Katiba ya WANANCHI vs YA MAKINDA

Pax

JF-Expert Member
May 3, 2009
268
87
Kama ilivyopendekezwa lazima tuanze kujipambanua kati ya wanaouunga "Muswada wa Makinda" versus " Muswada wa Wananchi". Kwa mtizamo wangu kama tutajigawanya katika pande hizi mbili, majina haya tu yanatupa sisi tunaopinga muswada wa Makinda nafasi kubwa ya kushinda. Hamna mtu mwenye akili timamu atakayesimama kwenye jukwaa kusema anautetea muswada wa Makinda, hilo jina linabomoa mno. Hata kwa mtu wa kijijini kabisa akiambiwa achague pasipo hata kujua kilichomo ni wazi atachagua upande wa wananchi.

Tukitumia jina kama chungwa na ndizi walivyotumia Kenya haitakuwa rahisi sana kwa wananchi kuelewa na tutatumia nguvu nyingi mno kupiga kampeni. Lakini tukitua majina nayopendekeza itahitaji little efforts watu kujua nini tunapigania. Na ushindi ni dhahiri. Naomba tuanze kueneza majina haya mawili na kuajiandaa kwa kampeni.

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom