Katibu Mkuu TFF Mwesigwa amkaripia Jerry Muro na kumpa jina baya

Jeri muro ni mbishi, mbumbumbu na mwenye majivuno. Kwenye mpira kiongozi wa club huwezi kubishia maamuzi na kanuni za wazi za CAFU na FIFA. Hii yaonyesha viongozi wa vilabu vya soka tulio nao. Anajivunia masters hajui watu wanaongelea PhD na post doc though waweza kuwa na hivi vyote bado mtu mwenye diploma akawa na weredi na uelewa zaidi.

Ukiona mtu katika jamii anasema wazi wazi viwango vya elimu yake kwamba sijui ana Masters, PhD sijui na digrii aina yoyote ile ujue lipo tatizo kubwa...YANGA ina bahati mbaya mno...kiongozi yeyote yule katika jamii iwe ni katika soka au sekta yoyote ile ni lazima awe makini katika mambo mbalimbali ikiwemo namna ya kuonekana na pia kuongea katika jamii...sasa tatizo lililopo katika soka yetu ni kuwa watu wanapenda mipasho...na usishangae kuwa hayo aliyoongea huyo msemaji wa YANGA wako wengi waliompongeza...Soka ya Tanzania ina matatizo makubwa...
 
Mwesiga umemchokoza Muro,je unaiweza vita ya maneno? Msije baadae kusuhishwa na wadau wa soka au wizara. Ungempotezea tu
 
Mmmmmmmh, je, ni kweli JERRY MURO amesema YANGA ni kubwa kuliko CAF?????????? jamani, siamini hivyo....
Kasema mkuu nimemsikia mwenyewe ithink alikua amepaniki maana yule jamaa ni dakika sufuri. Sikiliza michezo saa tatu hope wata mquote
 
Umemwona abiria wa Ubungo-Posta anayeenda Mwembechai akasafiri kwanza hadi Posta ndio arudi Mwembechai?

Mfano wako hau-apply hapa. Mwesiga alitoa hoja kwanza kisha akaenda mbali zaidi. Ni kama mtu anayetoka Ubungo - Mwembechai kuamua kufika usalama pia kusalimia jamaa baada ya kumaliza shughuli zilizompeleka mwembechai
 
Sawa iwe hivyo. Yaani mtu akiulizwa jawabu ya hesabu ya tano mara nane akajibu sawasawa kuwa ni arobaini na akaendelea kwamba tano hiyohiyo mara kumi ni hamsini, utamuhesabuje?
 
Jeri muro ni mbishi, mbumbumbu na mwenye majivuno. Kwenye mpira kiongozi wa club huwezi kubishia maamuzi na kanuni za wazi za CAFU na FIFA. Hii yaonyesha viongozi wa vilabu vya soka tulio nao. Anajivunia masters hajui watu wanaongelea PhD na post doc though waweza kuwa na hivi vyote bado mtu mwenye diploma akawa na weredi na uelewa zaidi.
Hizo PHD zimesaidia nini Taifa...masikini wa kutupwaaa
 
Mmmmmmmh, je, ni kweli JERRY MURO amesema YANGA ni kubwa kuliko CAF?????????? jamani, siamini hivyo....
Vitu vingine ni rahisi sana kusema, ila tujiulize wameshalipa pesa ya kutumia uwanja? Ile 5% ya mapato ya uwanjani kupelekwa CAF wataikokotoa namna gani? Maamuzi mengine yanatia mashaka sana na hapa inatupa fursa ya kupima weledi wa Muro kuwa Msamaji wa Yanga.
Utamsikia oohhh mimi nimesoma vyuo vya nje sijasomea vyuo vya Manzese, wakati vyeti vyenyewe ni vya online, unaanza kusoma leo kesho unamaliza. Halafu kesho utawasikia hawana pesa za kusafirishia timu na kuanza kutembeza bakuli.
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, katibu mkuu wa TFF amemjia juu Jerry Muro mkuu wa kitengo cha habari cha Yanga kuwa ni mbumbumbu na mtu asiyejua mambo ndio maana yeye peke yake kati ya viongozi wa Yanga ndio anaendelea kupiga kelele kuhusiana na mechi za Yanga.

Hii si kawaida kwa Mwesigwa ambaye ana haiba ya upole, uungwana na huzungumza kwa tahadhari kubwa kila mara. Lakini leo wakati akizungumza na kituo cha Clouds FM kuhusu haki za matangazo ya television za mechi za Yanga ktk kombe la Shirikisho, amejibu lawama za Jerry Muro na kumwita mbumbumbu, kwa kuwa hawakuhudhuria semina za CAF na haonekani kujua vitu vingi.
kupe lazima alalamike hajapata damu ya yanga
 
Back
Top Bottom