Katibu Mkuu TFF Mwesigwa amkaripia Jerry Muro na kumpa jina baya

Baba Kiki

JF-Expert Member
May 31, 2012
1,544
940
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, katibu mkuu wa TFF amemjia juu Jerry Muro mkuu wa kitengo cha habari cha Yanga kuwa ni mbumbumbu na mtu asiyejua mambo ndio maana yeye peke yake kati ya viongozi wa Yanga ndio anaendelea kupiga kelele kuhusiana na mechi za Yanga.

Hii si kawaida kwa Mwesigwa ambaye ana haiba ya upole, uungwana na huzungumza kwa tahadhari kubwa kila mara. Lakini leo wakati akizungumza na kituo cha Clouds FM kuhusu haki za matangazo ya television za mechi za Yanga ktk kombe la Shirikisho, amejibu lawama za Jerry Muro na kumwita mbumbumbu, kwa kuwa hawakuhudhuria semina za CAF na haonekani kujua vitu vingi.
 
Mwesigwa alichokifanya ni kumjibu Jerry Muro. Alitakiwa ajibu hoja za Jerry Muro.
 
Huyu jamaa nilimwona wa maana sana enzi zile akiwa ITV. Lakini nilivyomsikiliza leo Clouds kiukweli jamaa ni boya kabisa, anapayuka hovyo, haeshimu mjadala kwenye chombo cha habari, anatumia lugha ya ukakasi hewani, hataki kuwapa host wake muda wa kuongea nk.

Sidhani kama ameelimika huyu jamaa,:ingawa shule anaweza kuwa amepitia.
 
siyo siri Kijana Jerry Muro, sijui Amekula Maharagwe Gani? Badilika Brother Umekuwa na Maneno Mengi Mapa haipendezi.
 
Leo ndo siku nimemdharau sana Muro, analeta siasa kwenye mambo ya maana.

TFF inabidi wamuangalie kwa jicho la tatu.
 
Mwesigwa alichokifanya ni kumjibu Jerry Muro. Alitakiwa ajibu hoja za Jerry Muro.
Jeri muro ni mbishi, mbumbumbu na mwenye majivuno. Kwenye mpira kiongozi wa club huwezi kubishia maamuzi na kanuni za wazi za CAFU na FIFA. Hii yaonyesha viongozi wa vilabu vya soka tulio nao. Anajivunia masters hajui watu wanaongelea PhD na post doc though waweza kuwa na hivi vyote bado mtu mwenye diploma akawa na weredi na uelewa zaidi.
 
Jerry Muro ni lofa Grade A ameambiwa ni mbumbumbu wa kanuni za CAF akaanza mboyoyoo kuwa kasoma ana masters etc.... leo kajaa upepo vibaya mno
 
Back
Top Bottom