Katiba ya CCM vimeo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katiba ya CCM vimeo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mugishagwe, Aug 27, 2006.

 1. M

  Mugishagwe JF-Expert Member

  #1
  Aug 27, 2006
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 295
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ni ilani hii hii ya Mchapakazi kama anavyo itwa na tafiti inataka kutupeleka pabaya wachilia mbali bajeti kuchwangiwa kuna mengi ya kiini macho hapa na yatafumuka siku ndoa na waandishi wa habari ikifa kwa sasa ni sisi tunayaona wananchi wanaona mazuri tuu na haya ngalawa kwenda upande hawaoni maana hakuna wa kuwaripotia . Ilani inatumaliza hii sasa .

  Kanisa lamuonya Kikwete
  KKKT yaungana na TEC kupinga Ofisi ya Kadhi Mkuu
  na Mwandishi Wetu


  KANISA la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) limeionya serikali iachane kabisa na mpango wa kuanzisha Mahakama ya Kadhi Mkuu.


  Kwa kauli laini lakini zenye msimamo thabiti, kanisa hilo limesema uanzishwaji wa mahakama hiyo ni jambo la hatari, na unaweza kuchochea udini.


  Kanisa hilo limetoa onyo pia kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuepuka kutunga sheria ya kuanzishwa kwa Ofisi ya Kadhi Mkuu, kwa maelezo kuwa mahakama hiyo itadhoofisha Katiba ya nchi.


  KKKT pia imevionya vyama vya siasa vinavyotumia hoja ya Kadhi Mkuu kujinadi kwa masilahi ya kisiasa, kwamba vitahatarisha amani, umoja na mshikamano wa kitaifa uliotukuka tangu nchi hii ipate uhuru.


  Msimamo huo wa kanisa hilo kubwa nchini umetolewa mwezi huu katika Baraza la Maaskofu wa KKKT, lililokutana Chuo Kikuu Kishiriki cha Makumira, Arusha.


  Tamko hilo lilisainiwa na Mkuu wa Kanisa hilo, Askofu Dk. Samson Mushemba. Linasema wazi kwamba faida za kutenganisha dini na serikali zimeonekana tangu nchi ipate uhuru; na limehoji sababu zinazowafanya watawala waone kuwa faida hizo hazilifai taifa hili sasa.


  “Tunatambua kwa dhati na fahari kubwa, kuwa serikali yetu haina dini na kwamba huu umekuwa msingi imara wa kuimarisha umoja na mshikamano wa kitaifa. Aidha, tunatambua kuwa serikali yetu na mihimili yake yote muhimu inao wajibu wa kuhakikisha kuna kutenganisha mambo ya dini na mambo ya serikali ili kulinda mshikamano wa kitaifa,” inasema sehemu ya tamko hilo.


  Kwa hatua hii, KKKT linakuwa kanisa la pili kubwa nchini kutoa tamko dhidi ya jitihada za serikali kuanzisha Mahakama ya Kadhi Mkuu.


  Tayari Kanisa Katoliki limeonyesha upinzani mkali dhidi ya mahakama hiyo kwa sababu zile zile zinazotolewa na KKKT, kwamba ofisi hiyo itakuwa chanzo cha vurugu na ubaguzi wa kidini, na mambo ya madhehebu ya dini hayahitaji kutungiwa sheria inayowahusu Watanzania wote.


  Zimekuwapo pia hoja nyingi dhidi ya jitihada hizo za serikali, zikisema iwapo sheria itatungwa kuwaruhusu Waislamu kuwa na mahakama yao, itakuwa imeruhusu utitiri wa mahakama za kidini zinazotambuliwa katika madhehebu mbalimbali ya kidini; na kwamba hali hiyo itadhoofisha mahakama zilizopo zinazotambulika kisheria.


  Wengine wamedai kwamba hili ni jaribio la kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya Kiislamu hatua kwa hatua, jambo ambalo wasingependa Rais Kikwete ahusishwe nalo.


  Katika msimamo wao kuhusu Mahakama ya Kadhi, maaskofu wa KKKT wamehoji msukumo wa serikali inayoongozwa na Rais Kikwete, wakasema unaibua shaka na maswali matatu ya msingi:


  “Tangu tupate uhuru serikali imesisitiza kutokuwa na dini na faida zake tumeziona. Ni kwa faida gani leo, tunalishawishi Bunge letu kutunga sheria ya kuunda Mahakama ya Kadhi?


  “Vyombo vilivyoundwa kwa mujibu wa sheria, huendeshwa kwa kodi ya Watanzania wa dini zote. Ni kwa nini leo hii tunadiriki kujaribu kujadili kuruhusu kisheria, kundi moja la kidini, kuendesha ofisi yake na mahakama yake, kwa kutumia fedha za walipa kodi wote?


  “Je, kuwaundia Waislamu mahakama yao hakutaweka mwanya unaoweza kuwafanya kudai nafasi ya pekee katika utawala wa nchi hii? Na je, mahakama hii itatuhakikishiaje kuwa haki za wanawake zitahifadhiwa?” inasema sehemu ya hitimisho la tamko la maaskofu hao.


  Suala la kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi Mkuu hapa nchini limekuwa likiibuka na kupotea katika medani za siasa kwa zaidi ya muongo mmoja sasa tangu kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa.


  Wapo wanasiasa walioitumia hoja hiyo kama ngazi ya kupandia ili kuvuta hisia za Waislamu.


  Aliyekuwa Mbunge wa Bagamoyo, marehemu Kanali Mohamed Ramia na aliyekuwa Mbunge wa Temeke, Augustine Mrema, waliwahi kurusha kete zao kwa kutumia hoja hii.


  Serikali, katika awamu tatu zilizopita, imekuwa inaipuuza hoja hiyo tangu miaka ya 60. Lakini zipo habari kwamba Awamu ya Nne, chini ya Rais Jakaya Kikwete, imedhamiria kuanzisha Mahakama ya Kadhi Mkuu, kuwaridhisha Waislamu. Alipokuwa anagombea urais mwaka jana, Kikwete aliifanya hoja ya Kadhi Mkuu kuwa mojawapo ya ajenda zake muhimu.


  Bidii hii ya serikali kuanzisha ofisi ya Kadhi Mkuu imewagusa wananchi wengi na kuibua mijadala ya makundi mbalimbali ya wasomi, wanasiasa, viongozi wa dini na wanahabari.


  Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), lilikuwa la kwanza kutoa msimamo wa kupinga na kuionya serikali kuhusu hatua ya kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi Mkuu nchini.


  TEC iliitahadharisha serikali kuwa makini na hoja hiyo, ilimtaka Rais Kikwete aiangalie kwa makini na atoe muda kwa jamii kuijadili kwa kina kabla ya kuitekeleza.


  Siku chache baada ya TEC kutoa msimamo huo, Naibu Mufti, Sheikh Abubakar Zubeir, alikaririwa na vyombo vya habari akieleza kuwa mtu au kikundi chochote kinachopinga kuanzishwa kwa mahakama hiyo, hawatakii mema Waislamu.


  Tamko la Sheikh Zubeir lilifuatiwa na kauli nzito ya viongozi waandamizi watatu wa kanisa walioungana na TEC kupinga kuanzishwa kwa mahakama hiyo huku wakikilaumu Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuliweka suala hilo katika ilani yake ya uchaguzi.


  Viongozi hao waliinyooshea kidole CCM kuwa ni chama chenye wanachama wa dini mbali mbali, hivyo kitendo cha kuingiza katika ilani yake ya uchaguzi suala linalopendelea kikundi kimoja cha dini ni kuhatarisha umoja wa kitaifa na linaweza kuchochea migogoro ya kidini.


  Pia walipinga kuwapo kwa mjadala wowote unaohusu suala hilo bungeni na baadaye kuingizwa kwenye katiba na sheria za nchi.


  Walipendekeza masuala yanayohusu dini yaachwe mikononi mwa waumini wa dini kuyajadili na kufikia muafaka.


  Walieleza wasiwasi wao kuwa iwapo serikali inayoongozwa na CCM italikumbatia suala hilo, itakuwa inajigeuza kundi la madikteta, kwani historia inaonyesha kuwa serikali nyingi zilizojitumbukiza katika mambo ya kidini zimezaa udikteta wa ajabu.


  Agosti 23, Baraza la Ulamaa la Bakwata, nalo liliibuka na kuwashambulia wanaopinga kanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi Mkuu nchini.


  Katika tamko la Baraza hilo lililosomwa kwa waandishi wa habari na Sheikh Mkuu, Issa bin Shaaban Simba, linasema kitendo cha kumzuia mtu au kikundi kutekeleza ibada au kudai na kupata haki yake ni cha uchochezi ambao unaweza kuvunja amani ya nchi.


  Simba alisema baraza hilo linaamini kuwapo kwa Mahakama ya Kadhi Mkuu nchini ni miongoni mwa haki za kimsingi ambazo Waislamu kwa mujibu wa kitabu chao cha Kurani Tukufu, lazima wazipate.


  Mufti Simba alisema kwa muda mrefu Waislamu wamekuwa wakiwavumilia wasiokuwa Waislamu kwa kutowaingilia katika mambo yao na taratibu zao za dini.


  Aliwataka wasiokuwa Waislamu kujenga heshima kwa wenzao na kutambua kuwa Waislamu pia ni sehemu katika jamii ya Watanzania ambao wana haki pia ya kusema, kusikilizwa na kupewa huduma katika nchi yao.


  Lakini hoja ya wanaopinga hoja hii ni kwamba suala hilo libaki kuwa la Waislamu, liwahusishe Waislamu katika taratibu zao za dini, na kama inavyosisitiza KKKT, hoja ya Kadhi Mkuu isitungiwe sheria na Bunge na kulipiwa kodi na Watanzania wote wanaotegemea mfumo wa kisheria uliopo, na unaomhusisha kila mmoja.


  KKKT inasema: “Ufafanuzi uliotolewa kuhusu kazi na wajibu wa Mahakama ya Kadhi umeonyesha kuwa Mahakama hii itashughulikia kufunga ndoa za Kiislamu na kuzihakiki uhalali wake, masuala ya talaka, mirathi, dini (tawheed), ibada na hadhi ya Waislamu.


  “Mambo haya ni ya msingi katika ustawi wa familia na jamii kwa ujumla. Hata kwa ufafanuzi huu, tunatambua kuwa jamii ya Watanzania inazo ndoa mseto, familia mseto na mali zinazomilikiwa kwa misingi ya imani mseto. Mseto huu ni msingi wa mshikamano katika jamii. Uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi utabomoa kwa hakika nguzo hii muhimu ya maridhiano pale matatizo yatakapotokea katika familia husika.”


  Tayari Rais Kikwete anashutumiwa kwa kulibeba suala hili, na kwamba katika miezi michache aliyokaa madarakani, mwenendo wa utendaji wake umeonyesha dalili za kukumbatia udini, huku yeye mwenyewe akiukemea udini katika hotuba zake majukwaani.
   
 2. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #2
  Sep 2, 2006
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  Mzee Busara,

  Heshima yako mkuu, hii thread inahusu Ilani ya CCM kwa mwaka 2005/2006, kuna tread zinazohusu udini huko upande mwingine,

  lakini hiii ni strickly, kuhusu Ilani ya CCM!
   
 3. M

  Mugishagwe JF-Expert Member

  #3
  Sep 2, 2006
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 295
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kwiwikwikwi kama hizi ndiyo busara basi iko kazi sana . You cannot fool us ndugu .
   
 4. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #4
  Sep 3, 2006
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  Mzee Busara,

  Tafadhali nenda kachangie thread ya udini, hiyo jihad yako ipeleke kule Lebanon, kawasaidie ndugu zetu wa Hezbollah kule sio kututisha hapa na dini yako, wewe huoni kuwa hakuna mtu mwenye interest ya ujihad wako hapa!

  Mimi sina muda na mpuuzi kama wewe, huna lolote zaidi tu kutumwa na RO kuja kuchafua hiii forum maana finally tume-hit panapotakiwa, hapa tunaijadili CCM iliyoooza kama alivyosema mwanzilishi wake Mwalimu Nyerere, afadhali mimi nimeeita mazingombwe, yeye alisema ".......imeoza...na itasafishwa na wanachama wenyewe wa ndani ya CCM........." na mimi ni mmojawapo,

  hizo lecture zako za udini peleka huko mjini maana ninaamini unaishi pale Sanamu Monument, kwani si ndio downtown pale au ni Saigon, hivi iko wapi hiyo Saigon/Masikani, anakotoka RO na nyinyi?
   
 5. C

  Chifu Ihunyo Member

  #5
  Sep 3, 2006
  Joined: Jul 3, 2006
  Messages: 62
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mzee Invice

  Ukali wa hoja za Mzee Es ndiyo sasa unaonekana maana hakuna anayekuja mpya akaacha kuhubiri juu ya Es , Sam , Mugishagwe nk . Mzee Es sasa tunazidi kukuamini zaidi maana hoja zako zinawaumiza wengi humu . Endelea kusema na sisi tutakuwa na kazi ya kuchambua pumba na ukweli .Sema tu bwana endelea kutueleza uozo wa pale UK sasa kapewa Mwana Mama .
   
 6. Ogmulik

  Ogmulik Member

  #6
  Sep 3, 2006
  Joined: Jun 4, 2006
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  lugha ambayo isio takiwa ndio hii. Sawa una mtazamo mwingine lakini ni vizuri lugha inakua ya busara

   
 7. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #7
  Sep 3, 2006
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  Wazee Ihunyo na Invicible,

  Heshima mbele wakuu, ninasema wembe ni ule ule! Hawa ninawajua wote kwa karibu hawanidanganyi hawa, ndio maana hawana majibu na uzuri ni kuwa hapa kwenye forum ndio wamekosea kabisaa maana hapa watu wanajua pumba na mchele hata kama vikichanganywa namna gani.

  Nia na madhumuni ni nchi yetu, wala sio personal, na wanunue magazeti na media lakini sisi wananchi tutaendelea kuwalima hapa, bila huruma, hamna cha dini wala Usilamu ni Tanzania yetu, that is all hawawezi waache uongozi wapo wanaoweza tena wengi!

  Mzee Mwanasiasa,

  Ni muda mrefu sasa toka tupate michango ya aina yako bila ya matusi, lakini maneno ni mazito, keep it up!

  Mzeee O,

  Tunasikia kinyaa sana hapa, watu wanapotaka kuleta udini katika issue ambazo ni tatizo lake ni incompetence za viongozi wetu, hakuna mwenye tatizo na dini zao hapa!

  Mzee Q,

  Bravo mzee, umenigusa sana na umasikini wa Mwalimu, na hatukusikia watoto wake wakipelekwa na wazungu huko ulaya, halafu issue ya Mahalu hiyo ni nzito bro, mimi nimeisikia na kuwa ameapa kuwa anasubiri kupelekwa mahakamani ili akamwage ukweli wa yeye alipewa ngapi, na wengine walichukua ngapai kati ya hizo shillingi Billioni tatu!

  Kuna aliyesema kuwa hii ni forum ya upinzani, hapana sio kweli, hii ni objective forum inayochambua ukweli bila huruma, na wala kujali mtu alichaguliwa kwa aslimia 80%! bila ya kuwa na record! Na the best of all, ina watu wenye access to great information za nchi yetu!
   
 8. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #8
  Sep 3, 2006
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,718
  Likes Received: 1,211
  Trophy Points: 280
  Quarz
  Great contribution!
   
 9. S

  Sam JF-Expert Member

  #9
  Sep 3, 2006
  Joined: Jun 6, 2006
  Messages: 416
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  This was deleted.
   
 10. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #10
  Sep 3, 2006
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Ninaomba kueleweshwa hapa juu ya mada hii . Hii mada na mtoa mada nadhani wako so clear lakini majibu ya mada zenyewe haziendani na mada ilivyo. Kwa nini mtu usifungue mada yako ya ubaguzi uendelee kutukana watu huko na utuachie tujadili Katiba na Ilani ya CCM ?.

  Fillga futa hizi post zinaleta chokochoko. Stabd firm linda hii forum watu tutahama hapa kwa maneno kaka haya .
   
 11. S

  Sam JF-Expert Member

  #11
  Sep 3, 2006
  Joined: Jun 6, 2006
  Messages: 416
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mzeeshughuli Bwana
  Kuan mtu anaandika pumba humu nadhani ametumwa kuimaliza hii forum, naingiza mambo wala hayahusiani na topic yenyewe.
   
 12. S

  Sam JF-Expert Member

  #12
  Sep 3, 2006
  Joined: Jun 6, 2006
  Messages: 416
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Busara
  Mimi nimeshaomba msamaha na kufuta matusi yote, sikujua naongea na kichaa. Hapa nilipo nasikitika kupoteza muda wangu. Naomba nionyeshe hiyo post iko wapi niiondoe.
   
 13. S

  Sam JF-Expert Member

  #13
  Sep 3, 2006
  Joined: Jun 6, 2006
  Messages: 416
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Nimefuta kwa sababu nimegundua mtu ninayeongea naye ni kichaa. Kama angekuwa mzima ningeyaacha na nisingeumba msamaha kwa kuongea nilioyoongea nadhani umenipata. Kwa hiyo unaona mimi ni kichaa kwa kutojibu? Naomba nikuelewa hapo.
   
 14. S

  Sam JF-Expert Member

  #14
  Sep 3, 2006
  Joined: Jun 6, 2006
  Messages: 416
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo unataka kusema mimi ni kichaa siyo au na wewe unataka yako.
   
 15. S

  Sam JF-Expert Member

  #15
  Sep 3, 2006
  Joined: Jun 6, 2006
  Messages: 416
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  wastage of time.
   
Loading...