Katibu Mkuu CHADEMA Dr.Vicent alaani tukio la Mkuu wa Mkoa Mrisho Gambo kuvuruga uwekaji wa jiwe

Nimewashukuru sana ITV kwakweli kila mwenye macho kaoni jinsi Lema alivyo haribu sherehe hadi wafadhili wanampigia magoti anyamaze mkuu wa mkoa amalize... Hivi lema alijuaje hatotajwa wakati mkuu wa mkoa hajamaliza kuongea?
Mimi nafikiri Lema anapaswa kupimwa akili.
Ni kweli kabisa........maana hata angekuwa ni mkurya angesubiri kwanza then ndio angeanza kuonyesha yaliyo moyoni amewahi kumkatisha jamaa kabla hajamaliza kuzungumza....
 
Lema Alikuwa anawashwa na nini hadi akawa anapiga makelele? ni Sawa na Siku ya Uzinduzi wa Daraja Raisi anaongea alafu Dau asimame aanza kupiga kelele... nini maana yake hii kwa Lema ukosefu wa Heshima kikazi huwezi kumuhukumu mkuu wa Mkoa kama hajamaliza kuongea Mrisho kamstahi sana Lema maana Lema alistahili kwenda lock up directly and then lile kosa alilosema kuwa Mkuu wa Mkoa atumie Polisi la sivyo atauwawa natumai yupo lock tayari akisubiri kupelekwa kesho mahakamani kwa Kutishia kuua hadharani sidhani hata kama kunahitajika ushahidi zaidi ni aanze tu kutumikia kifungo...
 
Yaani wafadhili wanawekeza billions of money hapo nyie mnaleta siasa,aibu gani hii kwa Taifa
 
Ila CHADEMA bwana, wana unique behavior, mbunge ambaye wananchi wamekupa heshima kwa kukuamini na kukupigia kura uwaongoze, wakiwa na uhakika na hekima na busara zako unaanza kupayuka na kuleta fujo mbele za watu eti kisa haujapewa Promo. Kulikua na sababu gani kuleta zile fujo? Haikutosha kusubiri zamu yake nae akasema ukweli? That is stupid. Je sasa ndio umeonekana kiongozi bora? Tunashindwa kujifunza chochote kutoka kwako brother lema.
Yaani acha tu na kuna mapuuzi eti yanamsifu kuwa alichofanya pale ni sawa sawa maana hakutendewa haki........mimi nimeona aibu sana ingawa yule si mbunge wangu.
 
Hawa jamaa Mungu alisha walaano kwa kuwanyima akili na maarifa,haiwezekani zaidi ya miaka 55 ya uhuru wameshindwa kuwawezesha wananchi kupata hata mlo mmoja wa siku zaidi ya umasikini mtupu,ujinga,maradhi,ufisadi na kadha wa kadha.
Bora unyimwe kingine na Mungu kuliko kunyimwa akili na maarifa,haiwezekani Taifa lilojaliwa na kubarikiwa na Mungu kwa kuwa na rasilimali karibia zote dunia lakini watu wake hata mlo tu hushindwa kupata.
Hakika ccm imelaaniwa na watu wake pia toka kwa Allah na adhabu hii hakika itawala wote vizazi na vizazi kwa yeyote yule aliye ndani ya ccm.
Ni aibu ya dunia RC mteule wa nafasi za ukada wa chama chake afanye maajabu mbele ya wageni na Mhe. Mbunge aliyechaguliwa na wengi kwa maslahi ya wengi tofauti na yule wa kuafuata maagizo ya Mkuu wake na kumridhisha pamoja na
chama chake.
Time will tell soon vs the hell ccm and his people.
Amen mufti.....aaaaamen
 
Tangu 1961-2015 ccm iliongoza mtaa Fulani,mwaka 2016, ccm ilipigwa chini mwenyeti mpya kupitia chadema,ametafuta wadau wakawekeza tukapata solo kubwa ,ccm wakakaa kwenye vikao vyao nakusema tumzuie eneo hilo nifinyu,wakasema likifanikiwa atatushinda uchaguzi ujao!!

Hii ndio ccm ambayo lengo kubwa kwao simaendeleo ya watu bali ya kikundi cha ccm( chukua ......)
Sasa ka wameshindwa miaka hamsini kutengeneza hata madawati sembuse maendeleo.
 
Kama kuna viongozi wanaivunjia heshima serikali ya Yohana basi ni huyu jamaa wa Yohana, ametufanya tuone mamlaka ni kijiwe cha kusutana na kufanya kila aina ya upumbavu
 
CCM wanazidi kujivua nguo.
Huyo Gumbo atapata credit kubwa akishirikiana na Lema. Ila akichuana nae ataondoka kama wengine.
Arusha wanampenda Lema na hawaangalii sera.

Mrisho Gambo ni Mkuu wa Mkoa Arusha sio Arusha Mjini.
Godbless Lema ni Mbunge wa Arusha Mjini sio wa Mkoa Arusha.
 
Back
Top Bottom