Katibu mkuu Dr.W.P.Slaa punguza kamati - fungua makucha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katibu mkuu Dr.W.P.Slaa punguza kamati - fungua makucha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by THE PERFECT, Jul 19, 2011.

 1. THE PERFECT

  THE PERFECT Member

  #1
  Jul 19, 2011
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Binafsi nilikuwa msitari wa mbele katika kapeni zako katika uchaguzi mkuu uliopita, ulipochakachuliwa watu tulitaharuki,kimsingi tulikosa raha wapiganaji wote, lakini ulivyo na kipaji cha kuongea UlITUFARIJI na binafsi nilikuelewa hasa pale uliposema kuwa sasa ni muda muafaka kwako kukijenga chama kama katibu mkuu.

  Nilifarijika na turifarijika, kweli tumeona harakati Arusha,mbeya, ruvuma na mwanza binafsi nilikoshwa na huku kuliko mikutano mingine well... katibu mkuu naomba na kamati kuu ya chadema iwe inafanya maamuzi magumu kuliko kuwa mnaamua kuwa na kamati kila mara inapohitajika kufanya maamuzi

  1.kwa mfano isue ya Zitto kugoma kutoka bungezi siku ya ufunguzi wa bunge- kupinga matokeo ya uchaguzi na kudai katiba mpya.
  chemada iliunda kamati.
  2.isue ya Shitambala iliundwa kamati.
  3. kwa mfano issue ya madiwani arusha chadema imeunda kamati.
  4. kwa mfano isue ya Shibuda chadema imeunda kamati
  BUt isue ya Kafulila hakukuwa na kamati anyway...
  Katibu kama kamati ndio isue basi tuwe na kamati ya kushugulikia mambo iwe ya kudumu.

  my take: madiwani wa Arusha hatua zichukuliwe-kamati imetoka na barua bila hatua.
  sasa tena shibuda oh No its enough for kamati kamati ubadhilifu wa fedha
  na kupoteza muda na iman kwa wapenda maendeleo FUNGUA MAKUCHA
   
 2. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #2
  Jul 19, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Unataka afanye yeye uchunguzi au? Upupu huo.
   
 3. THE PERFECT

  THE PERFECT Member

  #3
  Jul 19, 2011
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  toa opinion za kujenga kama kweli ni mpganaji wa kweli...
  kama isue ya shibuda uchunguzi wa nini... wakati shibuda alishapewa barua ile ya awali
  na Zitto wake. warning lakini karudia tena maana yake nini? kamati ya nini tena ushahidi upo kila sehemu
  Red uchunguzi upi?
   
 4. m

  mwanakazi Member

  #4
  Jul 20, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kama ni kamati zinazotenda kazi husika vyema mimi nadhani sio tatizo! na hili nawapongeza cdm kwani tumeona mambo yao yakiisha vizuri tu kichama kupitia utendaji wa hizo kamati....katika chama au hata taasisi yoyote (tofauti na taasisi binafsi) kuunda kamati kwa tatizo linaloweza kuibua mawazo/maoni tofauti ni vyema na haki kwani itaepusha ile migogoro ya kwamba mtu flani ndo kanifukuza/kaniazbu....so 2 me nazani kamati ni muhimu hasa katika kuyapa maamuzi yatakayotelewa ile sura kuwa ni maamuzi ya chama na sio ya watu flani au ya viongozi.
  na kwa cdm itaepusha ile dhana ya kuwa cdm ni chama cha watu flani flani.....

  BUT Kamati za serikali yetu zisizo na meno wala effect yoyote ktk utatuzi wa matatizo na kero za wananchi mimi cziungi mkono kabisaaaaaaaaa! kamati za kutumia mamilioni ya fedha bila sababu za msingi nazani hazina tija hata kidogo.
   
 5. p

  politiki JF-Expert Member

  #5
  Jul 20, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  nikukumbushe kidogo mheshimiwa kuwa kafulila aliitwa kwenye kamati kwa ajili ya kujitetea lakini hakutokea mwenyewe na akaamua kujitoa kwa sababu ushahidi ulikuwa mwingi na mwenyewe alishauona. kuhusu kamati ni kitu kizuri kwa maana hapa mnayaweka maisha ya mtu kisiasa hatarini
  kwahiyo ni bora maamuzi hayo yapitie vichwa vingi ili kupata mawazo mbalimbali cha msingi tu ni kwa kamati kusimamia maamuzi yake ni hatari kwa maamuzi kama hayo kufanywa na mtu mmoja au wawili ndipo udikteta unapoanzia.
   
 6. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #6
  Jul 20, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Kamati ni muhimu sema labda iwe ya kuduma- kamati ya maadili that is all
   
 7. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #7
  Jul 20, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,483
  Likes Received: 5,567
  Trophy Points: 280
  Mkuu haya mambo ya kamati ndio tunayoyapinga kule chama tawala na serikali yao.sio kwa sababu hazitoi majibu tu bali zinatumia muda na gharama kubwa bure,kuna mambo yako wazi kabisa wala hayataki kamati,mtu ameongea upuuzi hadharani bado tunaunda tume! Hakuna namna ya kushughulika na mambo kama haya mpaka tume! Kwanza kuchelewa kuchukua hatua inafanya watu wasahau yaliyotokea na hivyo bdae kuleta dhana isiyo nzuri.tumepiga kelele na hizi tume kila cku alafu cdm wanaziendekeza tena! Hakuna justification ya kuunda tume kwenye makosa ya wazi na katiba ya chama ipo wazi sasa kamati imchunguze shibuda nini? We are not serious na haya ya kuzunguka mbuyu mwisho na cdm tutaanza kutafuta majibu ya kisiasa badala ya facts kwenye mambo mengi, let be straight na kila mwanachama aliyeamua kwa hiari yake kujiunga na chama ajue na kuheshimu hilo full stop!
   
 8. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #8
  Jul 20, 2011
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  kwa hili naunga mkono, chadema imekua kama ccm... tume, kamati, kabati etc

  weak or no decision making platform/capacity
   
 9. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #9
  Jul 20, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,483
  Likes Received: 5,567
  Trophy Points: 280
  kamati kwenye mambo yanayotaka tafiti na kuhusisha wataalamu wa fani mbalimbali.ebu tuseme ukweli kamati inamchunguza nini Shibuda?
   
 10. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #10
  Jul 20, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Dr.Slaa tuakuamini kwa usikivu fanyia kazi hili uone kama kuna umuhimu wa kupunguza kamati katika maamuzi.Kamati ziwepo tu kwa mambo technical yanayohitaji utaalam zaidi.Lakini la shibuda liko so objective.Halihitaji kuelimishwa, huyu ni mtovu wa nidhamu wana CCM kule shy walichoka naye kiukweli si kwa kusingiziwa.Nakumbuka pia aliwahi kuchelewesha maendeleo jimboni Maswa enzi za ubunge wa DR.Pius Yasebasi Ng'wandu kwa kuanzisha malumbano yasiyo na tija.CDM mkitaka kujua ubaya wa Shibuda fanyeni kumuuliza DR.Ng'wandu atawahabarisha uovu wa shibuda.It is evident that Shibuda must go now without delay
   
 11. F

  FUSO JF-Expert Member

  #11
  Jul 20, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,834
  Likes Received: 2,306
  Trophy Points: 280
  CHADEMA hawakurupuki katika kutatua mambo, CHADEMA ni taasisi kama ulikuwa hujui mpaka leo. So far so good for CHADEMA - Haya mambo madogo madogo ni sawa na kuwa na pilau zuri sasa mainzi nayo yale ya kijani na njano lazima yamendee mendee.

  Sisi tunachanja Bunga - wenzetu magamba mengine yameshindikana KUKOBOKA na mengine yanazidi kuota hadi Bungeni.

  Siungi mkono Hoja.
   
 12. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #12
  Jul 20, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Dr fanyeni maamuzi magumu kumng'oa shibuda. Swala lake halikuwa na haja ya kuunda kamati maana utovu wake umekuwa unajionyesha kwa kujirudia mara kadhaa.

  Mngeweza kumuita na kumsikiliza halafu mnapiga kura tu kupitia kikao cha kamati kuu kilicho kaa. Wengi wakibaliki ang'oke anapewa barua hapohapo. Kwangu kamati kwa shibuda si tija.
   
 13. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #13
  Jul 20, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  kama sijakusom vile,sijui unamaanisha nini!ninachojua,cdm ni chama makini isiyokurupuka katika maamuzi!!kwa hiyo we ulitaka mambo mengine wapotezee tu bila kuyachunguza!ni hatari kwa chama
   
 14. THE PERFECT

  THE PERFECT Member

  #14
  Jul 20, 2011
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naungana nawe mkuu... tumsaidie Dr. naona kutoka hapa atajifunza.... imagine Mnyika anajisikiaje pia sie ma fine wake?
   
 15. D

  Dr Willibrod Slaa Verified User

  #15
  Jul 20, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 675
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  Mouddymtoi,
  Thanks. Ni kweli Kamati zinachukua muda na wakati mwingine gharama. Lakini tukumbuke demokrasia ni aghali. Chadema inajali sana Demokrasia. Kanuni ya 8.0 ya "Kanuni za kusimamia shughuli,mwenendo na maadili ya Wabunge wa Chadema" (Toleo la 2006), inasomeka ifuatavyo:- Ili hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi ya Mbunge au Mwenyekiti wa Halmashauri hatua zifuatazo zitatakiwa zifuatwe:- i)Malalamiko ya utovu wa nidhamu au jombo lolote linalolalamikiwa yafikishwe kwenye kikao cha Kamati Kuu kwa maandishi kupitia ofisi ya Katibu Mkuu. ii) Kamati Kuu bila kulazimika kuita pande zinazohusika, itajadili "mantiki" ya lalamiko na kuona kama kuna hoja ya msingi katika lalamiko husika.iii) Kamati Kuu ikiridhika kuwa kuna hoja ya msingi itaunda Kamati ya watu kati ya 5 na 7 ili kuchunguza suala linalo lalamikiwa kwa kuwapa hadidu za rejea. Chadema huwa haikurupuku, bali inafuata Katiba yake, Kanuni, Maadili. Hivyo Dr Slaa hawezi kukurupuka akafumua "makucha" peke yake itakuwa kinyume na utaratibu tuliokubaliana ndani ya Chadema. Kuna mambo ya kiutendaji yaliyoko ndani ya mamlaka ya Katibu Mkuu, lakini pia kuna mambo ambayo yamewekewa utaratibu mahususi. Hata kama hatupendi utaratibu huo, lakini kwa kuwa ndio uliokubalika ndio utakaofuatwa hadi mamlaka iliyotengeneza katiba na Kanuni hizo itakapoweka utaratibu mwingine. Nadhani hoja hii imeeleweka.
   
 16. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #16
  Jul 20, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Dr Slaa kwenye mambo amboyo yako wasi hutoa maamzi hapo hapo ingawa hapa hapa jamvi watu wali mwandama sana kwenye issue ya kati wa Tabora alipo-msimamisha kazi...
   
 17. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #17
  Jul 20, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  you are a great thinker the perfect,binafsi sielewi ni kwanini wanamlea shibuda
  na wanaona kabisa kila kitu kiko wazi,...

  shitambala walimlea akaja kuwa aibisha,na shibuda atawachafua mda si mrefu
  pale atakapoa hama chama kabla ya mda wa bunge kuisha,...sijui mnaogopa nini,
   
 18. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #18
  Jul 20, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wakuu ameelezea vizuri sana Dr. Slaa kuwa anafanya hivyo kwa kufuata katiba ya chadema, na si maamuzi yake yeye kama Dr. Slaa ama Katibu Mkuu wa chadema.
  Kwa hiyo kama tunataka Dr. Slaa aoneshe "makucha" yake basi hatuna budi kufanya marekebisho ya katiba ambayo naamini haijatengenezwa na Dr. Slaa pekee.
   
 19. N

  Nyakarungu JF-Expert Member

  #19
  Jul 20, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  VIONGOZI NA WAPENZI WA CHADEMA,

  Taifa letu linaingia katika matatizo makubwa na ya aibu, si kwa sababu hatuna kanuni wala si kwa sababu hatuna katiba inayokidhi viwango vya utawala bora.
  Sifa zote za kutengeneza kanuni tunazo na nyingi zimeandikwa na wengi tunazisoma.

  Tatizo kubwa ni aina ya watu wanaosimamia hizo kanuni na sheria, watu wasio na haiba ya heshima kwa kanuni na maadili ya taaluma zao, watu wasiofikiria kesho juu ya maamuzi ya leo, watu hao hujikuta wanavunja utaratibu yakinifu wa kanuni au hata sheria kwa manuafaa binafsi.

  Hivi sasa nchi yetu imefikia hatua mbaya ya mambo ya kijamii na kiuchumi kwa sababu hizo za kuwa na watawala waoga wa kuheshimu taratibu na kanuni amabazo pengine zimewafanya wao wafikie hatua waliyonayo ya kiutawala.

  Niliwaona wanachama na wapenzi wengi wa chadema wakiwa na mihemuko ya kutaka Shibuda afukuzwe, ni kweli wengi walitaka afukuzwe kwa makosa yaliyoainishwa hapo kabla,...........
  Chadema chama kinachopendwa na kuaminiwa na wanachi na wanatamani siku moja kichukue dola, ni lazima kikae mbali na aina hiyo ya uendeshaji niliyoiweka hapo juu, ni lazima kifanye mazoezi ya demokrasia, ni lazima kionyeshe UMMA kuwa kinahehimu kanuni zake za kikatiba au za kitaasisi kama zilivyoandikwa, ni lazima kiwe tayari kuwapa imani wananchi juu ya uwezo wake wa kuheshimu demokrasia na watu wawaamini viongozi wake hawatageuka kuwa madkteta kama watapewa nchi.

  Hivyo nasisitiza wasingeweza kuchukua hatua kwa kupima upepo wa wananchi bali kwa kupitia njia sahihi na ya kuaminika kwa wote.
  kamati imeundwa na viongozi tunaowaamini na tuwape muda watakuja na maandiko ya kitaalam yatakayotoa majibu ya mwisho.

  Kuundwa kwa kamati sio taabu ila taabu iko kwenye uwezo wa kamati,na hatua baada ya kamati kukamilisha kazi yake, kamati zote huundwa kwa lengo moja la kutaka kupata ukweli kwa njia za kitaalamu na haki, kamati iliyoundwa na kamati kuu naiamini kwani inaongozwa na mwanasheria A. Safari, na wasaidizi wake ni watu ninaowafahamu kiwango cha umakini wao.

  Tofauti ya kamati za chadema na zile ziundwazo na serikali yetu ni kuwa;- Matokeo ya utafiti wao huwa siri, na hubaki mikononi mwa kiongozi mkuu wa nchi, hivyo uamuzi wa kuchukua hatua au hata kuzitoa hubaki wake,kwa chadema tunaomba ziwe wazi na kwa kuwa kamati hiyo ndogo imeundwa na kamati kuu basi taarifa hizo zitapelekwa katika kitengo ilichoelekezwa na hazitakuwa za siri, ili ziwape wananchi imani zaidi na wananchi watofautishe kamati za chadema na zile nyingine, kuliko kuziweka chini ya meza na kuwafanya watu waanze kuzifananisha na zile ziundwazo na kuushia kuwa na matokeo ya siri,ni lazima tuwe tofauti na wanaomalizia zamu yao ya kuwaonea wanynge.

  Naamini mtanielewa kuwa chadema ni chama tofauti sana na kina mikakati ya kujiweka tofauti kwa vitendo sio kwa kauli tu, nawaomba tuvute subira.
   
 20. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #20
  Jul 20, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Unataka yafanywe maamuzi ya kukurupuka?wewe unataka CHADEMA iwe kama NCCR MAGEUZI YA 1996 ambapo mrema alikuwa anafanya maamuzi ya haraka na ya kijinga?acha watu wafanye uchambuzi yakinifu kabla ya kutoa maamuzi!!
   
Loading...