Kwanza lazima uelwe, tofauti ya per capita kati ya Kenya na Tanzania ni $ 560. Huu ni mgawanyo wa kipato chote cha nchi kwa kila mwananchi. Kenya wako $1522 Tanzania tuko $960, PPP Kenya wako $3,360 Tanzania $3,097. Sasa hapo kuna tofauti ya kusema kama Kenya wametuacha mbali sana?? Sidhani kama Kenya inafaa kuwa kipimo chetu cha maendelo. Japo ni wenzetu katika EAC na ni majirani zetu lakini hatutakiwi kutumia Kenya kama kipimo, tulitakiwa kuangalia nchi za mashariki ya mbali kupata hamasa za maendelo.
Wenzetu wa nchi zilizoendelea (Bara la ulaya, bara la Marekani ya kaskazini) wametumia itikadi zote mbili (ubepari na ujamaa) kwa zaidi ya miaka 200. Nchi kama Marekani, chama cha Republican ni chama cha kibepari, Democrat ni chama cha kijamaa. Canada hivyo hivyo, Uingereza ni hivyo hivyo. Wakati sisi tuna kwaruzana ni itikadi gani ndio ina faa kutatuwa matatizo yetu, wenzetu they’re having the best off both sides.
Naona hawa jamaa wa TISS wamekukwaza sana, labda ni swala la sintofahamu. SFO hata kama ikitokea kuwa ni kitengo cha TISS, hawatahusika na mustabali wa kuhakiki mtu yoyote anayetaka kuchukuwa nafasi ya uongozi. Nikuulize swali moja, hivi unaweza kuiona afisa wa SFO ana kakimbizane na magaidi mtaani? There is no connection kati ya watu wanotumika kwenye vetting ya viongozi na watu wanotumika kudhibiti financial crimes. Kwa hiyo hoja yako ya kuwa TISS ndio wamemuweka rais kikwete avurunda uchumi na wao ndio wanamlinda hilo sio kweli. It's kind of funny to hear a Chadema supporter ambao wanasema ni bora ya kikwete kuliko Mangufuli). Na ukumbuke uchumi wetu unakuwa monitored na benki kuu chini ya wizara ya fedha na mipango kuliko watu wa usalama. Na ndio maana benki kuu wanatowa ripoti ya uchumi kila mwezi, kutuhabarisha mustakabali wa nchi yetu.
Mkuu, unapo chukulia kuwa 70% ya watanzania ni below 35yrs of age, lakini ukimbuke kuwa hao 70% ya sio wote wanaoruhusiwa kupiga kura. Wengi katika hilo kundi ni watoto wa chini ya miaka 18 ambao hawaruhusiwi kupiga kura. Uchaguzi wa 2015 ulikiwa na jumla ya wapiga kura millioni 23.3, kati ya hao vijana wa umri wa miaka 18 - 35 walikuwa 57%. Umri wa 36 - 50 walikuwa 25% na zaidi ya umri wa 50 walikuwa 18%. Sasa unafikiri ukawa walipigiwa kura na vijana wote 57%? Ukumbuke kuna wafuasi wangapi wa Ukawa na Chadema walio kasirishwa na kumleta Lowassa na kumuondoa kipenzi chao Slaa? Inajulika dunia zima, vijana wana hulka ya juu sana wakati wa kampeni kabla ya uchaguzi, lakini siku ya kupanga foleni na kupiga kura hawaonekani, hii inadhihirisha kwenye uchaguzi wa 2015. Walioandikishwa ni milioni 23, waliopiga kura million 16, millioni 7 walilala nyumbani bila kupiga kura. Unaona jinsia hao target voters wenu wanavyo waangisha?
Sina tatizo na kuongea kuhisu uchaguzi wa serikali za mitaa, kwanza sina uhakika na 40% unayosema kuwa Ukawa walishinda kulinganisha na 2009. Hebu angalia matokeo kamili hapa chini
CCM yaongoza matokeo ya jumla serikali za mitaa | East Africa Television
Hata kama mmeshida kura au viti vingi so what, kwani nyinyi ni wacongo au wazambia kwamba hamruhusiwi kushinda uchaguzi Tanzania? Japo unasema Lowassa hakusaidia kushinda kwasababu alikuwa bado hajajiunga, lakini ukawa haukusaidia? Even though ukawa ni umoja usio kuwa na uwiano ulio sawa lakini umesahidia sana kuongeza kura kwa upinzani. Tusubiri mwakani kwenye uchaguzi mwingine wa serikali za mitaa tuone kama bado nguvu ya Ukawa inaweza kushindana na CCM.
Kitu ambacho you guys hamkijuwi, CCM ni muajiri mkubwa wa political scientist, research, stratagist, activest na legal advisors. Kazi yao kubwa ni kupitia statistics zote na kujenga hoja ya wapi pakwenda na nini cha kufanya kuwafikia walemgwa.