanamke wa kwanza duniani kushika wadhifa huo.

  Waziri Membe alisema Ki-moon ni rafiki mkubwa wa Tanzania na Afrika, kwani hata kabla ya kuwa na nafasi aliyo nayo sasa, akiwa waziri wa mambo ya nje wa Korea Kusini, aliishawishi serikali yake kuipa Tanzania misaada. Miongoni mwa misaada hiyo ni kujenga daraja la Malagarasi, Kigoma, ujenzi wa vyuo vya ufundi, ujenzi wa hospitali ya kufundishia chuo kikuu Muhimbili na mingine mingi.

  Alitoa mwito kwa wananchi kumpokea kwa wingi na kwa heshima kubwa. Mei 12 mwaka jana wazee 12 walikamatwa na Polisi Zanzibar kwa tuhuma za kudai Pemba ijitenge na Zanzibar, kwa madai kuwa ilikuwa imesahaulika kwa maendeleo. Kwa mujibu wa ofisa usalama wa Chama cha Wananchi (CUF), aliyetajwa kwa jina la Said Miraji, wazee hao walikamatwa usiku.

  Wazee hao wiki moja kabla walikuwa wamewasilisha madai yao kwa Ofisa Mwandamizi wa UN, Dar es Salaam, Oscar Fernandez-Taranco, wakimtaka awasilishe madai yao hayo kwa Ki-moon.Baada ya kukamatwa kwa wazee hao, CUF ilisema ilikuwa imewaagiza wabunge wake kutunza familia za wazee hao, huku chama hicho kikishughulikia hatima yao.

  Miraji alithibitisha kuwa waliokamatwa walikuwa wafuasi wa CUF. Mwezi mmoja kabla ya kukamatwa kwao, wazee hao walikuwa wamemtaka aliyekuwa Balozi wa Marekani nchini, Mark Green, kuwasilisha ujumbe wao kwa Rais George Bush, ili awasaidie kujitenga na Muungano wa Zanzibar na Bara.
  Source: gazeti la Habari Leo
   
Loading...