Katibu mkuu CWT asimamishwa, ni yule aliyekataa uteuzi wa Rais Samia

Kulwa Jilala

JF-Expert Member
Sep 6, 2022
3,510
7,755
Kamati ya Utendaji ya Taifa ya Chama wa Walimu Tanzania CWT imemsimamisha kiutendaji Katibu Mkuu wa chama hicho Josephat Maganga, kwa tuhuma za uvunjifu wa katiba ya Chama na kanuni zake ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka na fedha.

Akizungumza na wanahabari jijini Dodoma mwenyekiti wa kikao cha Kamati ya Utendaji Taifa ya Chama cha Walimu Tanzania Thobias Sanga, ambae ni mwakilishi wa Walimu kutoka Njombe, amesema kuna changamoto kubwa katika utendaji hasa matumizi ya 2% makato ya mshahara wa walimu.

Kikao hicho kimefanyika chini ya mti kikiwa na wajumbe 18 kati ya 32 wa Kamati ya Utendaji ya Taifa ya CWT, wakimsimamisha kiutendaji katibu mkuu wa chama hicho hadi pale tuhuma zake zitakapofikishwa Katika baraza kuu

Chanzo: EastAfrica TV
 
Cc Mpwayungu Village
FB_IMG_1686054824727.jpg
 
Hao viongoz wapigaj tu, hakuna la maana wanalofanya zaid ya kugawa tishet na sakfu

Cwt inaenda kufa shimon sasa, ni vile tu serikal imefumbia macho lkn kuna uozo huko

Sasa walimu ujanja ni chama cha chakuhawata makato 5000/= only kuliko huko 2%
 
Back
Top Bottom