Katika hali isiyokuwa ya kawaida, katibu mkuu wa TFF amemjia juu Jerry Muro mkuu wa kitengo cha habari cha Yanga kuwa ni mbumbumbu na mtu asiyejua mambo ndio maana yeye peke yake kati ya viongozi wa Yanga ndio anaendelea kupiga kelele kuhusiana na mechi za Yanga.
Hii si kawaida kwa Mwesigwa ambaye ana haiba ya upole, uungwana na huzungumza kwa tahadhari kubwa kila mara. Lakini leo wakati akizungumza na kituo cha Clouds FM kuhusu haki za matangazo ya television za mechi za Yanga ktk kombe la Shirikisho, amejibu lawama za Jerry Muro na kumwita mbumbumbu, kwa kuwa hawakuhudhuria semina za CAF na haonekani kujua vitu vingi.