Katiba ya CCM VS Watanzania; Vita Vimeanza na Kikwete Hana Majibu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katiba ya CCM VS Watanzania; Vita Vimeanza na Kikwete Hana Majibu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by niweze, Apr 8, 2011.

 1. n

  niweze JF-Expert Member

  #1
  Apr 8, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tumeona jinsi gani hiki chama ccm na viongozi wake wanacho tarajia kukifanya juu ya katiba yetu. Ukweli ni kwamba, tulioyaona mwaka jana sio uhujumu ila na vita vilianzishwa kuwa kandamiza watanzania. Mbinu zilizo tumika kumwibia Dr Slaa uraisi zimeandika “Katiba” tena kuwakandamiza Watanzania kwa miaka mingine mitano. Kinachotuacha na butwaa watanzania wote ni kwamba mishtuko tunayoiona katika jamii yetu sasa inazidi kuwa mikubwa sana. Ni kweli sisi watanzania tunashindwa kuwazuia ccm wasilete hii katiba yaoTanzania? Hili ni swali la kila mtanzania na lazima tuanze kampeni kubwa kuwaelimisha watanzania wote.

  Kwanini nasema hivi na kuwataka watanzania wajiandae na vita kuzuia hii katiba ya ccm? Tumeona uchaguzi ulivyoibiwa na tunajua wengi mpaka leo hatuamini hili limetokea October 2010. Tume ya Makame ilifanya kazi ya kuiba kura kila mkoa na mpaka leo hatuna majibu kwanini wananchi walinyimwa haki yao ya kupiga kura, hasa vijana? Kwanini wananchi milioni karibu 20 waliojiandikisha na waliopiga kura ni milioni 5? Kwanini matokeo ya wagombea wote wa upinzani walinyimwa haki ya kuyaona matokeo katika vituo vyote? Tusema haya ni matokeo au udanganyifu wa kumweka kikwete na kuwaandaa watoto wao kama January aje kuwaongoza watanzania kama baba zao? Majibu, Katiba iandikwe na sheria ziundwe jinsi ya kuundwa kwa kamati ya usimamizi wa uchaguzi na wawakilishi toka kila chama. Kila mgombea apate haki ya kuyaona matokeo kituoni na kupata haki ya kuyapinga kabla hayajatangazwa na mahakamani ili kulinda demokrasia ya watanzania.

  Jambo jingine nataka tulizungumzie ni kuwepo kwa madaraka ya raisi yasiyo na maana. Nchi kama Tanzania haihitaji kuwa na raisi ambaye anapewa madaraka ya kuteua viongozi kila mahali. Kazi ya raisi lazima ielezwe kwa upya na madaraka ya raisi pia yapunguzwe ili lengo liwe kujenga nchi. Hakuna umuhimu wowote ule kwa raisi kutoshtakiwa kwa makosa akiwa ofisini na hata akiwa ameondoka ofisini. Tanzania leo hatuna umuhimu wa raisi kuteua viongozi hasa baraza la mawaziri bila uchunguzi wa rekodi zao na utendaji wao uliopita, hasa bila kuhusisha kwa kamati za idara bungeni. Historia ya uongozi wa ccm tumeuona, raisi Mwinyi, Mkapa na Kikwete wote wanaonekana mbele ya Watanzani kama ni wenye makosa mengi na wanaongoza kwa uvunjaji wa sheria za nchi. Tukianzia kwa Mwinyi, ndie alianzisha uingizaji wa makampuni fake Tanzania na kutokuwa mkweli. Sifa moja chafu ya Mwinyi ni Mkewe ambaye alihusika na biashara kila mahali bila kulipa kodi. Mwinyi aliuza viwanda na hata wanyama bila idhini ya watanzania. Mkapa ndio sasa King wa wizi Tanzania, Mkapa kaongoza Tanzania na tukipatwa na wizi mkubwa wa mabilioni ya pesa yakitoweka, zaidi mkewe nae akiongoza makampuni ya ajabu Tanzania. Mkapa kaongoza chini ya wizi wa pesa kwenye makampuni na zaidi hili swala la rada ambalo ni aibu tupu, makampuni yaliohusika na hizi scandals uingereza waadhibiwa wazi na kukubali makosa yao ila Tanzania hakuna hatua yeyote imewaachukuliwa kati ya Mkapa na Yona. Kikwete yeye katumia uraisi wake kuwaibia watanzania wizi wa EPA, Dowans na migodi, zaidi ni uchaguzi wa 2010. Legacy ya maraisi wa Tanzania tunafahamu na “Katiba” peke yake ni jibu. Watanzania tusikubali na Tujiunge kukataa majibu ya Katiba ccm, Tunataka "Katiba" na Democratic Reforms kwa manufaa ya Watanzania. Tunachokiona ni kwamba ccm wanawategemea wajinga na wasiosoma na kuandika kuunga mkono katiba hii wanayotengeneza.

  Maswali na ushauri kwa Dr Slaa na Chadema, viongozi wa vijana cdm, viongozi walimu chuo kikuu dsm, vijana nchini, wazalendo wachache ndani ya ccm; mtakaa kimya hii katiba ipitishwe na wabunge wa ccm na chama chao?
  Mikakati gani mnafanya kuwaelisha wasiotambua umuhimu wa katiba au walionyuma?
  Ushahuri kwa Chadema ni kuendelea na maandamano na mikutano ya kuwaelimisha wananchi taifa zima. Tunajua according to UN human rights, wananchi wana haki ya kuandamana kwa amani kudai haki zao. Evidences tunaziona huko Libya, Ivory Coast, Ushindi wa kumwondoa Mubarak – Egypt na Ben Ali – Tunisia. Tupiganie haki zetu, demokrasia yetu na kujenga taifa jipya.
  Bunge lawaka moto

  404
  Wanasiasa wapinga muswada wa kurekebisha katiba

  To be Continue...
   
Loading...