Katibu Mkuu CHADEMA Dr.Vicent alaani tukio la Mkuu wa Mkoa Mrisho Gambo kuvuruga uwekaji wa jiwe

Ndomaana nasema kuwa razima tufe na kupona tudai katiba mpya iri tuondoe uo ukada kwenye cc m tuhamue tunataja katiba mpya
 
Machadema hayana hoja kwa sasa....Lema jana alikua hataki jina la mawala litajwe na Gambo
 
alimzuiaje?? kwa kutomtaja ama??
Mkuu hata mimi najiuliza hayo maswali!
Mkuu wa mkoa amefanya kosa gani la kuleta ile kadhia!!
Au hawa wenzetu Ni vichaa??? Kwasababu kila nikirudia kuiangalia video naona Mkuu wa mkoa akihitubia Na Lema kuleta fujo tu!!
 
Motochini,

Hebu tuipende Tanzania, tushirikiane kuilinda, kuihifadhi na kuiendeleza, tusishangilie Upuuzi wenye kuidumaza. Ujenzi wa mradi ule ulipaswa kutazamwa kitaifa zaidi kuliko kimashindano ya siasa za vyama. Naona RC kakwamisha juhudi za Rais kutaka maendeleo ya nchi. Katupaka rangi chafu kwa Wahisani. Usiseme wahisani ni nani na ni nini kama wengine walivyopata kujiropokea katika fedha za MCC, duniani tunaishi kwa kushirikiana.

Kwa waumini wa vyama kuliko taifa, RC yuko sahihi. Mimi nasema alilolifanya halina manufaa kwa Tanzania. Anapaswa kulaaniwa.

Hapo ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa. Unapoteza muda wako bure ameshindikana huyo!
 
Nilisikia hata wananchi waliokuwa kwenye Mkutano huo wakiguma na kupiga kelele kupinga alichokuwa anakisema RC. Wenye Clip waiweke humu ili watu waache kuleta uongo uongo. Ni kweli kwamba Lema hajafanya vizuri kujaribu kumkatiza RC wakati anatoa hotuba yake, hapo hata mimi siko nyuma yake. Lakini kosa kubwa kabisa, ni RC ambaye anapaswa kuonyesha uongozi na ukomavu kuongoza shughuli nyeti kama hizi, kufanya siasa za chuki za wazi wazi kwenye mambo ya msingi yanayowahusu wananchi anaowaongoza. Kuna ushahidi wa kutosha kabisa kwamba Mbunge Lema ameshirika kwa kiasi kikubwa katika kufanikisha mradi huo. Na zi lazima miradi yote mizuri iletwe na chama cha Mapinduzi peke yake. Na maneno aliyokuwa anasikika akiyazungumza Lema mbele ya umati huo wa watu ni ya ukweli. Swali langu, hivi ni nani aliyesema katika nchi hii ni dhambi kumsifia kiongozi wa upinzani anapokuwa amefanya jambo zuri? Je ni kweli RC Gambo angemshukuru Lema kwa kazi yake nzuri ya kufanikisha mradi huo, chama chake kingekosa kura mwaka 2020?
 
Machadema hayana hoja kwa sasa....Lema jana alikua hataki jina la mawala litajwe na Gambo
Lema ana matatizo mawalla ndie katoa kiwanja kulikuwa na sababu gani apande hasira vile?halafu ninamshangaa lema eti mradi usimame usiendelee kisa eti yeye hajatajwa kushukuriwa! Yaani wanawake na watoto wakose kisa eti mkuu wa mkoa kwenye hotuba hajamshukuru lema kwa mchango wake? Lema ana akili timamu kweli?
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimelaani vikali kitendo kilichofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kumzuia Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya huduma za mama na mtoto.

Akizungumza tukio hilo Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Vicente Mashinji, alisema kuwa amesikitishwa sana na kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Arusha kuvuruga sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya huduma za mama na mtoto

"Si tu kwamba ameonyesha kukosa staha kwenye jamii, pia ameonyesha kutounga mkono mahitaji ya nchi na dunia mzima "hasa kwa mahitaji ya akina mama na watoto" alisema

"Nalaani tabia hizi za kihuni zisizo na tija kwa Taifa. Ikumbukwe tu kwamba, mwanzo ngoma ni lele, tabia ya mkuu wa mkoa huyu inajenga chuki na yaweza kuleta machafuko yasiyo na lazima, mtu wa hivi hafai kabisa katika jamii "alisema Katibu Mkuu

Tukio hilo linadaiwa kuleta aibu mbele ya viongozi wa mataifa ya nje akiwemo kiongozi mwakilishi wa ADF pamoja na Mwakilishi wa Maternity Africa.

Chanzo: Hivi sasa

Mkuu, hakuna aliyemzuia mh lema kuweka jiwe la msingi, ukizingatia kuwa yeye ndiye aliyefanya chini juu mh.gambo awepo kuweka jiwe la msingi. Hata mimi ningefanya kama mh gambo
 
Nilidhani huwa una busara kumbe na ww umeona kukwea ngazi inakubidi upindishe ukweli?

Kuna fafanuzi nyingi + Video Clip humu ndani huwezi kuzisoma na kuelewa kilichotokea? Au unadhani hiyo video imejituma tu hakukuwa na wahudhuriaji wengine ktk eneo la tukio?

Be neutral unless otherwise utakuwa bias.
Kwa hiyo.unataka niseme nini? Kwa clip niliyoiona mimi nimeona kwamba Lema ndiye kaleta vurugu. Naomba ya kwako inayoonyesha Mkuu wa Mkoa akileta vurugu kwa sababu mimi.sijaiona.
 
Kwenye suala LA maendeleleo huyu mkuu wa mkoa anafanya anatafuta sifa za kumahushia hadhi yake kwa jamii....kama anatafuta kujionyesha kwa bosi wake kuwa anapingana na upinzani afanye hivyo kwa kuleta jambo jipya LA kimaendeleo na si kudandia mgongoni mwa juhudi za watu wwngine.....kwa nyakati hizi Watanzania wa kudanganywa kihivyo ni wachache sana....
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimelaani vikali kitendo kilichofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kumzuia Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya huduma za mama na mtoto.

Akizungumza tukio hilo Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Vicente Mashinji, alisema kuwa amesikitishwa sana na kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Arusha kuvuruga sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya huduma za mama na mtoto

"Si tu kwamba ameonyesha kukosa staha kwenye jamii, pia ameonyesha kutounga mkono mahitaji ya nchi na dunia mzima "hasa kwa mahitaji ya akina mama na watoto" alisema

"Nalaani tabia hizi za kihuni zisizo na tija kwa Taifa. Ikumbukwe tu kwamba, mwanzo ngoma ni lele, tabia ya mkuu wa mkoa huyu inajenga chuki na yaweza kuleta machafuko yasiyo na lazima, mtu wa hivi hafai kabisa katika jamii "alisema Katibu Mkuu

Tukio hilo linadaiwa kuleta aibu mbele ya viongozi wa mataifa ya nje akiwemo kiongozi mwakilishi wa ADF pamoja na Mwakilishi wa Maternity Africa.

Chanzo: Hivi sasa
Huyo katibu Mkuu wenu Mashinji ufahamu wake mdogo, Lema kazuiwa wapi na kwa nn huyo katibu asilaani utoto uliofanywa na LEMA
 
Huyo katibu Mkuu wenu Mashinji ufahamu wake mdogo, Lema kazuiwa wapi na kwa nn huyo katibu asilaani utoto uliofanywa na LEMA
La msingi hawa viongozi siasa zao waweke kando linapokuja suala kama hili

Ilikuwa haina maana ya kuleta ubishano
 
Back
Top Bottom