Katiba ya ndoa/mahusiano

Kimsingi vipengele unavyovitaja ni muhimu na nafikiri ni muda muafaka wa kuanza kuvianisha na kuvijua hata kabla haujaingia kwenye ndoa tatizo ni kuwa wengi wetu hatusomi hivi vitabu vya dini kwasababu vitu vya msingi ulivyovizungumzia vingi viko kwenye vitabu vya dini na vinatoa muongozo wa majukumu ya msingi ya kila mmoja wetu

hebu tupeni maandiko yaliyo define majukumu ya ndoa kwanza

chakula kitafutwe na nan na nani akitayarishe

watoto ni jumuku la nani kulea

usafi wa nyumba kazi ya nani? :d
 
NN

mie naona bora watu wachukulie kuwa ndoa ni mkataba labda wanaweza 'kujitoa' wakiona wameshindwa.

sasa hivi mtu analazimisha kukaa na mtu pengine japo anamtesa kwa kuwa hajui kuwa ni mkataba tu kaa mwengine anaweza kujivua akiamua
 
akuna katiba zaidi ya yale mwanzilishi wa ndoa mwenyewe yani mungu aloiweka mtakwenda kushoto na kulia ukweli utabaki palepale
 
hebu tupeni maandiko yaliyo define majukumu ya ndoa kwanza

chakula kitafutwe na nan na nani akitayarishe

watoto ni jumuku la nani kulea

usafi wa nyumba kazi ya nani? :d

kwa juu juu biblia inasema mwanaume atapata chakula chake kwa jasho na mwanamke atazaa kwa uchungu. Kifupi jukumu la mama ni malezi. Kulea watoto na baba yao na baba kutafuta mkate wa familia
 
Suala jingine najiuliza, hii katiba inaweza kuwa applicable kwa wanandoa wote ama kila ndoa iwe na kijikatiba chake
 
kwa juu juu biblia inasema mwanaume atapata chakula chake kwa jasho na mwanamke atazaa kwa uchungu. Kifupi jukumu la mama ni malezi. Kulea watoto na baba yao na baba kutafuta mkate wa familia

kuzaa ndo kulea?

kupika ni kulea? kufua nguo jee? kupiga deki? :smile-big:
 
ulidhani ni starehe tu? Kuna kazi ya kuaminiana, kupendana, kuzaa, kulea watoto n.k. Sasa haya yote yanahitaji mwongozo ulio wazi

Hizo kazi zote nazijua, I meant kama unaomba kuajiriwa? ndo maana kuwe na katiba ya what to do and what not to do! mi nilidhani ndoa ni maisha tu, unaishi kadiri utakavyowezesha, sasa tukianza kupangiana wewe utazaa, mimi nitaleta chakula, etc. ikatokea kuwa umeshinda kuleta chakula siku hiyo, punishment! hujazaa, kwenu................ tutafika kweli?
 
majuzi kuna mkenya mmoja alitengeneza katiba yake kuainisha ni jinsi gani mpangilio wa maamuzi na uwajibikaji vinavyopaswa kuwa ndani ya nyumba. Aliandaa hiyo katiba baada ya kusumbuliwa na wanawake wa awali. Alizungumzia machache kwa ufasaha tu. Swali ni je, kuna haja ya kuwa na maandiko yanayotoa mwongozo wa majukumu ya baba, mama na watoto? Yawezekana ikaleta maridhiano baada ya kila mmoja (wazazi) kusoma, kuridhia na kusaini

kama kwa wengine ndoa ni ndoano hiyo katiba itakuwa ya kizungumkuti
 
Hizo kazi zote nazijua, I meant kama unaomba kuajiriwa? ndo maana kuwe na katiba ya what to do and what not to do! mi nilidhani ndoa ni maisha tu, unaishi kadiri utakavyowezesha, sasa tukianza kupangiana wewe utazaa, mimi nitaleta chakula, etc. ikatokea kuwa umeshinda kuleta chakula siku hiyo, punishment! hujazaa, kwenu................ tutafika kweli?

ukichukulia mambo kiivyo ni sawa na kutumia silika. Lazima kuwe na mipangilio; baba afanye nini na mama afanye nini. Kumsaidia mwingine katika majukumu yake ya kikatiba iwe ni hiari tu
 
kulea ni kuwapa love tu watoto na kuwakatza tabia mbaya ..........manual jobs hazimo kwenye ulezi.

ndio maana matatizo yasiyo na msingi huibuka. Utampaje mtoto au mume mapenzi kama hujayaweka katika vitendo. Mapenzi si nadharia. Mapenzi ni uwajibikaji. Yesu angesema nawapenda upeo kisha akasepa zake bila kupitia yale mateso tungejua anatupenda kiasi gani?
 
kuna masharti na vipengele vyengine havija ainishwa kwenye vitabu vya dini............hapo wanaweza kujianishia wenyewe kwa manufaa yao.

'nani ana jukumu la kupika' inaweza kuwa mfano mmoja tu wa miongoni mwa yasiyo ainishwa kwenye vitabu husika

jamani jukumu la kupika si linajulikana ni la nani?:yield:
 
Back
Top Bottom