Katibu Mkuu CCM kukaimiwa na Naibu Katibu Mkuu Bara, Anamringi Macha. Ni bada ya Chongolo kujiuzulu

Hakuna mtu aliyeko CCM mwenye uwezo wa kushindana ama kuwekeana bifu na aliyekalia kiti cha enzi. Ni unalia, unagugumia ukimaliza unafuta machozi maisha yanaendelea.

Samia amechagua kushika njia yake na taratibu linakuwa joka kubwa zaidi ya Magufuli.

Kinana na JK ni ufisadi tu ndo unawatoa roho na wanaona njia zao nyingi hasa Bandari ulaji unakatika na mishe nyingi za JK zinakwenda mrama sio kwakua aliyeko madarakani anawabania laah isipokua aliyeko madarakani anaogopa kuwabeba.

The only person angeweza kubeba uchafu wa JK na mawakala wao alikua Lowassa peke yake. 2015 ilikua ajali kubwa sana kwa wanamtandao na hawatakaa wapone yale majeraha. JK aridhike na Posho za Salma na Ridhiwani.
Mkuu angalia draft yako vizuri, look at what they are not showing us, that is the bigger picture! Focus on the kingmakers not the kings!
 
Mbaya zaidi hao wote wakitoka wanakua victim wa kivuli cha rais na aliyeko madarakani hajifunzi na aliyetoka hataki kuwa somo la historia kwa watu.

Nyerere alikuja kuwa victim wa siasa za akina mwinyi na watu wao....

Mwinyi somehow alikua victim wa siasa za mkapa...

Mkapa akawa victim wa siasa za wanamtandao hadi kufikia kulia kwa kijana wake Magufuli.

JK na wanamtamdao wenzie walikua victimised na siasa za magufuli kupita kiasi and magufuli asingekufa JK alikua anakwenda ndani.

Samia alifaa awe mwanafunzi mwema wa historia bahati mbaya sana historia haimjengi mwafrika kulinganisha na wenzetu ulaya.
Mkuu pokea 👏💐🎖️
 
View attachment 2828819
Tumepokea barua ya kujiuzulu kwa Katibu Mkuu wetu, Ndugu Daniel Chongolo. Tumeridhia.

Tunafanya uchunguzi na jambo hili linaweza likachukua muda kukamilika, kwa sababu hiyo Naibu Katibu Mkuu (Tanzania Bara) utakaimu hadi hapo taarifa ya uchunguzi itakapokamilika.

(Haya ni maneno ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan ndani ya kikao cha NEC kilichofanyika jijini Dar es Salaam leo.
No time to waste!, Anamringi apandishwe cheo ashike nafasi ya chongolo!
 
Unaiba kura iwapo huna kura za kutosha, sisi tukiiba tutaishia kujiibia zetu. Hatuhitaji katiba ya kupendelea chama chochote, Bali tunataka katiba inayoheshimu matakwa ya wananchi sio ya kikundi fulani.
Hamjawahi kuwa na kura za kutosha na wengi wenu hawapigi kura hufurahia amsha amsha za kampeni mwisho wa siku hawana muda wa kupoteza kwenye fuleni!
 
Binafsi nampongeza chongolo kwa moyo wa dhati, uamuzi wa kungatuka ni uamuzi wa busara mno, Amekwisha ona kwa mbali sana ya kwamba wale vijana wasio na adabu wala nidhamu na wenye viburi huenda wakaingizwa chamani, ya nini kuja kuvunjiana heshima na vijana ambao pengine walikosa malezi na kufunzwa adabu, amengatuka, hana makubwa apangiwe kazi nyingine hana tatizo!
 
Kwa hii kauli ya Samia maana yake maneno aliyoandika Chongolo jana kuhusu kujiuzulu kwake ni ya kweli, amesingiziwa uongo, hivyo akaamua kujiuzulu ili kulinda hadhi yake na ya chama chake.

Tatizo linakuja, kama issue ya Gekul Samia aliweza kuchukua hatua, jambo linaloonesha alishauriwa na vyombo vyake vya usalama, iweje kwa hili la Chongolo Samia atuambie anafuatilia?

Kwanini asingefuatilia ili kujiridhisha halafu watakapokutana kwenye hiki kikao chao awe na jibu kamili? au Samia anataka kutuaminisha hili la Chongolo linekuja ghafla sana kuzidi lile la Gekul?

Hapa Samia ameamua kufunika kombe mwanaharamu apite, baada ya muda wamteue KM mpya maisha yaendelee, kwa maana nyingine kapigwa bao na Chongolo.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Akina nani hao wameendasha ajenda ya kumchafua Chongolo?

Kwamba kwasababu alisikia tetesi za uteuzi wake kutenguliwa, kaamua kujiuzulu mwenyewe baada ya kujitungia uongo wa kujichafua?
 
Back
Top Bottom