Katiba ya CCM na Vyombo vya Dola

Katiba ya CCM na Vyombo vya Dola

Ccm ni chama kikongwe kinamuda mrefu katika utawala. Kipo kila kata kitongoji vijijini na mijini. Vyama vya upinzani venyewe viongozi wao wametokana na Ccm. Muundo wa serikali ya nchi umetokana na Ccm. Upinzani wanahitaji rasmali ya watu na uchumi kuifikia Ccm ndio maana Nccr ilivuma sasa almost hakipo wakaja Cuf nao ndio hivyo tena. Sasa Chadema na wao bado wana tatizo kubwa la uchumi na ubunifu. Ndio maana upinzani upo zaidi baadhi miji mikuu hapa nchini ndipo kidogo wana mafanikio. Ccm ina mizizi ndani ya nchi hii viongozi wengi wamepitia Ccm iwe wa kijeshi au kiserikali n.k. tutambue hilo. Ccm kuondoka madarakani sio upinzani ushinde hapana kabisa tena hadi pale Ccm yenyewe ipate migogoro tena mikubwa ndipo viongozi wa ndani ya Ccm tena wawe wengi wajitenge na kuanzisha siasa zenye nguvu za watu kiuchumi n.k. na wajijenge kabla kuanzia kwenye mashina ndipo Ccm inaweza ikashindwa. Illa kwa hali ya sasa Ccm ni chama tawala na kinafaa kuongoza japo kinamapungufu mengi lakini kwa upinzani ulivyo bora ya Ccm. Mwenye kufahamu siasa na historia ya nchi hii atatambua na kuujua ukweli.
Kwa nini CCM inashindwa kutengeneza mazingira sawa ya ushindani ili tujue hayo unayojinasibu nayo yapo au ni porojo? Kwa nini CCM inaua watu wanaoonekana kujenga hoja thabiti mbadala? Kwa nini CCM iko tayari kwa machafuko kuliko kuwakabidhi nchi wapinzani nchi kwa amani?
 
Ni kweli kuwa TISS ni taasisi muhimu sana hapa nchini. Hata hivyo haya uliyoandika hapo umeteleza sana, hiyo sio kazi yao, hizo kwenye red umetumia sana 'hisia za kujipendekeza'. TISS sio Mungu.

Ungekuwa ni afisa usalama wa taifa, ungejua kuwa hizo kwenye red ni kazi za mwenyezi Mungu na hakuna hata moja inayofanywa na TISS. Na kama huwa unasoma misahafu basi kasome Zaburi 127:1-2 pia itakusaidia. Hata hivyo nakielewa sana ninachokuandikia hapa kwa vitendo kabisa. ('practically'.)
mkuu iko hivi nilichokifanya mimi ni kujaribu kugusia umuhimu wa hao watu hata kwa vitu vile "basic" kabisa
ambavyo aliye tajiri au masikini, msomi au asiyemsomi, na chama na asiye na chama ana nufaika navyo, etc na ndio nikatolea mfano wa upatikanaji wa mahitaji hayo au huduma hiyo ya kila siku unategemea msaada mkubwa wa hao wazee wa mstari.
 
kwahiyo TISS wanaona ni sawa nchi iongozwe na majizi ya richmond,escrow,epa,meremeta,deepgreen eti??? tembo malaki wameuawa ndio TISS wanaona ni bora kuliko ukawa??? duuh nchi maskini mwaka wa 50 huu bado umeme maji makazi kilimo elimu afya ni shida ndio unadai TISS wanawataka hao??

shida ni katiba mkuu siku TISS wakitibitishwa na independent body ili wawe free from political influence ndio mwisho wa ccm

ila msitudanganye eti polisi hawashawishiki wakati hujiulizi kura milion 6 (NEC) hakuna hata familia ya mwanajeshi hta mmoja iliowapa kura ukawa???
muhim wekeni tume huru na badilini katiba CCM inatoka mapema sana
Haya ni maoni yako, kwasababu hauna ushahidi wowote wa kuwa ukwawa wanamajibu mbadala ya nchi hii. Wengi walio kuwa ukawa hawajawahi hata kuwa wakuu wa wilaya. Uongozi ni precess, na wala sio kitu cha kuotea.
 
Tiss kazi yake ni kuhakikisha nchi inakuwa salama katika kipindi chote

Unaweza ukaona tiss inaikumbatia ccm lakini huwezi jua kilichopo ndani yake......Vyama vya upinzani vinakosa support kutoka tiss kutokana na kutoeleweka vimekuwa havina agenda maalum....vimekuwa vyama vinavyoongozwa na matukio havina vision yoyote....

Chama cha upinzani kinamchukua mtu huyo huyo aliyekatwa na tiss kutokana na kutokuwa na maadili katika ustawi wa taifa kumsimisha kugombea urais

Kwa kweli upinzani tanzania mkae chini kama mnafaa kupewe nchi hii na sio kuja na vihoja
Rudia kusoma ulichoandika kisha ujitathimini kama fikra zako ziko sawasawa
 
Tangu mwaka 09/12/1961 TANU-CCM ilifunga ndoa na TISS. Baada ya Tanzania kuingia mfumo wa vyama vingi bado CCM na TISS wameendeleza ndoa yao.

Kila lifanywalo hapa nchini Tanzania na TISS hufanywa kwa maslahi ya CCM si kwa maslahi ya Taifa. Wana UKAWA hawawezi kukabidhiwa Nchi ikiwa bado TISS inafanya kazi na kupokea maelekezo yote chini ya vigogo wa CCM ambao ni mkuu wa wilaya, mkuu wa mkoa na mkuu wa nchi hawa makada hufanya vikao, hupokea taarifa zao na wakati mwingine huwaelekeza cha kufanya kwa wakati gani kwa maslahi yao ya kisiasa.

Bashite hadi sasa hajashughulikiwa, huu ni mfano mojawapo kwa namna gani vyombo vya Usalama huelekezwa cha kufanya na CCM kwa maslahi yao ya kisiasa.

Wanasheria na wabunge andaeni hoja binafsi ipelekwe bungeni iangaliwe namna fulani ya kuitenganisha CCM na TISS vinginevyo ikulu UKAWA Mtaendelea kuichungulia kwa nje miaka Yote.

Mungu ibariki Tanzania.
Umezungumza ukweli ambao haupingiki. Vyama vya upinzani lazima vifanye ya ziada ilikuweza kuongoza nchi. Ukianzia tume ya uchaguzi pia sio huru. Uchaguzi ujao bila tume huru ni afadhari wasishiriki uchaguzi
 
Umezungumza ukweli ambao haupingiki. Vyama vya upinzani lazima vifanye ya ziada ilikuweza kuongoza nchi. Ukianzia tume ya uchaguzi pia sio huru. Uchaguzi ujao bila tume huru ni afadhari wasishiriki uchaguzi
Mkuu unawaza kama mimi ,huwa natamani wasishiriki hata chaguzi ndogo kama Hakuna tume huru ili washiriki wao wenyewe
 
kule ukawa tulipochukua majimbo na kata, hawakuwepo hao wazee wa unanijua mimi ni nani!
 
Sasa kama mwajua hazikosekani, Je Nini kipi cha kufanyika pindi unapokutana na mchanyato kama huo..?? Maana watanzania wengi ni watu wa kupenda kudandia mambo juu juu bila ya ufahamu wa kutosha wa jambo husika.
kuna namna ya kuchambua chuya,,hapo ndipo kuna tofauti
 
Hao wote uliowataja kama mngekuwa na hoja madhubuti na thabiti za kuweza kuwa shitaki kwa yale wanayo yafanya
basi mbona milango ya mahakama iko wazi , kwani mahakama ni chombo huru na cha hak kwa wote, no one is above the law.
The law doesnt work to the people in power and the law doesnt work to people with money except manji ...lol
 
Hata hao Tiss wakijitenga na ccm bado sana wapinzani kupewa nchi hii siyo ya majaribio wewe watu gani hawaeleweki wanasimamia nini ili mradi tu kuenenda na matukio
Ebu kuwa na fikra huru basi ili uweze kujitofautisha mjinga na mpumbavu
 
Kuna watu wanavichwa vigumu sana wakati hali halisi wote tunaijua sijui ni nidhamu ya uoga au kujipendekeza? Tupo kwenge vyama vingi lakini sheria nyingi na mifumo mingi bado ni ya chama kimoja hilo lipo wazi halihitaji shule. Pili huwezi kumjudge dereva huyu mbovu wakati hujampa Gari aendeshe hata mara moja.

NB: Ili tuendelee ni wakati sasa wakuachia siasa za ushindani wa hoja zipate nafasi, na hii inawezekana kama baadhi ya vyombo kama TISS, polisi n.k vifanye kazi kwa maslahi ya taifa au kwa kukidhi haja ya vyama vingi na sio kimoja, TUME HURU YA UCHAGUZI wote ni mashaihid tume yetu inavyofanya vituko atakayekataa atakua anaishi abroad 'rejea alichosema pole pole kama CCM itakubali kuundwa kwa tume hutu nn kitatokea', SP Separation of power pia ni sehemu muhimu sana kwa kila muhimili kuwa watchdog wa mihimili mingene na Kupunguzwa kwa madaraka ya mkuu.

Yote haya yanakibeba chama kilicho madarakani sometimes huwa natoa salute kwa wapinzani maana wanafanya siasa katika mazingira magumu lakini still wanapambana na wanazidi kujiongezea viti bungeni.. ni muda tu hope yote haya yatakwisha

'jiwe jeusi'
 
Issue sio kupewa like ila hapa ni kueleza upande wa pili wa shilingi.

By the way kwani hii mada inahusu mashindano ya kupewa like ..??? ufafanuzi pls.
Basi sawa...punguza povu mkuu,nimeona tayari ushapewa like.
 
Mnatapatapa aiseeee!!!usalama kwanza !! Vyama baadaye!! Sikiliza kwanza: siku mkiacha kutafuta madaraka kwa njia za kishetani hata Mungu atawafikilia kuwapa uongozi Wa nchi!!
 
Tukubaliane kitu kimoja, upinzani mmeshindwa kuwashawishi TISS, Jeshi, Polisi hata umaa kwa ujumla kama mko tayari kubeba mzigo wa Tanzania, hili sio jambo lililo fichika.

TISS ina majukumu mengi, moja kati ya majukumu yao, ni kulinda ustawi wa hii nchi. Leo hii nchi ya amani na utulivu, ichukuliwe na watu wasiojielewa mwisho wa siku hakuna Tanzania wala amani.

Jipangeni kwanza ndio muaminiwe.


Precisely..Upinzani wameshindwa kuwaaminisha TISS kwamba wanatosha

Kichekesho ni pale mtu anakuwa vetted out na TISS alafu ninyi mnamchukua mkitegemea atashinda

Poor Minds
 
Precisely..Upinzani wameshindwa kuwaaminisha TISS kwamba wanatosha

Kichekesho ni pale mtu anakuwa vetted out na TISS alafu ninyi mnamchukua mkitegemea atashinda

Poor Minds

Hapo kwenye vetting ndio watu wengi hawapajuwi, wanafikiri watu wanateuliwa kiholela.
 
Precisely..Upinzani wameshindwa kuwaaminisha TISS kwamba wanatosha

Kichekesho ni pale mtu anakuwa vetted out na TISS alafu ninyi mnamchukua mkitegemea atashinda

Poor Minds
Kwa hiyo unathibitisha kwamba TISS hufanya vetting ndani ya CCM.
Kama vetting zenyewe ni za aina ya watu kama Bashite wanaoaminiwa basi kama Taifa tumekwisha
 
Back
Top Bottom