Katibu Mkuu CCM Dk. Bashiru atolea ufafanuzi na upotoshaji wa Maalim Seif Sharif

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
KATIBU MKUU WA CCM DKT. BASHIRU ALLY ATOLEA UFAFANUZI UPOTOSHAJI WA MAALIM SEIF SHARIF HAMAD

03 Desemba, 2019

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally amesema, Maalimu Seif aliyekuwa kada wa CUF kabla ya kuhamia ACT, atumie elimu yake vizuri ajenge Chama Chake ili kiweze kushindana na CCM.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na wanaCCM Mkoa wa Kusini Pemba alipokuwa akizundua tawi la Ole jimbo la Ole mara baada ya kufungua tawi hilo.

Amesema katika ziara yake ya siku tisa visiwa vya Unguja na Pemba, ina lengo la kuimarisha uhai wa Chama (kufunga mitambo) ya ushindi kwa uchaguzi wa mwaka 2020 hivyo, amesikitishwa na kauli ya Maalim Seif ya kukejeli ziara hiyo ambayo ipo kihalali na madhumini yake ni bayana.

"Maalim Seif hakuwahi kwenye matamko yake ama mikutano yake kunizungumzia kwa ukali na chuki kiasi kile kama alivyofanya, hivyo kama mitambo tu nimeifunga siku tisa mitetemeko hii imeanza kusababisha taharuki je ikianza kufanya kazi itakuaje? Mimi sitaki kumjibu maana kwa bahati mbaya anawashauri wabaya kwa sababu kwa kasi ya ziara yake asingewezea kufuatilia bila kuwatuma watu, na ziara yangu kote imekuwa hadharani na vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti, nimeshangaa kusikia mambo ambayo hayakutokea kwenye ziara yangu" Katibu Mkuu amesisitiza

"Katika hili niwaase wanaCCM na watanzania msimuhukumu Maalim Seif kwa kuwa hata yeye anapotoshwa na wanaomshauri, tangu awe mshauri amekuwa hatafuti tena taarifa za kweli, kila anachopokea anakwenda kuropoka". Ameongeza

Aidha, ametumia fursa hiyo kumuomba, ajenge chama chake kipya maana chama kile kinahitaji muda wa kutosha akianza kufukuzana na mitambo yake asilaumu kwenye masanduku ya kura atakapofungua na kukuta sifuri.

"Mimi ninatumia fursa hii kumshauri, Muda hauna huruma, muda hausubiri, kupoteza muda kufukuzana na mitambo ninayoifunga itamgharimu yeye na chama chake, hivyo awe na nidhamu ya muda na ajenge chama chake kichanga na Sisi tujenge chama chetu tukutane uwanjani." Ameongeza

Dkt. Bashiru ameendelea kwa kueleza kuwa, watanzania wa leo na Tanzania ya Dkt. John Pombe Magufuli na Dkt. Ali Mohamed Shein hawadanganyiki tena wana macho yao na wanaona, na hasa vijana waliodanganywa kwa muda mrefu na wametumia hila nyingi sana kuwadanganya leo wametambua ukweli.

Aliongeza pia Maalim na wenzake wametumia hila nyingi sana kuwadannya watanzania kuhusu Muungano, kuhusu miradi ya maendeleo, lakini miaka takribani kumi na tisa ya Dkt. Ali Mohamed Shein akiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar amefanikiwa kuimabadilisha kwa kiasi kikubwa Zanzibar, imekuwa na amani nautulivu kwa kiasi kikubwa, miradi mingi ya maendeleo imetekelezwa kuliko kipindi kingine chochote amekuwa ni mtu wa kuhimiza amani, upendo na maendeleo wakati wote.

"Kazi ya Dkt. Shein imejenga na kuboresha mahusiano mazuri baina ya Wazanzibar na Tanzania bara, sasa maalim Seif anawatangazia watu kuwa ziara yangu ya siku tisa visiwani Zanzibar ni kuitawala Zanzibar, hili ni jambo la ajabu na ni la chuki nzito dhidi ya watanzania ninawasihi wasimuhukumu wamsamehe." Dkt. Bashiru ameeleza

Pia Katibu Mkuu aliendelea kufafanua kuhusu vikao mbalimbali alivyovifanya akiwa Afisi kuu Zanzibar ambavyo havikuwa vya usiri wowote na kila jambo lilikiwa wazi kwa kuwa yote yaliofanyika yalikuwa ni yenye kulenga kuboresha maisha ya watanzia na na sio kama alivyodanganywa na wanaomshauri kumpotosha.

Wakati huo huo, Dkt. Bashiru amemshauri Maalim Seif kutumia elimu aliyoipata kwa jasho la Watanzania kwa manufaa ya watanzania nasio kujaribu kuifarakanisha nchi kwa uchu wa madaraka.

Kabla ya mkutano huo wa ndani, Katibu Mkuu ameshiriki ujenzi wa jengo la Tawi la Kendwa, ametembelea wazee, na kuweka jiwe la msingi katika Tawi la CCM la Ole.

Hii ni ziara ya kuimarisha uhai wa Chama na kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015 - 2020 Visiwani Zanzibar.

Imetolewa na;
Afisa Habari
Ofisi ya Katibu Mkuu
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

IMG-20191203-WA0054.jpeg
IMG-20191203-WA0056.jpeg
 
Back
Top Bottom